.

CHUO CHA UDEREVA CHA NYATO'S CHAWATUNUKU VYETI MADEREVA WALEMAVU 19

Aug 31, 2016

 Mkuu wa Usalama Barabarani Wilaya ya Ilala, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Peter Mashishanga (kulia), akimkabidhi cheti, Mpoki Mwasunga, baada ya kuhitimu mafunzo ya udereva ya mwezi mmoja katika chuo cha udereva cha Nyato's kilichopo Majohe Bomba mbili Manispaa ya Ilala Dar es Salaam leo. Wahitimu 19 ambao ni walemavu walihitimu mafunzo hayo.
 Mkurugenzi wa shule hiyo Wilfred Nyato (kulia), akizungumza kwenye hafla hiyo.
 Mkuu wa Usalama Barabarani Wilaya ya Ilala, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Peter Mashishanga, akiangalia  alama ya usalama barabarani. Kushoto ni Mwenyekiti wa Taifa wa Kamati ya Taifa ya Usalama Barabarani kwa watu Wenye Ulemavu, Kabateke Jutoram na Mkurugenzi wakitengo cha Elimu kwa Umma kikosi cha Usalama barabarani nchini,Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP),Mossi Ndozero.
 Wahitimu wakiwa kwenye hafla hiyo.
Mshairi, Kiiza Amani akitoa burudani kwenye hafla hiyo.
 Mkuu wa Usalama Barabarani Wilaya ya Ilala, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Peter Mashishanga (katikati), akihutubia kwenye hafla hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Taifa wa Kamati ya Taifa ya Usalama Barabarani kwa watu Wenye Ulemavu, Kabateke Jutoram na Mkurugenzi wakitengo cha Elimu kwa Umma kikosi cha Usalama barabarani nchini,Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP),Mossi Ndozero.
Mkurugenzi wakitengo cha Elimu kwa Umma kikosi cha Usalama barabarani nchini,Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP),Mossi Ndozero, akitoa neno kwenye mkutano huo.H
 Mkuu wa Usalama Barabarani Wilaya ya Ilala, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Peter Mashishanga (kushoto), akimkabidhi cheti, mhitimu, Subira Semsimbazi.
Hapa James Hizza akipokea cheti chake.
Sikujua Mbwembwe, akikabidhiwa cheti chake.
Wahitimu wakionesha vyeti vyao.
Stafu Sajeni, Enock Machunde akitoa darasa kwa hitimu hao kuhusu sheria za usalama barabarani.
Koplo, Faustina Ndunguru, akizungumza kwenye mkutano huo.

Na Dotto Mwaibale

WATU Jamii ya walemavu ambao ni maderava wa vyombo vya moto wametakiwa kujitokeza kwenye shule mbalimbali za udereva ili kupata mafunzo ya udereva ikiwa pamoja na kupata leseni kabla ya kutumia vyombo hivyo.

Wito huo umetolewa Dar es Salaam leo na Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa kipolisi wa Ilala,Peter Mashishanga wakati akiwatunuku vyeti walemavu 19 ambao wa mefunzo ya mwenzi mmoja katika shule ya udereva ya Nyato's iliyopo Majohe Bomba mbili Manispaa ya Ilala.

Alisema kuwa ipo haja ya walemavu ambao wanamiliki vyombo vya moto na kuendesha vyombo hivyo kabla hawajaingia barabarani ni vema wakapata mafunzo ya kujuwa alama,kanuni na sheria za usalama barabarani.

"Ni muhimu kwa kundi hili ambalo leo mmepata vyeti vya kuhitimu mafunzo ya udereva kwenda kuwa mabalozi kwa wengine ambao hawajapata fursa ya kupata mafunzo kama  nyie kwenda  kuwahamasisha ili wajiunge katika vyuo vya udereva ikiwamo chuo hiki cha Nyato's ambacho kimeaza mpango wa kutoa mafunzo haya kwa nchi nzima kwa kushirikiana Kamati ya Taifa ya Usalama Barabarani kwa watu Wenye Ulemavu."alisema Mashishanga

Aidha aliwaeleza wahitimu hao kuwa wahakikishe  wanakwenda kupata majaribio kwa wa kufunzi wa kikosi cha Usalama barabarani ili wapate leseni zitakazo wafanya waweze kuendesha vyombo vya vya moto.

Kwaupande wake Mkurugenzi wakitengo cha Elimu kwa Umma kikosi cha Usalama barabarani nchini,Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP),Mossi Ndozero alisema kuwa ni muhimu kwa wahitimu hao kwenda kuzingatia sheria za usalama barabarani ikiwa pamoja na kuvaa kofia ngumu,na kutozidisha abiria.

Naye Mkurugenzi wa shule hiyo Wilfred Nyato alishukuru kwa ushirikiano uliopo kati ya   Jeshi hilo na taasisi yake ambapo pia ametoa  ofa ya kusoma bure kwa mlemavu Thomas Kone ambaye hivi karibuni alipata msaada wa bajaji kutoka kwa Rais Dk. John Magufuli.

Nyato alisema kuwa kimeazisha mpango wa kutoa mafunzo  ya udereva kwa kushirikiana na kamati ya  Taifa ya usalama kwa watu wenye ulemavu kwa lengo la kukabiliana na matukio ya ajali za barabarani.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU NCHINI WATAKA SERIKALI KUTOWAONA WACHOCHEZI KATIKA JAMII

Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Victoria magharibi, Mayigi Makobela, akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo ya Watetezi wa Haki za Binadamu yanayofanyika Jijini Mwanza.
Na George Binagi-GB Pazzo @BMG
Serikali imeshauriwa kutoa ushirikiano kwa watetezi wa haki za binadamu ili kurahisisha utendaji kazi wao badala ya kuwaona watetezi hao kama wachochezi katika jamii na wakati mwingine kuwafungulia mashitaka.

Ushauri huo umetolewa hii leo Jijini Mwanza na Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, Onesmo Olengurumwa, kwenye mafunzo ya siku tatu kwa watetezi wa haki za binadamu kutoka mikoa mbalimbali nchini.

Amesema katika baadhi ya maeneo kama Loliondo mkoani Arusha kwenye mgogoro wa ardhi kati ya wananchi na mwekezaji, watetezi wa haki za binadamu wamechukuliwa kama wachochezi na kufunguliwa mashitaka jambo linalosababisha baadhi yao kushindwa kutekeleza majukumu yao na wengine kuacha kabisa shughuli za utetezi.

Akifungua Mafunzo hayo, Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Victoria magharibi, Mayigi Makobela, amesema serikali itaendelea kuwaelimisha wachimbaji wadogo ili waifahamu vyema sheria ya madini namba 4 ya mwaka 2010 ili kupunguza migogoro iliyopo na kwamba imetenga zaidi ya hekta elfu 12 kwa ajili ya wachimbaji wadogo wadogo wa madini.

Pia amesema serikali imetenga shilingi bilioni 6.6 kwa ajili ya ruzuku kwa wachimbaji wadogo na kuwahimiza kujiunga kwenye vikundi ili wapatiwe ruzuku hiyo.

Baadhi ya washiriki wamesema mafunzo hayo yatawasaidia kuimarisha utendaji wao wa kazi jambo litakalowasaidia kutimiza vyema wajibu wao katika jamii bila kuonekana wachochezi huku pia wakiwa katika upande salama dhidi ya maisha yao.
Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Victoria magharibi, Mayigi Makobela, akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo ya Watetezi wa Haki za Binadamu yanayofanyika Jijini Mwanza.
Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Victoria magharibi, Mayigi Makobela, akizungumza na wanahabari nje ya Mafunzo ya Watetezi wa Haki za Binadamu yanayofanyika Jijini Mwanza.
Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, Onesmo Olengurumwa, akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo ya Watetezi wa Haki za Binadamu yanayofanyika Jijini Mwanza.
Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, Onesmo Olengurumwa, akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo ya Watetezi wa Haki za Binadamu yanayofanyika Jijini Mwanza.
Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, Onesmo Olengurumwa, akizungumza na Wanahabari nje ya ufunguzi wa Mafunzo ya Watetezi wa Haki za Binadamu yanayofanyika Jijini Mwanza.
Mmoja wa washiriki wa semina hiyo akihojiwa na wanahabari
Miongoni mwa washiriki wa semina hiyo akihojiwa na wanahabari
Mmoja wa washiriki wa semina hiyo akihojiwa na wanahabari
Washiriki wa Semina
Mwonekano kwenye semina
Picha ya pamoja

RAIS DK. SHEIN AWAAPISHA WATEULE WAKE IKULU YA ZANZIBAR LEO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha ACP Sida Mohamed Himid kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, anayeshuhulikia Idara Maalum za SMZ,katika  hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo Agosti 31, 2016. (PICHA NA IKULU YA ZANZIBAR)

 Rais Shein  akimkabidhi vitendea kazi ACP Sida
 Rais akisaini kiapo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Nd,Hassan Khatib Hassan  kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto,atayeshuhulikia masuala ya Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto,katika  hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
Baadhi ya Mawaziri wa Wizara za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Viongozi katika taasisi mbali mbali walioteuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe,Zubeir Ali Maulid (kulia) na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe,Omar Othman Makungu ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Viongozi wa Taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja

Makamanda Wakuu wa Vikosi vya SMZ walihudhuria katika hafla ya kuapishwa Viongozi wa taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi, walioteuliwa na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja

WAPENDA AMANI NCHINI WALAANI TAMKO LA JUKWAA LA WAHARIRI.


Na Sheila Simba-Dar es salaam.

Wapenda amani nchini wamelaani kitendo cha Jukwaa la Wahariri (TEF)kutoa tamko dhidi Serikali kuhusu kufungia vituo viwili vya redio hivi karibuni.

Wakiongea kwa nyakati tofauti Jijini Dar es Salaam, wameonyesha Dhahiri kuchukizwa na TEF na kusema hawajui wanalolifanya.

Bwana Juma Ramadhan, Mkazi wa Ilala, amesema kuwa hapendezwi na watu kutetea chombo kinachohatarisha amani Nchi na mali zao kwa kuandika habari za uchochezi.
“Mimi nimekaa nchini kwa kipindi kirefu sijaona machafuko je huyu anayechochea uvunjifu wa amani ana lengo gani kwa Taifa?”, aliuliza Ramadhani

Naye  Bi Mercy Mwakitalima Mkazi wa Sinza, amesema kuwa Jukwaa hilo linapaswa kusimamia na kuongoza vyombo wanavyosimamia kutokutumia maneno na lugha isiyofaa ili kuepeka kuliingiza taifa katika machafuko.

Ameongeza kuwa wahariri wanapaswa kusimamia maadili ya uandishi wa habari ili vyombo vyao viandike habari zinazingatia umoja kitaifa uliojengeka kwa muda mrefu.

“Taifa letu ni la amani na inatakiwa kulindwa kwa gharama yoyote,naviomba vyombo vya habari nchini kuheshimu sheria za Nchi,ki ukweli siku hizi baadhi ya vyombo wanaongea sana vitu ambavyo havina faida yoyote kwa jamii, naipongeza Serikali kwa hatua waliochukua ili iwe fundisho kwa wengine”alisema Mwakitalima

Ameongeza kuwa sekta ya habari nchini inatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuhubiri amani na sio kutumia maneno yanayochochea uvunjifu wa amani kwani kufanya hivyo kutapelekea Taifa pabaya kwa kuwalisha watanzania vitu visivyofaa.

Kwa upande Mwalimu wa shule ya Msingi Kinondoni aliyejitambulisha kwa jina moja la Mwamvua,ameiomba Serikali kuharakisha Muswada habari ili kuwa na watu wenye sifa pekee katika sekta ya habari kwani kwasasa sekta ya habari imepoteza umaarufu wake.

“sekta ya habari nchini kwa sasa haina mwelekeo kila mtu ni mwandishi wa habari bila hata kuwa na taaluma ya habari hili ni tatizo lazima Serikali ilifanyie kazi mapema ili kuepeuka kuwa na watu wasiojua maadili ya kazi hiyo,”alisema Mwamvua.

Naye Joseph Jeremia ameomba Serikali kuendelea kuvichukulia hatua vyombo vya habari ambavyo vinamwelekeo wa kuhatarisha amani ya Tanzania kwa kuvifuta kabisa.

Amesema amani ni rahisi kuipoteza lakini ni kazi ngumu kuijenga kama ilivyo hapa nchini.

Jukwaa la wahariri walitoa tamko hilo, kufutia Serikali kupitia kwa Waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo Nape Nnauye, kutangaza kufungia vituo viwili vya radio kwa kutangaza habari za uchochezi,ambazo ni Radio five ya Arusha na Radio Magic fm ya jijini Dar es salaam.


MAPITIO YA MAGAZETI CHANNEL 10, TBC1 NA MLIMANI TV, LEO AGOSTI 31, 2016

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI WANYAMA NJE YA NCHI.

Mhe. Prof. Jumanne Maghembe, Waziri wa Maliasili na Utalii

Na Hassan Silayo
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe amesema kuwa serikali imepiga marufuku biashara ya kusafirisha wanyama hai nje ya nchi mpaka pale itakapowekwa misingi mizuri ili nchi iweze kunufaika na biashara hiyo.

Prof. Maghembe ameyasmea hayo wakati wa kipindi cha TUNATEKELEZA kinachoandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO na TBC 1 ambapo alisema Serikali iliamua kuangalia upya utaratibu huo wa kuuza wanyama hai na kuamua kusitisha biashara hiyo hadi pale taratibu na misingi mizuri ya biashara hiyo itakapowekwa.

“Ni kweli kulikuwa na utaratibu wa kuuza wanyama hai nje ya nchi bila kuiwezesha nchi kupata faida yoyote ile, hivyo kwa sasa kama nchi tumeamua kupiga marufuku biashara kwa maslahi ya taifa”.

“Haiwezekani uuze wanyama hai nje halafu anayenufaika ni yule anayenunua na kuiacha nchi bila faida yoyote ya uwepo wa maliasili hiyo, hivyo kama nchi tumeamua kupiga marufuku biashara hiyo hadi pale misingi mizuri ya kibiashara itakapowekwa na kuiwezesha Tanzania kunufaika na rasilimali zake, na nisisitize kwa sasa hata Chawa wa Tanzania hataweza kusafirishwa nje ya nchi”. Alisema Prof. Maghembe.

Aidha, Prof. Maghembe alisema kuwa kwa sasa Serikali imeweka mikakati madhubuti ya kupambana na ujangili wa wanyama pori kama Tembo na Faru ikiwemo kukamata watu wote wanaohusika katika biashara hiyo na mpaka sasa wameshakamata  baadhi ya watu akiwamo mwanamama anayejiita malikia wa pembe za ndovu ambaye alikuwa kinara katika biashara hiyo.

Prof. Maghembe aliongeza kuwa hatua hiyo imeonesha mafanikio kwani kwa kipindi cha hivi karibuni soko la mauzo ya pembe za ndovu nje nchi hasa bara la Asia ambao ndio walikuwa wanunuzi wakubwa wa bidhaa hizo yameshuka na hatua hiyo inatokana na mikakati iliyowekwa na Serikali.

Akizungumzia wizi katika mazao ya misitu Prof. Maghembe alisema kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua za kupambana na wizi wa mazao ya misitu na imekubaliwa kuwa iwapo gari litakamatwa likiwa na mazao hayo bila kuwa na kibali, Serikali itataifisha gari hilo na wahusika watashtakiwa kama wahujumu uchumi.

Pia Prof. Maghembe alisema kuwa kwa sasa utawekwa utaratibu wa magari yote yanayobeba mazao ya misitu kusafiri mchana kwenye gari lililo wazi ili kurahisisha ufuatiliaji na udhibiti wa wizi huo.

Serikali imeahidi kuanzisha miradi ya ufugaji nyuki kwenye vijiji vilivyo pembezoni mwa misitu ili kuweza kudhibiti uchomaji moto kwenye kwenye maeneo hayo hali itakayowezesha pia utunzaji wa mazingira

MAGAZETI YA NDANI NA NJE YA TANZANIA LEO, AGOSTI 31, 2016
TANZANIA


ยช