.

WAREMBO 30 MISS TANZANIA WATINGA KAMBINI LEO, WAPEWA SOMO LA AWALI NA MISS TANZANIA WA SASA

Sep 30, 2016

Baadhi ya Washiriki watakaowania Taji la Miss Tanzania 2016 wakiwa katika picha pamoja muda mfupi baada ya kuwasili kambini. Jumla ya Washiriki 30 kutoka kanda mbalimbali nchini wameingia Kambini leo Septemba 30, 2016 tayari kwa maandalizi ya Shindano hilo linalotarajiwa kufanyika mwishoni mwa Mwezi ujao.
Mrembo anaeshikilia Taji la Miss Tanzania kwa sasa, Lilian Kamazima akizungumza na Warembo alipokutana nao leo Septemba 30, 2016 kwenye Hoteli ya Regency, Jijini Dar es salaam. ambapo jumla ya Washiriki 30 wameingia kambini leo tayari kwa maandalizi ya Shindano hilo linalotarajiwa kufanyika mwishoni mwa Mwezi ujao.


Baadhi ya Washiriki wa Miss Tanzania 2016 wakimsikiliza kwa makini Mrembo anaeshikilia Taji la Miss Tanzania kwa sasa, Lilian Kamazim.
 Warembo wakifanyiwa Usaili na viongozi wa Miss Tanzania.

TANESCO YAFANYA KIKAO CHA UJIRANI MWEMA NA VIONGOZI WA JAMII INAYOZUNGUKA VITUO VYA KUFUA UMEME WA GESI VYA KINYEREZI JIJINI DAR ES SALAAM

 Meneja wa Kituo cha kufua umeme kinyerezi I, Mhandisi Lucas Busunge, akifungua kikao cha ujirani mwema kati ya TANESCO, TPDC na viongozi wa jamii inayozunguka Vituo vya kufua umeme wa Gesi vya Kineterezi jijini Dar es Salaam Septemba 30, 2016.
 Mkuu wa Kitengo cha Usalama, TANESCO Makao makuu, Misana Gamba

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
SHIRIKA la Umeme nchini TANESCO na viongozi wa dini, vyombo vya dola na viongozi wa Serikali za Mitaa sita inayozungu vituo vya kufua umeme wa Gesi asili vya Kinyerezi jijini Dar es Salaam, wamekubaliana kuweka mikakati ya pamoja kuhakikisha jamii inashiriki katika ulinzi wa miundombinu ya umeme.
Makubaliano hayo yamefikiwa leo Septemba 30, 2016, kwenye kikao cha ujirani mwema kati ya TANESCO, TPDC, viongozi wa dini, viongozi wa serikali za mitaa na vyombo vya dola ili kujadili namna bora ya kulinda miundombinu ya umeme kwenye vituo hivyo.
“Umeme wa Gesi ni umeme salama kabisa, hata hivyo ni wajibu wetu kushirikiana pamoja kuhakikisha miundombinu ya umeme huu wa Gesi inatunzwa na kulindwa,”, Meneja wa Kituo cha Umeme Kinyerezi I, Mhandisi Lucas Busunge alianza kwa kusema wakati akiwakaribisha wajumbe kwenye kikao hicho.
Tumeona tuitane hapa leo ili tujadiliane pamoja namna bora ya kuhakikisha umeme huu utokanao na Gesi ambao Serikali imeiingia gharama kubwa, miundombinu yake inalindwa na nyinyi viongozi mnao wajibu mkubwa wa kuwafikishia ujumbe wananchi wanaoishi maeneo yanayozunguka mitambo hii. Alisema Mhandisi Busunge.
Akitoa mada juu ya Mambo yanayoweza kusababisha uharibifu wa miundombinu ya umeme wa Gesi na hasara inayoweza kulikumba taifa na jamii kwa ujumla, Mkuu wa Usalama wa TANESCO makao makuu, Misana Gamba alisema, “Lazima tutambue kuwa Serikali imewekeza fedha nyingi katika ujenzi wa vituo hivi na fedha hizi ni za walipa kodi wa Tanzania, kwa hivyo ni wajibu wetu sote na sio TANESCO pekee kuhakikisha tunalinda miundombinu hii kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo,” alisema Gamba
Akifafanua zaidi, Mkuu huyo wa usalama alibainisha mambo ambayo jamii inapaswa kuelewa kuwa ni hatari dhidi ya miundombinu ya umeme ambayo ni pamoja na kuwasha moto, kulima au kuchimba mchanga, mmomonyoko wa udongo, wezi wa vyuma, uvuvi haramu, kujenga, kufanya biashara au kuendesha magari makubwa sehemu ambayo miundombinu hiyo ya umeme wa Gesi inapita.
Mkuu huyo wa usalama wa TANESCO alisema, hatari inayoweza kutokea endapo mambo hayo yatafanywa ni pamoja na kurudisha nyuma jiyihada za Serikali katika kuwaletea umeme wananchi, lakini pia hatari ya kulipuka kwa mitambo hiyo ambapo madhama makubwa yanaweza kuwakumba wananchi.
Akichangia kwenye mazungumzo hayo, Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji, ambaye ndiye alikuwa muendesha kikao, alisema, Shirika la Umeme Tanzania, TANESCO, imekuwa ikitoa elimu kwa umma juu ya umuhimu wa kutunza miundombinu ya umeme kwa faida ya Watanzania wote, na hatua ya kikao hicho ni mwendelezo wa utoaji elimu na kuwataka viongozi hao kuwa mabalozi katika maeneo yao, kwenye nyumba za ibada, ili kusudi wananchi wengi waelewe umuhimu wa kuunza miundombinu ya umeme ambayo kimsingi ni mali ya Watanzania wote.
Naye afisa mwandamizi wa usalama Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini, (TPDC), Elias Muganda, alitahadharisha juu ya shughuli za kiuchumi kwenye eneo linakopita bomba la Gesi na ksuema hiyo ni hatari. “Kwa sasa kuna mabomba mawili yenye Gesi tayari, ambayo yako umbali wa mita 2 kwenda chini, yakipata mgandamizo unaosababishwa na magari makubwa kupita juu yake inaweza kupelekea leakge na kusababisha Gesi kuvuja na matokeo yake kila mtu anayajua ni moto.” Alifafanua
Akatoalea mfano wa mabomba yaitwayo Carthodic Protection, ambayo huzuia kutu, lakini tayari kuna watu wanang’oa vyuma hivyo na hii inaweza kusababisha kutu na mabomba kutoboka,alitahadharisha, Muganda.
Wakichangia mazungumzo hayo, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kanga, Shamte Mlanzi Mkali, alitoa wito kwa viongozi wenzake wa Mitaa, kila wanapokutana kwenye vikao, moja ya ajenda ya kuzungumza ni pamoja na usalama wa mitambo ya Gesi.
Hata hivyo viongozi wengi walionyesha umuhimu wa TANESCO kutoa ajira kwa vijana waishio maeneo ya jirani na mradi ili waweze kuona manufaa ya moja kwa moja ya ujio wa mradi huo.
Mambo yaliyoazimiwa kwenye kikao hicho ni pamoja na ulinzi wa miundombinu ya Gesi iwe ni moja ya ajenda za vikao vya Serikali za Mitaa, na iwe marufuku kwa mtu kupita au kukatiza eneo la Mitambo bila ya kibali maalum, uwepo utaratibu wa kuwaalika viongozi wa TANESCO/TPDC kwenye vikao vya Serikali za Mitaa kama itahitajika.
Maazimio mengine ya kikao hicho kilichomuhusisha pia Mkuu wa upelelezi wa Kituo cha Sitakishari-Ukonga,  SSP, Hassan Okello, ni pamoja na kampuni za ulinzi kwenye eneo la mitambo zijulikane kwa viongozi wa Serikali za mitaa yote inayozunguka eneo la mradi.
Mitaa iliyoshiriki kwenye kikao hicho ni pamona na Mtaa wa Kanga, Kibaga, Kinyerezi, Kichangani, na Kifura.

 Mhandisi Busunge
 Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji (aliyesimama), akizungumzia umuhimu wa viongozi wa mitaa kushirikiana na TANESCO katika kuelimisha umma, kutunza miundombinu ya umeme
 Afisa Usalama wa TANESCO makao makuu, Fidelis Almasi, akielezea namna viongozi wanavyoweza kushiriki katika kuelimisha wananchi umuhimu wa kutunza miundombinu ya umeme na athari za zitokanazo na uharibifu wa miundombinu hiyo kwa jamii na serikali
 Mkuu wa upelelezi, Kituo cha polisi Sitakishari-Ukonga, MrakibuMsaidizi wa Polisi, (ASP), Hassan Okello, akiwatoa hofu viongzoi hao kuhusu kutunza siri wanapotoa taarifa za wahalifu na uhalifu na kwamba yeye binafsi yuko tayari siku zote kuhakikisha usalama kwenye eneo hilo unazingatiwa
 Afisa Usalama Mwandamizi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini, (TPDC), Eliasi Muganda, amesema, mabomba mawili ya gesi tayari yana gesi na yako umbali wa kina cha mita 2 kutoka uso wa ardji na hivyo hayahitaji mgandamizo kutoka juu kwani ni hatari yanaeza kupata nyufa na kuvujisha Gesi

 Afisa Elimu wa Kata ya Kinyerezi, Mwalimu Mercy Mtei, (kulia), yeye amesema, atawashirikisha walimu na wanafunzi kueneza ujumbe kwenye jamii
 Sheikh Juma Swaleh wa Msikiti wa Othman Bin-Afan wa Kinyerezi
 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kichangani, Niyukuli Leonard (kulia)
 Mchungaji Jacob Msami,  akizungumza
 Ustaadhi Ally akizungumza
 Mchungaji Ariel Mungereja wa Kanisa la EAGT, Kinyerezi
 Afisa Usalama wa Kituo cha Kinyerezi I, Furaha Munisi, akifafanua mambo mbalimbali ya kiusalama ambayo viongozi hao wanapaswa kuyachukua na kuwaelimisha wananchi
Picha ya pamoja baada ya kikao

WAZIRI MKUU MAJALIWA KASSIM MAJALIWA AHAMIA RASMI DODOMA, LEO DESEMBA 30, 2016

 Waziri Mkuu akiwapungia viongozi na wananchi wa mkoa wa Dodoma alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma leo Septemba 30, 3016
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakisalimiana na Madiwani wa Manispaa ya Dodoma baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Septemba 30, 2016.
Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa na mkewe Mary wakiagana na watuimishi wa Makazi ya Waziri Mkuu ya Dar es salaam kabla ya kuondoka kuelekea Dodoma Septemba 30, 2016.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokewa na Meya wa Manispaa ya Dodoma Jafar Mwanyemba na viongozi wengine wa mkoa huo
 
Waziri Mkuu, Kasim Majliwa akiwapungia wananchi baada ya kuwasili kwenye makazi yake mjini Dodoma Septemba 30, 2016.
Meya wa Manispaa ya Dodoma, Jafar Mwanyemba, (kushoto), akimkabidhi mfano wa funguo, Waziri Mkuu KassimMajaliwa, ikiwa niishara ya kumkaribisha Dodoma kama mkazi wa Manispaa hiyo, alipowasili kwenye makazi yake mjini humo Septemba 30, 2016.Waziri Mkuu ametimiza ahadi yake ya kuhamia Dodoma aliyoitoa bungeni ifikapo mwishoni mwa mwezihuu.
 Waziri Mkuu akionyesha funguo hiyo yamfano baada ya kukabidhiwa
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wazee wa Dodoma  baada ya kukaribishwa kimira na wazee hao Septemba 30, 2016
Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa akizawadiwa kimira  na wanawake wa Dodoma ikiwa ni ishara ya kumkaribisha karika Manispaa hiyo, Septemba 30, 2016
Viongozi wa Manispaa na wananchi wakishangilia ujio wa Waziri Mkuu

MAKAMU WA RAIS WA BARAZA LA TAIFA LA CUBA KUWASILI NCHINI OKTOBA 2, 2016

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu ziara ya Makamu wa Rais wa Cuba Nchini, Mhe.Salvador Antonio Valdes Mesa anayetarajiwa kuwasili nchini kwa ziara ya siku tatu kuanzia tarehe 2 hadi 4 Septemba 2016.
Mhe. Waziri Mahiga akiendelea kuzungumza na Waandishi wa Habari kama wanavyoonekana pichani. =============================================

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ziara ya Makamu wa Rais wa Cuba nchini Tanzania
Makamu wa Rais wa Baraza la Taifa la Jamhuri ya Cuba, Mhe. Salvador Antonio Valdes Mesa anatarajiwa kuwasili nchini tarehe 02 Oktoba, 2016 kwa ziara rasmi ya siku tatu. Lengo la ziara hiyo ni kukuza na kuimarisha uhusiano wa kihistoria uliopo baina ya Tanzania na Cuba pamoja na kuangalia maeneo mapya ya ushirikiano. Nchi nyingine anazotarajiwa kuzitembelea ni pamoja na Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Botswana na Zimbabwe.
Shughuli mbalimbali zitakazofanyika wakati wa ziara
Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Mhe. Valdes Mesa atapokelewa na mwenyeji wake Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Tarehe 03 Oktoba, 2016 Mhe. Mesa atakutana kwa mazungumzo ya faragha na Mhe. Samia Suluhu Ikulu yakifuatiwa na mazungumzo rasmi kati yao na wajumbe waliofuatana nao.
Aidha, Mhe. Mesa atakutana kwa mazungumzo mafupi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli.
Baada ya mazungumzo hayo, Mhe. Mesa na Mhe. Suluhu watakuwa na mkutano wa pamoja na Waandishi wa Habari kuzungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Cuba.
Katika hatua nyingine, Mhe. Mesa atakutana kwa mazungumzo mafupi na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Y. Ndugai katika Hoteli ya Hyatt Regency. Baadaye siku hiyo hiyo, atakutana na Ujumbe wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Hotelini hapo kabla ya kushiriki Chakula rasmi cha Mchana, Ikulu kilichoandaliwa kwa heshima yake na Mwenyeji wake Mhe. Suluhu.
Mhe. Mesa ataondoka Dar es Salaam tarehe 03 Oktoba, 2016 alasiri kuelekea Zanzibar kwa ajili ya kuendelea na ziara yake Visiwani humo. Akiwa Zanzibar, Mhe. Mesa ambaye atapokelewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali Iddi atakutana kwa mazungumzo rasmi na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Dkt.  Ali Mohamed Shein, Ikulu ya Zanzibar.
Tarehe 04 Oktoba, 2016 Mhe. Mesa akiwa ameongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba atarejea Dar es Salaam akitokea Zanzibar kwa ajili ya kuendelea na ziara yake ambapo atatembelea Makumbusho ya Taifa.
Uhusiano wa Tanzania na Cuba
Uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Cuba ulianzishwa zaidi ya  miaka 50 iliyopita  na Viongozi Waasisi wa mataifa haya mawili, Rais Mstaafu wa Cuba, Mheshimiwa Fidel Castro na Baba wa Taifa, Hayati Julius K. Nyerere. Tangu Tanzania ipate uhuru Cuba imekuwa ikitusaidia katika maeneo mbalimbali ikiwemo afya, utamaduni, elimu, michezo, utalii, nishati, teknolojia na kilimo.
Ushirikiano katika Sekta ya Afya
Tanzania na Cuba zimekuwa zikishirikiana kwenye sekta ya afya ambapo hadi sasa kuna jumla ya Madaktari 30 kutoka Cuba wanaofanya kazi kwenye Hospitali mbalimbali Tanzania Bara na Zanzibar. Kati ya Madaktari hao 10 wapo Bara na 20 wapo Zanzibar wakiwemo wanaofundisha katika Kitivo cha Tiba, Chuo Kikuu cha Zanzibar na kutibu katika Hospitali mbalimbali Zanzibar.
Aidha, katika jitihada za Serikali za kupambana na malaria Serikali ya Cuba na Tanzania zilikubaliana kujenga Kiwanda cha Viuatilifu vya Kuua Viluwiluwi vya Mbu ambacho kimejengwa kwenye eneo la Viwanda Wilayani Kibaha, Mkoani Pwani na kuzinduliwa mwezi Julai, 2015.
Kiwanda hicho ambacho kilijengwa kwa ushirikiano kati ya Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) na Kampuni ya LABIOFAM ya Cuba kimekamilika na kwa sasa kinazalisha dawa za majaribio. Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha lita milioni 6 za viuatilifu kwa mwaka ambazo zinatosheleza kwa matumizi ya Tanzania na hata kuuzwa nchi nyingine za Afrika.
Sekta ya Elimu
Katika Sekta ya Elimu Tanzania na Cuba zimekuwa zikishirikiana kwenye programu mbalimbali ikiwemo nafasi za ufadhili wa masomo nchini Cuba kwa wanafunzi kutoka Tanzania. Kuanzia mwaka 2008 hadi 2014 jumla ya Watanzania 64 walipata ufadhili wa mafunzo nchini Cuba katika fani mbalimbali ikiwemo udaktari, uchumi, TEHAMA na Michezo.
Pia Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Cuba ilianzisha Programu ya Elimu kwa Vijana na Watu Wazima ambayo hutolewa kwa kutumia vifaa vya kufundishia vinavyomwezesha mwanafunzi kusikia na kuona (audiovisual). Inatarajiwa kwamba zaidi ya vijana na watu wazima milioni 3 watakuwa wameshiriki programu hii ifikapo mwaka 2017. Mradi wa majaribio ya program hii ulizinduliwa mwaka 2014 katika Manispaa za Ilala, Temeke, Kinondoni, Ilemela, Mwanga, Bagamoyo, Mkuranga na Songea.
Sekta ya Michezo
Katika Sekta ya michezo Serikali ya Cuba wametupatia Wakufunzi wa Ngumi, Judo na Riadha. Hivi sasa wanatoa nafasi za mafunzo nne kila mwaka kwenye mafunzo ya michezo na utaalamu wa mazoezi ya viungo.
Hivyo, pamoja na kutumia fursa ya ziara hiyo kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizi mbili Tanzania itatumia nafasi hiyo kujikita katika kuanzisha ushirikiano kwenye maeneo mapya hususan biashara na uwekezaji.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar es Salaam, 30 Septemba 2016

GAVANA BENKI KUU YA TANZANIA BENNO NDULU ASEMA KASI YA UKUAJI WA PATO LA TAIFA IMEONGEZEKA

GAVANA WA BENKI KUU NDULU
Na Abushehe Nondo na Lilian Lundo, Maelezo.
Kasi ya ukuaji wa pato la Taifa  kwa nusu ya kwanza ya mwaka yaani Januari mpaka Juni 2016 imeongezeka na kufikia asilimia 6.7 ikilinganishwa na asilimia 5.7 kwa nusu ya kwanza ya mwaka  2015.

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Benno Ndulu alisema kuwa kwa mujibu wa takwimu kutoka Ofisi  ya Taifa ya Takwimu , hali ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania imeendelea kuwa ya kuridhisha  ambapo katika robo ya pili ya mwaka 2016 ukuaji wa Pato la Taifa unakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 7.9 ikilinganishwa  asilimia 5.8 kwa kipindi kama hicho  mwaka 2015.

Ndulu alisema kuwa shughuli za kiuchumi ambazo zimesaidia kukua kwa uchumi katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2016 kuwa ni pamoja naUsafirishaji na uhifadhi wa mizigo asilimia 30.6, uchimbaji wa madini asilimia 20.5, Mawasiliano na Habari asilimia 12.6 na Sekta ya fedha na Bima asilimia 12.5.

Alisema ukuaji wa sekta ya uchukuzi na ujifadhi wa mizigo umetokana na kuongezeka kwa usafirishaji wa abiria kwa njia ya biashara na gesi asili ambao umekua kwa zaidi ya nusu ukilinganisha na robo ya pili ya mwaka 2015 kwa asilimia 9.4.

Akizungumzia hali ya ukuaji wa uchumi kwa nusu ya mwaka 2016 Ndulu alisema kuwa katika nusu ya kwanza ya  Januari hadi Juni mwaka 2016 kasi ya ukuaji wa pato la Taifa umeendelea kukua kwa kasi kutokana na baadhi ya sekta kuonekana kukua zaidi ikiwemo Uchukuzi na Uhifadhi wa Mizigo asilimia 17.4

Sekta nyingine ambayo imekua kwa kasi kwa kipindi hicho ni pamoja na sekta ya Uchimbaji wa Madini na Gesi asilimia 13.7, Mawasiliano asilimia 13.0 na sekta ya fedha na Bima asilimia 13.0.

Akifafanua michango ya shughuli mbalimbali zilizochangia ukuaji wa  kiuchumi  katika nusu ya kwanza ya Mwaka huo alizitaja kuwa ni pamoja na Uchukuzi na Uhifadhi  Mizigo asilimia 16.0, Ujenzi asilimia 10.7, na Sekta ya Kilimo ambayo inaonekana kukua kwa asilimia 10.3 katika nusu ya kwanza ya mwaka 2016.

Aidha alisema kuwa kwa kuangalia hali ya ukuaji wa pato la Taifa kwa nusu ya kwanza ya mwaka pamoja na viashiria mbalimbali vya uchumi ni mategemeo yao kwamba pato la Taifa kukua kwa asilimia 7.2 kwa mwaka 2016 litafikiwa. 

WAZIRI NAPE AKUTANA NA BALOZI WA SPAIN NCHINI

Waziri wa Habari, Utamaduni,  Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akizungumza na Balozi wa Spain nchini Bw. Felix Costales Artieda kuhusu kusaidia kuendeleza sekta ya Utamaduni na Michezo leo Septemba 30,2016 wakati Balozi huyo alipofika ofisini kwa Waziri  Jijini Dar es Salaam kukabidhi moja ya mradi wa Utamaduni uliokuwa ukifanywa na serikali ya Spain katika Bonde la Ufa la Olduvai Gorge Mkoani Manyara

WATEJA BAYPORT WAANZA KUPEWA HATI KILWA

Afisa Sheria wa Bayport Financial Services, Mrisho Mohamed katikati akimkabidhi hati yake ya kiwanja mteja wao aliyenunua kiwanja cha Kilwa, Mubarack Kirumirah kulia. Kushoto ni Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa.


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WATEJA wa viwanja vya Bayport Financial Services wilayani Kilwa, mkoani Pwani wameanza kupewa hati zao kutoka mradi wa Kilwa Msakasa unaoendeshwa na taasisi hiyo inayojihusisha na mikopo, huku ikiwa na dhamira ya kuwakwamua wateja wao na Watanzania kwa ujumla.

Mradi wa Kilwa Msakasa ni miongoni mwa miradi kadhaa inayoendeshwa na taasisi hiyo ikiwamo Bagamoyo, Vikuruti, Kigamboni na Kibaha na kujikita kurahisisha pia utoaji wa hati kwa wateja wao waliokamilisha utaratibu rahisi wa malipo ya viwanja hivyo.Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Masoko na Mawasiliano, Mercy Mgongolwa, alisema kwamba kuanza kutolewa kwa hati za mradi huo wa Kilwa ni sehemu ya mwendelezo wa kuboresha huduma zao za mikopo ya viwanja inayotolewa sehemu mbalimbali nchini Tanzania.
Mteja wa Bayport Financial Services, Mubarack Kirumirah kulia akitia sahihi kabla ya kukabidhiwa hati yake ya kiwanja cha Kilwa. Anayeshuhudia ni Afisa Sheria wa Bayport Financial Services, Mrisho Mohamed.
Shughuri za maandiko ya kukabidhiana hati zikiendelea katika ofisi za Bayport jana.


Alisema taasisi yao imeendelea kuboresha huduma zao ili kuhakikisha kwamba kila Mtanzania anapata uwezo wa kumiliki kiwanja chenye hati kwa ajili ya kuvitumia katika mipangilio ya maisha yao.

“Bayport ni taasisi ambayo imekusudia kuona watu wanamiliki viwanja vyenye hati kwa urahisi, hivyo kila aliyekopa kiwanja au kununua kwa fedha taslimu kupitia kwetu atakabidhiwa hati yake haraka iwezekanavyo kwa sababu tumedhamiria kuwakwamua wateja wetu wote, hivyo wale ambao hawajapata fursa ya kuhudumiwa na ofisi yetu wafanye hivyo ili waone namna gani Bayport ipo kwa ajili yao,” alisema Mercy.

Naye Afisa Sheria wa Bayport Financial Services, Mrisho Mohamed, aliwataka wateja wao kutembelea katika ofisi za taasisi yao zilizoenea nchi nzima ili wapate huduma bora za mikopo ya viwanja inayowahusu watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni binafsi pamoja na wajasiriamali.

“Tunajivunia kufanya kitu tofauti kwa wateja wetu ndio maana kila anayepata kiwanja kwetu tunahakikisha kwamba hapati usumbufu wowote wa kufuatilia hati sehemu husika badala yake sisi ndio tumechukua jukumu hilo tukiamini kwamba jambo hili litakuwa mkombozi kwa wateja wote,” alisema Mohamed.

Naye mteja wa Bayport aliyekabidhiwa hati yake ya kiwanja cha Kilwa, Mubarack Kirumirah Hamidu, aliwashukuru Bayport kwa kufanya kazi nzuri inayowaendelea usumbufu wateja wao kufuatilia hati za viwanja, jambo linaloonyesha utofauti mkubwa katika suala zima la ardhi.

“Nashukuru kwa kupata hati ya kiwanja change kwa kipindi kisichozidi miezi mitatu tangu nilipojitokeza kununua kiwanja cha Kilwa Msakasa, hivyo suala hili limenifurahisha na kuwaeleza Watanzania wenzangu kuchangamkia kununua viwanja vya Bayport,” alisema.

Wengine waliokabidhiwa hati zao za viwanja vya Kilwa ni Mrina Harish Mawji, Jigar Patel, Amina Haidari Amani, Victoria Ambrose Kundi na wengine wengi ambao wamekuwa miongoni mwa Watanzania waliojitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa ya mikopo ya viwanja vya Bayport vinavyoendelea kutolewa na taasisi hiyo nchini Tanzania.

MABONDIA KUPIMA UZITO KESHO KWA AJILI YA MPAMBANO WAO WA OCTOBER 2 KIMARA KOROGWE


Na Mwandishi Wetu
BABONDIA mbalimbali watakaozipiga siku ya jumapili ya October 2 katika ukumbi wa White House Bar Kimara Korogwe watapima uzito pamoja na Afya zao kesho jumamosi katika ukumbi uho kwa ajili ya kuzipiga siku inayo fuata

akizungumzia mpambano uho kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini ambaye ni mratibu wa mpambano uho Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa mabondia wote watapia uzito pamoja na Faya Zao siku ya jumamosi

Aliwataja baadhi ya mabondia watakaozipiga ambao  kesho watapima uzito ni kuwa ni mabondia Said Chino ambaye amejiandaa kuzipiga na >>INAENDELE>BOFYA 

SAYANSI YA SOKA: SALAM KWA TIMU ZA YANGA, SIMBA NA AZAM

Hii ni Makala iliyoandikwa kitaalam ikichambua kwa undani kuhusu soka, je ungependa kuisoma ili kujipatia maarifa? Tafadhali/BOFYA HAPA

MAGAZETINI LEO


ยช