.

RAIS MAGUFULI : KENYA, MSHIRIKA NAMBA MOJA WA TANZANIA KIBIASHA BARANI AFRIKA

Oct 31, 2016

Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania amekanusha madai kuwa serikali yake inazipuuza nchi jirani na kujikita zaidi katika masuala ya ndani.
Akizungumza Jumatatu akiwa katika safari yake ya kwanza nchini Kenya tangu aingie madarakani Novemba mwaka jana , Dkt. Magufuli amesema daima amekuwa akiwasiliana na Rais Uhuru Kenyatta kwa njia ya simu. Ameongeza kuwa Tanzania inaitambua Kenya kama 'mshirika wetu nambari moja wa kibiashara barani Afrika.' Amesema safari yake nchini Kenya inalenga kuimarisha zaidi uhusiano wa nchi mbili ambao umekuwa mzuri tokea siku za nyuma. Magufuli amesema amemfahamisha Rais Kenyatta kuhusu uhalisia wa mambo nchini Tanzania ambao ni kuwashurutisha Watanzanai walipe kodi na kupambana na ufisaid ili nchi isonge mbele.

Rais Magufuli (kushoto) na Rais Kenyatta
Rais Magufuli amekaribishwa kwa taadhima na heshima kubwa iliyojumuisha kukagua gwaride kamili la jeshi iliyoandamana na mizinga 21. Punde baada ya kuwasili, Rais Maguduli aliweka shada la maua katika kaburi la mwanzilishi wa taifa la Kenya, Mzee Jomo Kenyatta kabla ya kuelekea Ikulu ya Rais kwa mapokezi rasmi na mazungumzo na mwenyeji wake. Viongozi hao wamejadili masuala ya uhusiano wa nchi mbili na kieneo.

HAZARD,COSTA WAPELEKA KILIO ST.MARY’S,CHELSEA IKING’ARA UGENINI

chelsea-october-6
Timu ya Chelsea imepata ushindi wake wa ugenini wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji Southampton Mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza mechi iliyochezwa katika uwanja wa Mtakatifu wa St.Marry’s.
Wageni walikuwa wa kwanza kuandika bao kupitia kwa Eden Hazard dakika ya sita baada ya kuwachambua mabeki wa Southampton na mfungajia akipiga mpira wa chini chini na kumuacha mlinda mlango Forster akiwa hana la kufanya.
Baada ya kufungwa bao hilo Wenyeji walicharuka na kuliandama lango la Chelsea kama nyuki kutokana na mfumo wa Conte wakutumia wachezaji watano katikati huku nyuma akiweka watatu na kumubakiza mtu mmoja mbele uliwambana vilivyo wenyeji na kushindwa kupenya ngome ya wageni hadi mapumziko Chelsea walikuwa mbele ya bao moja.
Kipindi cha pili kilianza kwa Chelsea kupata bao dakika ya 55 kupitia kwa, Diego Costa baada ya kupokea pasi safi toka kwa kiungo mkabaji Matic huku likiwa bao lake la 7 na kuendelea kuwa kinara wa ufungaji kwenye msimamo wa Ligi hiyo.
Kwa matokeo hayo Chelsea wamepanda hadi nafasi ya nne ya msimamo wakiwa na alama 22 kwa michezo yao kumi wakati Southampton wamebaki nafasi ya tisa na alama 13.
VIKOSI:
SOUTHAMPTON (4-3-3-):Forster; Martina, Fonte, Van Dijk, Bertrand (McQueen 78); Romeu, Clasie (Boufal 61), Davis; Redmond, Tadic (Hojbjerg 78), Austin
SUBS NOT USED: Yoshida, Ward-Prowse, Taylor, Olomola
CHELSEA (3-4-3):Courtois; Azpilicueta, Luiz, Cahill; Moses (Ivanovic 87), Kante Matic, Alonso; Pedro (Willian 78), Costa (Batshuayi 89), Hazard
SUBS NOT USED: Begovic, Oscar, Terry, Chalobah
GOALS: Hazard 6, Costa 55
REFEREE: Mike Jones
ATTENDANCE: 31,827 (P.T)

WADAU WAJADILIANA JINSI SEKTA BINAFSI INAVYOWEZA KUSHIRIKI KATIKA MKAKATI WA UTEKELEZAJI THABITI WA MPANGO WA PILI WA MIAKA MITANO WA MAENDELEO YA TANZANIA, (FYDPII)

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii, (ESRF), Dkt. Tausi Mbaga Kida, (kulia), akizungumza kwenye Warsha ya majadiliano ya wadau kuhusu nafasi ya sekta binafsi katika kutekeleza mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano (FYDPII), kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Mkoawa Simiyu, Bw. Anthony Mtaka
 Naibu Katibu Mkuu Tume ya Mipango, kutoka Wiraza ya Fedha na Mipango, Dkt. Maduka Paul Kessy(kushoto0, akizungumza kwenye warsha hiyo.
Mkurugenzi wa Huaduma kwa Wanachama, Taasisi ya Sekta Binafsi, (TPSF), Bw. Louis Accaro, akitoa mada yake juu ya sekta za kipaumbele ambazo zinapaswa kujadiliwa ili kufanyiwa kazi, sekta hizo ni kutoka zao la Pamba na kuwa nguo, kutoka ngozi na kuwa mazao yatokanayo na ngozi, na pia viwanda vya madawa
 Baadhi yawashiriki wa warsha wakifuatilia mjadala
 Baadhi ya washiriki


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Anthony Mtaka, akizungumza wakati wa warsha hiyo

NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID
WADAU kutoka kada mbalimbali wamekutana kujadiliana jinsi sekta binafsi itakavyoshiriki katika utekelezaji thabiti wa mpango wa pili wa miaka mitano wa maendeleo ya Tanzania kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii, (ESRF), Dkt. Tausi Mbaga Kida, amesema sekta binafsi inao umuhimu mkubwa katika kushiriki kuandaaa na kujadili mipango mbalimbali ya maendeleo.
Dkt. Kida aliyasema hayo katika hotuba yake aliyoitoa kwenye Warsha ya majadiliano kuhusu nafasi ya sekta binafsi katika kutekeleza mpango wa pili wa miaka mitano wa maendeleo ya Tanzania, (FYDP II) iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Warsha hiyo iliyoandaliwa kwa pamoja na ESRF, Serikali kupitia Tume ya Mipango na Mpango wa Kusaidia Mabadiliko ya Kiuchumi, (SET), iliwakutanisha wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na Taasisi ya Sekta Binafsi nchini, (TPSF), CEO roundtable, Suma JKT, Taasisi ya Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) , wadau wa maendeleo kutoka Jumuiya ya Ulaya, mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) na wasomi.
Dkt. Kida alisema, Majadiliano hayo nimatokeo ya juhudi zilizoanza tangu  1998-200, ambapo ESRF ilishiriki katika uanzishwaji wa mpango wa Taifa wa Vision 2025 uliolenga kuitoa Tanzania kwenye kundi la nchi masikini hadi zile zenye uchumi wa Kati, (Middle income coutry.
“Mwaka 2011 ESRF ilifanya mkakati wa kupitia mpango huo wa vision 2015 na kubaini masuala kadhaa ambayo yalihitaji kuelezewa kama kweli taifa linaelewa mpango huo wa kipindi kirefu.” Alisema na kuongeza ni hivi karibuni sisi katika ESRF tulifanya mapitio ya mkakatiwa kwanza wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDPI), na MKUKUTA II, mapitio ambayo yamechangia kuingia katika Mpango huu wa pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano, (FYDP II), Alisema Mkurugenzi huyo Mtendaji wa ESRF.
 Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Tume ya Mipango, kutoka Wiraza ya Fedha na Mipango, Dkt. Maduka Paul Kessy alisema, “Kuna mambo matatu muhimu ya kuzingatia katika mkakati huu ambayo wajumbe mtalazimika kuyafanyia kazi kwa kina ambayo ni pamoja na kutambua kwamba nchi yetu imedhamiria kuingia kwenye uchumi wa viwanda, kwa hivyo rasilimali tulizonazo tuhakikishe zinalisha viwanda vyetu mfano tunapaswa tujadiliane ni kwa namna gani tunafikia hatua ya kuchakata pamba na ngozi hapa hapa nchini, na utengenezaji wa madawa.”, aliwaambia washiriki wa warsha hiyo.
Ili kutekeleza hilo, Viongozi wa Wilaya na Mikoa hawana budi kushirikiana na sekta binafsina kujadili namna ya kutekeleza maswala haya ili kusudi ifikapo mwishoni mwa Novemba mwaka huu, tutakapokutana tujue nini kilicho mbele yetu, alifafanuaDkt. Kessy.
Akitoa mada yake kuhusu ushirikishwaji wa sekta binafsi katika maendeleo ya nchi, Mkuu wa mkoa wa Simiyu Bw. Anthony Mtaka alisema, “Wakati umefika sasa, watanzania kuanzisha viwanda vidogo vya kuongeza thamani ya mazao na mifugo ili kuboresha maisha na kuondokana na tatizo la vijana kukosa kazi.
Akitolea mfano, Mkuu huyo wa mkoa ambaye ameteuliwa na Rais John PombeMagufuli kuogoza mkoa huo akitokea wilayani Mvomero mkoani Morogoro, alisema. “Sisi Simiyu tumepiga hatua, hivi sasa tunatengeneza chaki sisi wenyewe kwa matumizi ya shule, na tunataka pamba tunayolima ambapo Simiyu ndio mkoa unaoongoza kwa uzalishaji wa zao hilo, tuanze kutengeneza vifaa vya hospitalini vinavyotokana na zao la pamba. “ Alifafanua Mkuu huyo wa Mkoa kijana.
Bw. Mtaka pia alisema, asilimia 50 ya mifugo inatoka mkoani Simiyu na moja ya mkakati alioufanya kuwashirikisha SIDO na wadau wengine katika kuanzisha kiwanda kidogo cha kuongeza thamani ya maziwa na kutengeneza bidhaa mbalimbali zitokanazo na maziwa na nia yetu ni kusambaza viwanda vya aina hii kwenye kila wilayaniRAIS DK. MAGUFULI AWASILI JIJINI NAIROBI, APOKELEWA NA MWENYEJI WAKE RAIS UHURU KENYATTA


Rais Dkt John Pombe Magufuli, akilakiwa na Mwenyeji wake, Rais wa Kenya, Mh. Uhuru Kenyatta alipokaribishwa Ikulu, Nairobi nchini Kenya leo. Rais Magufuli yupo nchini Kenya kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
Rais Dkt John Pombe Magufuli (kulia) akiwa na Mwenyeji wake, Rais wa Kenya, Mh. Uhuru Kenyatta wakipokea salamu za kijeshi, katika viwanja vya Ikulu ya Kenya, Jijini Nairobi leo.
Rais Dkt John Pombe Magufuli akikagua gwaride la Jeshi la Kenya, alipowasili Ikulu jijini Nairobi leo.
Rais Dkt John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mwenyeji wake, Rais wa Kenya, Mh. Uhuru Kenyatta, alipowasili Ikulu ya Kenya, Jijini Nairobi leo.
Rais Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Naibu Rais wa Kenya, Mh. Willam Ruto.

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA TAMASHA LA MAZINGIRA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI KATIKA UKUMBI WA NKURUMAH HALL CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikikata utepe kuashiria kuzindia kitabu cha Pastoralism and Climate Change in East Africa kwenye Tamasha la Mazingira na Mabadiliko ya Tabia Nchi unaokutanisha wanasayansi, watafiti na wadau wa mazingira chini ya Usimamizi wa Kigoda cha mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na mabadiliko ya Tabia ya nchini katika ukumbi wa Nkurumah Hall, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza viongozi wengine kuonyesha juu kitabu cha Pastoralism and Climate Change in East Africa kuashiria kimezinduliwa rasmi kwenye Tamasha la Mazingira na Mabadiliko ya Tabia Nchi unaokutanisha wanasayansi, watafiti na wadau wa mazingira chini ya Usimamizi wa Kigoda cha mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na mabadiliko ya Tabia ya nchini katika ukumbi wa Nkurumah Hall, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano kimataifa unaohusu mabadiliko ya tabia ya nchi unaokutanisha wanasayansi, watafiti na wadau wa mazingira chini ya Usimamizi wa Kigoda cha mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na mabadiliko ya Tabia ya nchini katika ukumbi wa Nkurumah Hall, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Wajumbe walihudhuria mkutano wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano kimataifa unaohusu mabadiliko ya tabia ya nchi unaokutanisha wanasayansi, watafiti na wadau wa mazingira chini ya Usimamizi wa Kigoda cha mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na mabadiliko ya Tabia ya nchini katika ukumbi wa Nkurumah Hall, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye ukumbi wa Nkurumah Hall,tayari kufungua mkutano kimataifa unaohusu mabadiliko ya tabia ya nchi unaokutanisha wanasayansi, watafiti na wadau wa mazingira chini ya Usimamizi wa Kigoda cha mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na mabadiliko ya Tabia ya nchini katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

MAGAZETI YA LEO

TANZANIA
u
UK

IRAN NDIO NCHI SALAMA ZAIDI ULIMWENGUNI

Oct 30, 2016

Brigedia Jenerali Salam
Naibu Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH) amesema kuwa, Iran imesimama kidete na ndiyo nchi yenye amani na usalama zaidi ulimwenguni inapolinganishwa na ukubwa na aina ya vitisho na vikwazo vinavyozikabili nchi mbalimbali za dunia.
Brigedia Jenerali Hussein Salami amebainisha kwamba, Iran hii leo ina nguvu za kukabiliana na vitisho vyote na imesimama kidete katika hilo na kwamba imejiandaa kikamilifu kukabiliana na adui katika kiwango chochote kile.
Naibu Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (SEPAH) amesema kuwa, hii leo anga kwa ajili ya ukoloni katika ardhi za Kiislamu imebanwa zaidi na ardhi hizo zimegeuka na kuwa medani za jihadi za Waislamu.
Brigedia Jenerali Hussein Salami, Naibu wa Kamanda wa Jeshi la SEPAH
Brigedia Salami amebainisha pia kwamba, katika ardhi za Kiislamu ikiwemo Yemen ambayo imesimama kupambana na utawala wa Aal Saud mpaka nchini Bahrain ambako Waislamu wameamka, tayari kumejitokeza mapinduzi na kwamba ardhi hizo hivi sasa si mahala salama tena kwa uistikbari.
Naibu Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (SEPAH) amezungumzia pia matukio ya Iraq na kusema kuwa, wananchi wa nchi hiyo wamefanikiwa kudhibiti hali ya mambo katika medani ya vita na kupambana na magaidi huku Hizbullah ya Lebanon ikiwa fakhari ya ulimwengu wa Kiislamu inaendelea kuutikisa na kuuteteresha utawala haramu wa Israel.
ยช