.

RAIS DK.SHEIN AKUTANA NA BALOZI WA KENYA

Nov 30, 2016

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Balozi wa Kenya hapa Tanzania, Chirau Ali Makwere (kushoto), alipofika Ikulu Mjini Unguja, leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Balozi wa Kenya hapa Tanzania, Chirau Ali Makwere (kushoto), alipofika Ikulu Mjini Unguja, leo. (Picha na Ikulu, Zanzibar)

DANGOTE AFUNGA KIWANDA CHA SARUJI MTWARA, MITAMBO YAPATA KWIKWI

Mtwara
UZALISHAJI katika kiwanda cha saruji cha Dangote kilichopo Mtwara umeathirika kwa kiasi kikubwa tokea wiki iliyopita. Tatizo hili la muda limetokana na hitilafu za kiufundi katika mitambo ya kiwanda. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dangote Tanzania, Bwana Harpreet Duggal amesema mafundi wa Dangote wapo kazini na shughuli za uzalishaji zitarejea katika siku chache zijazo. 

Alisema kiwanda kilianza uzalishaji wa kibiashara mapema mwaka huu na kama ilivyo kwa kiwanda kingine kama hicho jambo lolote linaweza kutarajiwa hasa katika miezi ya mwanzo. Hata hivyo alizitaja hitilafu hizo kuwa ni za kawaida na uzalishaji utarejea katika kipindi kifupi kijacho. 

Alipoulizwa kuhusu gharama kubwa za uzalishaji, Bwana Duggal alisema unapolinganisha na gharama nyingine za uzalishaji katika Dangote, gharama za uendeshaji Tanzania ni za juu mno. Moja ya sababu kuu ni matumizi ya jenereta za dizeli katika kuendesha kiwanda. Na pia kiwanda kuwepo mbali na soko kuu la saruji kumechangia ongezeko la gharama za usafirishaji. Akasema serikali inaangalia suala hili la gharama na jinsi ya kutafuta njia ya kutupunguzia mzigo huu.

Akaongeza, “Tuna matumani makubwa kuhusu uwekezaji wetu wa muda mrefu hapa Tanzania na tupo makini, kwa kushirikiana na Serikali tutaweza kuhimili gharama za uzalishaji ili tuweze kuendelea kufanya bidhaa ya  saruji kuwa na bei nafuu nchini.”
Tangu kuzinduliwa kwa kiwanda cha saruji cha Dangote, bei ya saruji nchini Tanzania imeshuka kwa zaidi ya asilimia 30.


Kiwanda cha Dangote kilichopo Mtwara chenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 600 kina uwekezaji mkubwa katika saruji kuliko vyote katika Afrika Mashariki. Kina uwezo wa kuzalisha tani milioni tatu kwa mwaka na kutoa ajira ya moja kwa moja kwa zaidi ya watu 1000 wa Mtwara. 

RAIS LUNGU WA ZAMBIA AONDOKA NCHINI

Rais John Magufuli akiagana na Rais wa Zambia, Edgar Chagwa Lungu kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere wakati mgeni huyo alipoondoka nchini kurejea nyumbani jana Novemba 29, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Rais John Magufuli akiwapungia wananchi waliojitokeza kumuaga Rais wa Zambia, Edgar Chagwa Lungu kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere wakati alipoondoka nchini kurejea nchini Novemba 29, 2016. Wengine pichani ni Makamu wa Rais, Samia Suluhu na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Inspekta Jenerali wa Polisi, Ernest Mangu kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Novemba 29, 2016. Wapili kulia ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange na watatu kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi John Kijazi.
 Rais John Magufuli akiongozana na  mgeni wake, Rais Edgar Chagwa Lungu wakati mgeni huyo alipoondoka nchini kurejea nyumbani kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Novemba 29, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Rais John Magufuli na Makamu wa Rais, Samia Suluhu wakishuudia wakati Rais wa Zambia Edgar Chagwa Lungu akiagana na Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere kabla ya kuondoka nchini kurejea nyumbani Novemba 29, 2016.

RAIS DKT MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSTUKIZA GEREZA LA UKONGA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiweka saini kitabu cha wageni akiwa na Kamishna Mkuu wa Magereza John Casmir Minja kabla ya kuongea na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam jana Novemba 29, 2016
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipewa muhtasarai wa kazi na Kamishna Mkuu wa Magereza John Casmir Minja kabla ya kuongea na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam jana Novemba 29, 2016
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akikaribishwa na Kamishna Mkuu wa Magereza John Casmir Minja ili aongee na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam jana Novemba 29, 2016
Mmoja wa askari wa Kikosi Maalumu cha Magereza wakitoa kero zao mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam jana Novemba 29, 2016
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akichukua maelezo kutoka kwa maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam jana Novemba 29, 2016
Baadhi ya maafisa na askari wa Jeshi la Magereza wakimsikiliza Rais Dkt John Pombe Magufuli alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam jana Novemba 29, 2016
Askari wakiwa na shauku ya kutoa kero zao mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli alipoongea na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam jana Novemba 29, 2016
Mkuu wa gereza la Ukonga akieleza changamoto za kazi Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam jana
Novemba 29, 2016
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na baadhi ya maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam jana Novemba 29, 2016
PICHA NA IKULU

MAPITIO YA MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 30, 2016


WAHITIMU 57 WA ELIMU YA ANGA WATUNUKIWA VYETI MKOANI KIGOMA

NA RIPOTA  MAGRETH MAGOSSO MKOANI KIGOMA
ZAIDI ya wahitimu 50 kutoka Chuo Cha Hali ya Hewa  kilichopo wilaya ya kigoma Mkoa wa Kigoma,wameaswa  wafanye kazi kwa kuzingatia weledi,maadili na taratibu za watumishi wa umma,ili  kutoa huduma bora kwa maendeleo ya  Taifa.

Hayo yalibainika jana kigoma ujiji,kwenye mahafali ya 14  ya utoaji wav yeti kwa wahitimu  33 wa ngazi ya cheti  na mahafali ya tano  kwa wahitimu 24  ngazi ya  Stashahada waliohitimu elimu ya Anga ambapo ikitumika  sahihi  taifa litajihami na majanga mbalimbali hasa mabadiliko ya tabia nchi.

Akifafanua hilo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Laurent  Shauri alisema wahitimu hao wamepewa mafunzo stahiki ya watumishi wa umma  ambayo yanalenga maadili,weledi,taratibu na miongozo ya kazi ili,kuongeza ufanisi wa kazi kwa maendeleo ya taifa na waepuke  ngono zembe  inayopelekea  janga la ugonjwa wa upungufu wa kinga mwilini(UKIMWI).

Pia, chuo kinakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa bweni za wanafunzi na miundombinu bora ya utoaji wa elimu hiyo ambayo ni muhimu katika kukabilina na mabadiliko ya tabia nchi na kutoa fursa kwa wakulima kutumia utabiri huo ili kulima kilimo chenye tija utakaonufaisha sektan hiyo.

Akifunga sherehe hizo Mgeni rasmi ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa  Emanuel Maganga alisema  taaluma yao ni chachu ya kukabilina na mabadiliko ya tabia nchi,magonjwa na kuinua sekta ya kilimo na kuisihi mamlaka ya hali ya hewa iongeze vifaa vya kisasa ili kutabiri  ukweli itakuwa na thamani kwa jamii endapo utabiri  utakuwa wa kweli.

Mmoja wa wahitimu  hao Praseda Rafaeli alisema  atafanya kazi kwa uaminifu mkubwa kwa mujibu wa miongozo  ya taaluma yao ambayo ni tija kwa taifa kukabiliana na mafuriko,ukame ambapo utabiri wa kweli ni pamoja na vifaa vya kisasa ambavyo vitawapa mwelekeo na dira ya hali halisi ya hewa na namna ya kukabiliana na matukio yajayo.
Mwisho.

MADAKTARI NCHINI WAMETAKIWA KUITISHA MIKUTANO YA KIJAMII ILI KUJADILI MAGONJWA


Katibu Mtendaji wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA), Fabian Magoma  (kulia), akizungumza katika Kongamano la 33 la siku tano la Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA) linaloendelea Hoteli ya Kebby Mwenge jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto ni  Mwenyekiti wa TPHA anayemaliza muda wake, Daktari Bingwa  Elihuruma Nangawe.
Dk. Manase Frank akitoa mada kwenye kongamano hilo.

 Profesa Andrew Swai akitoa mada.
 Wadau wa sekta ya afya wakifuatilia kwa karibu mada zilizokuwa zikitolewa katika kongamano hilo.
 Kongamano likiendelea.
 Dk. Andronicus Aloyce Rwelamila kutoka Hospitali ya Tumbi Kibaha (kushoto) na Muuguzi wa Hospitali hiyo, Mary Gowele wakiwa kwenye kongamano hilo.
 Kongamano likiendelea

Usikivu katika kongamano hilo. Kushoto ni Mwenyekiti wa TPHA, Dk. Elihuruma Nangawe

 Profesa Japhet Kileo (kulia), akiuliza maswali kwenye 
kongamano hilo.
 Dk. Mwanahamisi Magwangwara (kushoto), akizungumza wakati akijibu maswali mbalimbali kutoka kwa wadau wa sekta ya afya katika kongamano la 33 la siku tano la Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA) linaloendelea Hoteli ya Kebby Mwenge jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni mtoa mada, Profesa Andrew Swai. 
Dk.Chilolo Edward (katikati), akijibu maswali kuhusu changamoto ya waendesha bodaboda. Kushoto ni Profesa Andrew Swai na Dk. Manase Frank. 
Mkurugenzi wa Shirika la Wanawake katika Jitihada za Maendeleo (WAJIKI), Janeth Mawinza akielezea changamoto ya matumizi ya pombe katika Manispaa ya Kinondoni.

Na Dotto Mwaibale

MADAKTARI nchini wametakiwa kufanya mikutano ya kijamii au wananchi ili kuwapa fursa ya kujua magonjwa yanayo wakabili.

Hayo yalielezwa na Dk. Manase Frank wakati akitoa mada katika kongamano la 33 la siku tano la Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA) linaloendelea Hoteli ya Kebby Mwenge jijini Dar es Salaam leo asubuhi.

"Changamoto kubwa tuliyonayo ni wananchi wengi kutojua magonjwa yanayowasumbua hivyo ni muhimu kwa madakatari kuitisha mikutano itakayowakutanisha na wananchi ili kuondoa changamoto hiyo" alisema Dk. Frank.

Alisema wagonjwa wengi wamekuwa wakikata tamaa kwa kuchangiwa na kauli za baadhi ya madaktari ambao wanashindwa kujua tatizo la mgonjwa husika hivyo wakati umefika wa madaktari kushirikiana kwa karibu na jamii, viongozi wa dini  ili kuondoa changamoto hiyo.

Akitolea mfano wa kijana mmoja ambaye alifiwa na ndugu zake wote wa karibu kutokana na ugonjwa wa ukimwi na kuishi kwa kunyanyapaliwa lakini baadaye afya yake ilikuja kuimarika kufuatia ushauri uliotolewa na daktari kwa  jamii iliyokuwa ikimzunguka wakati wa ugonjwa wake.

Mtoa mada mwingine Profesa Andrew Swai aliomba serikali wakati wa siku ya Jumamosi na Jumapili kufunga baadhi ya barabara ili zitumike kwa wananchi kufanya mazoezi ya kutembea ili kujenga afya za miili yako na kuepukana na magonjwa kama kisukari.

Akizungumzia changamoto ya matumizi ya bodaboda Dk.Chilolo Edward alisema kwa mwaka jana katika Hospitali za mikoa ya  Morogoro, Tumbi Pwani na Shinyanga kulikuwa na ajali 895 huku majeruhi wakiwa 4813.

Alisema majeruhi waliolazwa katika hospitali hizo walikuwa ni 4525, waliopewa rufaa kwenda hospitali za Bugando na Muhimbili walikuwa 71 na waliolazwa ni 702.

Alisema vifo vilikuwa 81 hivyo vilitokea baada ya kufikishwa Hospitalini ni 70 na vilivyotokea eneo la ajali vilikuwa 11.

Dk.Chilolo alisema ili kupunguza changamoto hiyo inapaswa watoa huduma za afya kutoa elimu kwa waendesha boda boda pale wanapofikishwa mahospitali kuhusu umuhimu wao katika familia na taifa kwa ujumla hivyo kuwa makini wanapoendesha vyombo hivyo vya moto badala ya kuacha kazi hiyo kufanywa na polisi au Sumatra.


ยช