Breaking News

Your Ad Spot

Nov 6, 2016

DKT. SHEIN ZIARANI PEMBA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na wakuu wa vyombo vya ulinzi nausalama Kisiwani Pemba, mara tu baada ya kuteremka kwenye ndege ksiwani humo Novemba 5, 2016 tayari kuanza ziara ya kikazi ya siku tano kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo. (PICHA NA IKULU  ZANZIBAR)


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiteremka katika Ndege ya Shirika la Ndege la AIR Tanzania mada baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Karume Pemba , Rais akiwa kisiwani humo atafungua miradi mbali mbali ya Maendeleo.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake katika sherehe ya Ufunguzi wa Jengo la Mahakama kuu ya Chake chake zilizofanyika Viwanja vya Mchezo wa Tenis Chakechake Pemba
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiwa na  Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe, Omar Othman Makungu, (kushoto) wakiwa katika sherehe ya Ufunguzi wa Jengo la Mahakama kuu ya Chake chake zilizofanyika Viwanja vya Mchezo wa Tenis Chakechake Pemba
 Jaji Mkuu wa Zanzibar akitoa hotuba yake Mhe, Omar Othman Makungu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe, Omar Othman Makungu, (wa pili kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe, Issa Haji Ussi (wa pili kulia) na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba,Utumishi wa Umma na Utawala Bora mara baada ya  kulifungua jengo la Mahakama kuu ya Chake chake Pemba  akiwa katika ziara ya siku tano kisiwani humo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akipata maelezo wakati alipotembelea sehemu mbali mbali baada ya kulifungua jengo la Mahakama kuu ya Chake chake Pemba akiwa katika ziara ya siku tano kisiwani humo, (kushoto) Jaji Mkuu wa Zanzibar
Mhe, Omar Othman Makungu
Baadhi ya wananchi kutoka shehia mbali mbali katika Wilaya ya Chake chake Pemba wakiwa katika sherehe za Ufunguzi wa Jengo la Mahakama kuu ya Chake chake lililofunguliwa  na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika ziara ya siku tano kisiwani humo

Majaji wa Mahakama Kuu na Wananchi pamoja na Wafanyakazi wa Idara hiyo wakiwa katika sherehe ya Ufunguzi wa Jengo la Mahakama kuu ya Chake chake lililofunguliwa  Chakechake Pemba na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika ziara ya siku tano kisiwani humo

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages