Breaking News

Your Ad Spot

Nov 7, 2016

FBI: HILLARY CLINTON HANA SHITAKA LA KUJIBU

US
Mkurugenzi wa FBI,James Comey
Mkurugenzi wa FBI,James Comey ameliambia bunge la Marekani kuwa baada ya kupitia barua pepe zilizogundulika kutoka kwa Hillary Clinton, wakati alipokua waziri wa mambo ya nje wamegundua kuwa hana hatia yoyote na hawatamfungulia mashtaka.
Kampeni za Clinton ziliingia doa wiki iliyopita baada ya mkurugenzi huyo wa FBI kusema kuwa watazipitia barua pepe zake zilizopatikana katika kompyuta ya msidizi wa zamani wa mume wake.
Kauli hiyo imeonekana kumfurahisha mkuu wa mawasiliano wa kampeni za Clinton Jennifer Palmieri
Marekani
Donald Trump,mgombea urais nchini Marekani
Wakati upande wa Bi Clinton wakifurahia hatua hiyo kwa upande wake Donald Trump amesema Hillary Clinton analindwa na mfumo wa wizi wa kura, amesema Bi Clinton angetakiwa kuchunguzwa kwa muda mrefu.
Na hivi sasa tunaunana moja kwa moja na Zuhura ebu tuambie baada ya FBI kusema hawatamshtaki Hilary Clinton, hali ikoje kwa sasa ikiwa ndio imebaki takribani siku moja uchaguzi ufanyike.BBC

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages