Breaking News

Your Ad Spot

Nov 17, 2016

HILLARY CLINTON: NILITAKA KUJIFICHA KABISA


Mgombea urais wa chama cha Democratic Hillary Clinton ameelezea masikitiko yake alipojitokeza hadharani mara ya kwanza tangu ashindwe kwenye uchaguzi wa rais nchini Marekani na Donald Trump wa chama cha Republican.
Bi Clinton, akihutubu mjini Washington DC amesema alikuwa hataki kutoka nyumbani tena.
Ameambia shirika la kuwasaidia watoto wasiojiweza kwamba uchaguzi huo umewafanya Wamarekani wengi kutafakari.
Bi Clinton aliongoza kwa wingi wa kura za kawaida lakini akashindwa kinyang'anyiro cha urais kupitia kura za wajumbe, ambazo ndizo huamua mshidni wa urais.
"Sasa, nitakiri kwamba kuja kwangu hapa halikuwa jambo rahisi," alisema alipokuwa akitunukiwa heshima na wakfu wa Children's Defense Fund.
"Kuna nyakati kadha wiki hiyo moja iliyopita ambapo nilitaka kujikunyata tu nikiwa na kitabu kizuri na nisiwahi kutoka nje ya nyumba tena."

Aliendelea: "Ninajua wengi wengu mmevunjwa moyo sana na matokeo ya uchaguzi. Hata mimi, pia, zaidi kushinda ninavyweza kueleza.
"Ninajua si jambo rahisi. Najua wiki moja iliyopita, watu wengi wamekuwa wakijiuliza iwapo Marekani ni nchi ambayo tumekuwa tukiamini ndiyo.
"Migawanyiko iliyowekwa wazi na uchaguzi huu imekolea, lakini tafadhali nisikezi ninaposema hili.
"Marekani ni ya thamani. Watoto wetu ni wa thamani. Kuweni na imani katika nchi yetu, mpiganie maadili yetu na daima, msikate tamaa."
Alipokuwa anatoa hotuba ya kukubali kushindwa wiki iliyopita, Bi Clinton alsiema Bw Trump anafaa kupewa fursa ya kuongoza.
Tangu wakati huo, amekuwa haonekani, ingawa siku moja alionekana akifanya matembezi porini.
Kwenye mawasiliano ya simu ambayo yalifichuliwa kwa wanahabari Marekani, alisikika akimlaumu mkurugenzi mkuu wa FBI James Comey, aliyetangaza kuanzishwa kwa uchunguzi mpya kuhusu kashfa yake ya barua pepe zikiwa zimesalia siku 11 kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika.
Baadaye uchaguzi ulipokuwa umekaribia kabisa, Bw Comey alisema hakukupatikana ushahidi mpya ambao ungebadilisha uamuzi wa awali wa FBI kwamba hakukuwa na ushahidi wa kumfungulia mashtaka.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages