.

JESHI LA SOMALIA LAKOMBOA ENEO IA JAUF JUDUD

Nov 20, 2016

Jeshi la serikali ya Somalia limefanikiwa kukomboa mji wa Jouf Judud katika mkoa wa Juba ya Kati huko kusini mwa nchi hiyo.
Ripoti zinasema kuwa mapigano ya kukomboa mji wa Jauf Judud yamesababisha vifo vya watu kadhaa na kujeruhiwa wengine wengi.
Mafanikio hayo ya jeshi la Somalia yanafuatia kukombolewa kwa eneo la kistratijia la  Bakool huko kusini magharibi mwa Somalia. Eneo hilo ambalo limekuwa likishikiliwa na wapiganaji wa kundi la kigaidi la al Shabab lilikombolewa baada ya mapambano makali ya jeshi la Somalia likisaidiwa na askari wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika (Amisom).
Hata hivyo ripoti zinasema baadhi ya vijiji na miji ya mkoa wa Juba ya Kati vingali vinadhibitiwa na wapiganaji wa kundi la kigaidi la al Shabab.
Kundi la al Shabab
Jeshi la Somalia likisaidiwa na askari elfu 22 wa Umojawa Afrika linaendelea kupambana na wapiganaji wa kundi la al Shabab hususan katika maeneo ya kusini mwa nchi hiyo.  

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช