.

KATIBUA MKUU WA UN ATOA INDHARI YA UWEZEKANO WA KUFANYIKA JINAI KUBWA SUDAN KUSINI

Nov 17, 2016


Katibu Mkuu wa Umoja w Mataifa ametoa indhari kuhusu uwezekano wa kufanyika jinai kubwa nchini Sudan Kusini.

Ban Ki moon ametoa taarifa na kutangaza kuwa kuna hatari ya kutokea maafa makubwa Sudan Kusini na hii ni katika hali ambayo vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa havina nyenzo zinazohitajika kuzuia maafa hayo.

Imeelezwa kuwa kupitia ripoti ya siri aliyotoa, Katibu Mkuu wa UN ameituhumu serikali ya Sudan Kusini kuwa imefanya uzembe na amelitaka Baraza la Usalama la umoja huo kuunda kikosi cha nchi za eneo za kutoa msaada kwa askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa.

Ban Ki moon, Katibu Mkuu wa UN

Katika ripoti yake hiyo, Ban Ki moon amebainisha kuwa kuna ushahidi unaoonyesha kuwa katika kipindi cha wiki zilizipota kumekuwepo ongezeko la vitendo vya kufurutu mpaka na uenezaji chuki nchini Sudan Kusini na vilevile wito wa kuzusha machafuko ya kikabila ambao unazidisha uwezekano wa kutokea maafa makubwa.

Ripoti ya Katibu Mkuu wa UN inatolewa katika hali ambayo siku ya Jumatatu, Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini alitangaza kuwa uvumi ulioenezwa na baadhi ya maafisa wa serikali wa kufanyika wizi wa dola milioni 280 katika hazina ya umma una lengo la kuchafua utendaji wa serikali katika mazingira nyeti na hasasi ya kisiasa yaliyopo hivi sasa nchini humo.

Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini

Ikumbukwe kuwa moja ya matatizo yanayowakabili wananchi wa Sudan Kusini kwa sasa ni ongezeko la ukosefu wa ajira ambao kwa mujibu wa Benki ya Dunia umefikia kiwango cha asilimia 12. Aidha raia zaidi ya milioni nne wanakabiliwa na hatari ya baa la njaa kutokana na vita na mapigano yaliyoikumba nchi hiyo.../

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช