.

TRUMP ASHINDA UCHAGUZI MAREKANI, CLINTON AKUBALI MATOKEO

Nov 9, 2016

marekani
MAREKANI: Mgombea Urais wa Chama cha Republican, Donald Trump ameshinda kiti hicho. Trumpa ambaye mpaka sasa ana kura 288 huku Hillary Clinton akiwa na kura 218 za wajumbe kati ya kura zote 538.
Kwa mujibu wa Katiba ya Marekani, Mshindi wa urais alitakiwa kushinda angalau kura 270 kati ya hizo 538 lakini Bw. Trump amevuka na kufikisha kura 279 mpaka sasa.

Clinton akubali kushindwa

CNN na NBC wameripoti kwamba mgombea wa chama cha Democratic Hillary Clinton amempigia simu Donald Trump na kukubali kushindwa.

Shangwe kambi ya Trump

Shangwe, nderemo na vifijo zimetanda miongoni mwa wafuasi wa Donald Trump.

Trump: Asanteni sana

Trump amepanda jukwaani Manhattan, New York. Amewashukuru wafuasi wake na kusema amepigiwa simu na Hillary Clinton “kuwapongeza”.
Akizungumza na wafuasi wake baada ya kutangazwa mshindi, Trump amewataka raia wote wa Marekani, waliomchagua na ambao hawakumchagua kuungana na kuanza kuijenga nchi yao kwani muda wa kampeni na siasa za kugawanyika umekwisha.(P.T)

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช