.

RAIS MAGUFULI AONGOZA KUMUAGA SAMUEL SITTA

Nov 11, 2016

Rais Magufuli akiteta jambo na Makamu wake mama, Samia Suluhu Hassan wakati wa kuuaga mwili wa aliyekuwa Spika mstaafu wa Bunge la Tisa katika viwanja vya karimjee Dar es Salaam
Rais Mstaafu wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akiipitia ratiba ya Msiba wa Marehemu Samwel Sitta
Sehemu ya viongozi mbalimbali
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza jambo kabla ya kutoa heshima za mwisho  kwa aliyekuwa Spika Mstaafu wa Bunge la Tisa na Mbunge wa Urambo Mashariki marehemu Samwel Sitta katika viwanja vya Karimjee Dar es Salaam  Mganga Mkuu wa Dar es Salaam, Grace Magembe (kushoto) akiuandaa mwili tayari kwa kutowa heshima za mwisho kwa Marehemu, Samwel Sitta
Sehemu ya viongozi
Sehemu ya viongozi mbalimbali


Mjukuu wa Marehemu Samwel Sitta, Maxwell Kijo, ambaye ni mwanafunzi  wa Darasa la Tatu Shule ya Msingi, Education Plus iliyopo Tegeta, akimfariji Bibi yake wakati wakutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Mbunge wa Mstaafu wa Bunge la Tisa na Mbunge wa Urambo Mashariki katika viwanja vya Karimjee Dar es Salaam

Rais John Pombe Magufuli,  akitoa heshima za mwisho mbelea ya jeneza lenye mwili wa marehemu Samwel Sitta ambaye alikuwa Spika mstaafu wa Bunge la Tisa na Mbunge wa Urambo Mshariki, katika viwanja vya Karimjee Dar es Salaam
Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Spika Msaafu, Samwel Sitta,  watatu kulia ni Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na mama Salma Kikwete
Rais Mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Spika Msaafu, Samwel Sitta
Spika Mstaafu wa Bunge, Anne Makinda akitowa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa, Samwel Sitta katika viwanja vya Karimjee Dar es SalaamMwandishi Mwandamizi wa Gazeti la Jambo Leo, Suleiman Msuya (kulia) akiteta jambo na mama Anna Mgwira wa Chama cha ACT, wa katikati ni Mwandishi Mwandamizi wa habari za Michezo wa Gazeti Hilo. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA) Mmiliki wa ujijirahaa blog

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช