Rais Barack Obama wa Marekani amemuonya rais
mteule wa nchi hiyo, Donald Trump kwamba hivi karibuni atashuhudia
ukweli wa mambo juu ya utekelezaji wa ahadi zake tata alizozitoa kwa
Wamarekani wakati wa kampeni.
Obama ameyasema hayo huko Athes Ugiriki katika kikao cha kwanza
na waandishi wa habari baada ya uchaguzi wa rais nchini humo ambapo
amemuonya rais huyo mteule juu ya kutotekeleza ahadi hizo.
Ameongeza kuwa, ahadi tata za Trump alizozitoa kwenye kampeni
kukiwemo kuwafukuza mamilioni ya wahajiri, kuvunja makubaliano ya
kiulinzi baina ya Marekani na Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi
NATO, makubaliano ya nyuklia baina ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na
kundi la 5+1, kuwazuia Waislamu kuingia Marekani na kujenga ukuta ili
kuwazuia raia wa Mexico kuingia nchini humo, ni mambo ambayo kutekelezwa
kwake ni kugumu kuliko kuyatamka tu. Lengo la matamshi hayo ya Obama ni
kuzitoa wasi wasi nchi za Ulaya kuhusiana na misimamo ya Donald Trump.
Akiwa katika safari yake ya mwisho nje ya nchi, Rais Obama
anatazamiwa kukutana na viongozi wa nchi za Jumuiya ya Ulaya na kuwapa
matumaini kwamba Washington itaendelea kutekeleza sera za kudumisha
ushirikiano na nchi hizo. Hii ni katika hali amabayo kabla ya hapo Rais
Barack Obama alionya kwamba Trump hana shakhsia ya kuwa rais wa
Marekani. Ushindi wa Trump katika uchaguzi wa tarehe 8 mwezi huu,
umeibua hali ya wasi wasi mkubwa kwa viongozi wote wa dunia kutokana na
misimamo yake hasi.
Kufuatia hali hiyo, maelfu ya raia wa Marekani wameendelea kufanya
maandamano katika miji mingi ya nchi hiyo kulalamikia kile wanachosema
ni ukandamizaji wa thamani za demokrasia.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269