Breaking News

Your Ad Spot

Nov 9, 2016

RADIAMALI YA VIONGOZI WA ULAYA KUHUSU USHINDI WA TRUMP

Viongozi wa Ulaya wameonyesha radiamali zao kufuatia ushindi wa Donald Trump wa chama cha Republican katika uchaguzi wa Rais uliofanyika jana.
Baada ya Donald Trump kutangazwa kuwa mshindi wa kiti cha urais nchini Marekani baada ya kutangazwa matokeo ya kura za uchaguzi, Rais Vladimir Putin wa Russia amemtumia ujumbe Trump akisistiza umuhimu wa kuhuishwa uhusiano wa nchi yake na Marekani katika kipindi cha uongozi wa Donald Trump.
Rais Putin wa Russia ataka kuhuishwa uhusiano wa nchi yake na Marekani kufuatia ushindi wa Donald Trump
Huko nyuma pia Rais Putin alisema kuwa Moscow itashirikiana na mgombea yoyote ambaye atachaguliwa kuwa Rais wa Marekani. Trump pia aliahidi kwamba atafanya jitihada kupunguza au kuondoa vikwazo vya miaka mitatu vilivyowekwa na Marekani na Umoja wa Ulaya dhidi ya Russia kuhusiana na hali ya mambo ya Ukraine. Wakati huo huo Bi Federica Mogherini Mkuu wa Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya amesema kuwa umoja huo utaendelea kushirikiana na Marekani. Mogherini ametuma ujumbe kwa njia ya twitter unaoeleza kuwa, uhusiano kati ya Umoja wa Ulaya na Marekani ni mkubwa zaidi kuliko badiliko lolote la kisiasa. Nao wanachama wa ngazi ya juu wa chama cha Kihafidhina cha Ujerumani wameutaja uchaguzi wa Marekani kuwa ulioshtua.
Federica Mogherini Mkuu wa Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya amempongeza Donald Trump kwa ushindi aliopata
Naye Jean- Pierre Rafarrin  Seneta wa mrengo wa kulia wa Ufaransa ametoa radiamali yake kufuatia ushindi wa Trump na uungaji mkono wa mwanasiasa Marine Le Pen kwa ushindi wa mgombea huyo wa chama cha Republican kwa kusema,  'katika mazingira kama haya tutaraji pia ushindi wa mrengo wa kulia wenye misimamo mikali katika uchaguzi wa Rais wa Ufaransa wa mwaka kesho.'
Donald Trump amesema leo baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi wa Rais wa Marekani kuwa, hatua za haraka zinapaswa kuchukuliwa ili kuijenga upya Marekani na kwamba ushirikiano wa wananchi pia unahitajika ili kupambana na matatizo ya kiuchumi nchini humo. Rais mteule wa Marekani ameongeza kuwa wanawake na wanaume waliosahaulika nchini humo, hivi sasa hawatasahaulika tena.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages