Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akizungumza na baadhi ya
wananchi waliokuja kupata huduma Makao Makuu ya Idaya ya Uhamiaji wakati
wa ziara yake ya siku moja aliyoifanya leo Kurasini jijini Dar es
Salaam.
Waziri Mwigulu akiwasili kwenye mradi wa ujenzi wa nyumba za makamishna wa Uhamiaji zinazojengwa Kijichi jijini Dar es Salaam kuzikagua. |
Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji, Abbas Rovya (kushoto), akimpigia saluti Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati) kabla ya kukagua
nyumba hizo za kisasa. Kulia ni Naibu Kamishna wa Uhamiaji (DCI),
Shaban Hamza.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kulia), akiangalia nyaraka
mbalimbali zinazochapishwa katika kiwanda cha kuchapa nyaraka za
Uhamiaji alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Kijichi jijini Dar es
Salaam leo. Kutoka kushoto ni Mrakibu Msaidizi wa Uhamiaji (ASP), Singwa
Mokiwa na Kaimu Kamishna Generali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli.
Mwigulu mbali ya kutembelea kiwanda hicho na mradi wa ujenzi wa nyumba
za kisasa za makamishna wa Uhamiaji pia alizungumza na wafanyakazi wa
Uhamiaji makao makuu Kurasini.
Waziri Mwigulu akipata maelezo zaidi ya uchapishaji kwenye kiwanda hicho.
Kaimu Kamishna Generali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli (kushoto), akimuelekeza jambo Waziri Mwigulu.
Waziri Mwigulu akiangalia nyaraka mbalimbali kwenye
kiwanda hicho.
Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Lusungu Ngairo (katikati), akimueleza jambo Waziri Mwigulu wakati wa ziara hiyo.
Na Dotto Mwaibale
SERIKALI imesema itaboresha mitambo ya kuchapisha nyaraka ya Uhamiaji ili kupata nyaraka zenye ubora wa kisasa.
Hayo
yamebainishwa Dar es Salaam leo mchana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mwigulu Nchemba wakati alipotembelea Kiwanda cha kuchapisha
Nyaraka cha Uhamiaji kilichopo Kijichi Temeke jijini Dar es Salaam.
"Napenda
kuwapongeza wenzetu wa Uhamiaji kwa kuwa na kiwanda cha kuchapisha
nyaraka zao sisi kama serikali tutaongeza nguvu ndani ya taasisi hii ili
kupata nyaraka bora zaidi " alisema Nchemba.
Mwigulu
alisema nyaraka nyeti za serikali ni vizuri zichapwe na taasisi husika
kama wanavyofanya uhamiaji jambo litakalosaidia kutozagaa hovyo mitaani.
Waziri
Mwigulu aliongeza kuwa hivi sasa mpango wa serikali ni kutengeneza
bidhaa zake kupitia taasisi zake kama ilivyo kwa viatu ambapo
wameelekeza vitengenezwe na Magereza na kutumiwa na vyombo vyote vya
ulinzi na usalama.
Alisema hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Rais Dk.John Magufuli la kuzipa uwezo taasisi za serikali hasa majeshi kujiimarisha kwa kufanya kazi za viwanda zenyewe kama za utengenezaji wa madawati, uchapishaji wa nyaraka kama wanavyofanya Uhamiaji na nyingine nyingi.
Alisema hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Rais Dk.John Magufuli la kuzipa uwezo taasisi za serikali hasa majeshi kujiimarisha kwa kufanya kazi za viwanda zenyewe kama za utengenezaji wa madawati, uchapishaji wa nyaraka kama wanavyofanya Uhamiaji na nyingine nyingi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269