Breaking News

Your Ad Spot

Nov 30, 2016

TIMU YA BUNGE YATUA TANGA KUJIFUA NA MASHINDANO YA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI YATAKAYOFANYIKA KENYA DESEMBA 14


 Mwenyekiti wa timu ya Bunge,William Ngereja ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Sengerema mkoani Mwanza akizungumzia maandalizi ya timu ya Bunge kuelekea mashindano ya Afrika Mashariki yatakayofanyika nchini Kenya.
 Mkurugenzi wa Benchi la Ufundi la timu ya Bunge,Stephen Ngony’ani alimaarufu Proffesa Maji Marefu akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye hotel ya Tanga Beach Resort ambapo timu ya Bunge imeweka kambi.

 Mwenyekiti wa timu ya Bunge,William Ngereja ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Sengerema mkoani Mwanza katika akiteta jambo na wachezaji wa timu ya Bunge kushoto aliyevaa tisheti nyekundu ni Mkurugenzi wa Benchi la Ufundi la timu ya Bunge,Stephen Ngony’ani alimaarufu Proffesa Maji Marefu
TIMU ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania “Bunge Sports Club”imetua mkoani Tanga leo kuweka kambi ya siku tatu kwa ajili ya kujiandaa na Mashindano ya Bunge la Afrika Mashariki yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Desemba 14 mwaka huu mjini Mombasa nchini Kenya.

Kikosi cha timu ya Bunge kilichosheheni wachezaji wa michezo ya mpira wa miguu,wavu,riadhaa ,kuvuta kamba na mchezo wa gofu ambao inajumuisha wachezaji 60 ambao watashiriki kwenye mashindanio hayo yanayotazamiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na kila kuonekana kujipanga imara.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga mara baada ya timu hiyo kutua,Mwenyekiti wa timu ya Bunge,William Ngereja ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Sengerema mkoani Mwanza alisema kuwa maandalizi kwa upande wa timu yao yamekamilika kwa asilimia kubwa.

Alisema kutokana na umuhimu wa mashindano hayo waliamua kuweka kambi mkoani Tanga ili kuendana na hali ya hewa kabla ya kwenda nchini Kenya kwa ajili ya kushiriki mashindano hayo ikiwa ni mpango wa kuimarisha kikosi chao.

  “Mimi nisema tu sisi kama timu ya Bunge nia na lengo letu kubwa ni kuhakikisha tunaibuka na ushindi kwenye mashindano hayo na ndio maana tumeamua kuweka kambi mkoani Tanga lakini pia hata hivyo pia kikosi chetu kimeimarika kutokana na usajili ambao tumekuwa tukiufanya kila baada ya miaka mitano “Alisema Ngeleja.

Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Benchi la Ufundi la timu ya Bunge,Stephen Ngony’ani alimaarufu Proffesa Maji Marefu alisema kuwa kikosi chao kimejipanga vizuri kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwenye mchezo huo.

Alisema timu hiyo ipo kwenye mazingira mazuri ya kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwenye mashindano hayo ili kuweza kutimiza dhamira yao waliojiwekea  ya kutwaa ubingwa.
Kwa upande wake,Nahodha wa timu ya Mpira wa Pete ya Bunge,Halima Mdee ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kawe alisema kuwa wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanafanya vizuri ili kutimiza dhamira waliojiwekea ya kuibuka na Ubingwa.

  “Nisema tu sisi kama timu ya mpira wa Pete ya Bunge tumejipanga vizuri na kikosi chetu kina hari kubwa ya kuhakikisha tunaiwakilisha nchi yetu ya Tanzania ipasavyo kwa mafanikio makubwa”Alisema. habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages