.

TRUMP AWATEUA WENYE CHUKI NA UISLAMU KATIKA NAFASI MUHIMU

Nov 20, 2016

Rais-mteule wa Marekani Donald Trump amewateua watu wenye chuki na Uislamu kuhudumu katika Ikulu ya White House jambo linaloashiria muendelezo wa sera zake za chuki ambazo zimewatia hofu Waislamu nchini humo.
Ijumaa mashirika ya kijamii na viongozi wa Waislamu Marekani walitangaza bayana wasiwasi wao kuhusu hatua ya Trump kuwateua watu wenye chuki na Uislamu katika nyadhifa muhimu za usalama wa taifa.
Hata baadhi ya maafisa wa serikali ya sasa na zilizopita Marekani wamebainisha wasi wasi wao kuwa watu walioteuliwa na Trump wataupa nguvu mtazamo wa Waislamu kuwa Marekani inaendesha vita dhidi ya dini ya Uislamu. Tokea Trump atangazwe mshindi katika uchaguzi wa  rais wa Marekani, kumeshuhudiwa wimbi la hujuma dhidi ya Waislamu na watu wa jamii za wachace nchini humo.
Rais-mteule wa Marekani Donald Trump
Ijumaa, afisa mstaafu katika Jeshi la Marekani Luteni Jenenrali Michale Flynn alikubali uteuzi wa Trump wa kuhudumu kama mshauri wa usalama wa taifa. Flynn ana historia ya kutoa matamshi makali dhidi ya Uislamu. Naye Seneta Jeff Session amekubali uteuzi wa Trump wa kuwa mwanasheria mkuu Marekani. Seneta huyo anaunga mkono kauli ya Trump ya kutaka kuzuiwa Waislamu kuingia Marekani. Aidha Trump amemteua mjumbe wa Congress, Mike Pompeo kuwa mkuu wa Shirika la Ujasusi la Marekani, CIA. Pompeo amekuwa akitoa madai kuwa viongozi wa Waislamu Marekani hawachukui misimamo imara dhidi ya ugaidi. Halikadhalika anapinga vikali mapatano ya nyuklia baina ya Iran na madola sita makubwa duniani. Ibrahim Hooper, Msemaji wa Baraza la Mahusiano ya Uislamu na Marekani CAIR amesema ni jambo la kushangaza kuona watu wenye chuki na Uislamu wakipewa nafasi muhimu katika serikali ya Trump.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช