Breaking News

Your Ad Spot

Nov 14, 2016

UJUMBE WA NCHI ZA NORDIC WATEMBELEA WIZARA YA MAMBO YA KATIBA NA SHERIA

hav1
Mkurugenzi Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Bw. Patience Ntwina (aliyesimama) akitoa taarifa ya utekelezaji wa Miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa kwa ujumbe wa wataalam kutoka Umoja wa Mataifa waliotembelea Wizarani hapo leo (14/11/2016).
hav2
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Afisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Zanzibar Bw. Kubingwa Mashaka Simba akitoa taarifa ya utekelezwaji wa miradi inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa kwa ujumbe wa wataalam wa Umoja huo waliotembelea Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Tanzania Bara leo (14/11/2016) jijini Dar Es Salaam. Ujumbe huo umeahidi kuendelea kufadhili miradi mbalimbali baada ya kuridhiswa na utekelezwaji wake.
hav3
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome akiongea katika kikao na wataalam mbalimbali kutoka ujumbe wa Umoja wa Mataifa ambao wametembelea Wizarani hapo leo (14/11/2016) ili kujionea namna Wizara hiyo ilivyofaidika na kutekeleza miradi mbalimbali inayofadhiliwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa. Wananchi hasa wasiojiweza wameweza kupata haki zao kupitia miradi hiyo.
hb1
Sehemu ya wataalam kutoka ujumbe wa Umoja wa Mataifa waliotembelea Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria wakiwa katika kikao na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ( hayupo pichani) ili kuona namna miradi inayofadhiliwa na Umoja huo inavyotekeleza. (P.T)

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages