NA MAGRETH MAGOSSO,KIGOMA
WANANCHI wa Manispaa ya kigoma Ujiji wameshangazwa na
kitendo cha ofisa maendeleo wa vijana mkoani humo Edward Manase kushindwa kujibu hoja ya asilimia tano ya
vijana kuwekezwa katika moja ya mfuko wa
hifadhi ya jamii, ilihali hawajajiunga
na mfuko huo(PSPF).
Hoja hiyo ilitolewa na mmoja wa
wanakamati kutoka Kata ya Bangwe Anatoria Cronery jana kwenye mafunzo ya kamati za kata tisa
zilizopo katika mradi wa uwazi,uwajibikaji ,mgawanyo wa rasilimali na mapambano
dhidi ya rushwa uliolenga kubainisha fursa za kata,matatizo na namna ya
kuzipatia ufumbuzi,uliodhaminiwa na Asasi ya kiraia ya Nyakitonto Youth For
Development Tanzania.
Awali Ofisa vijana Mkoa Edward Manase akiwasilisha mada ya fursa ya
vijana na mpango kazi ambapo alisema asilimia tano za vijana inakabiliwa na changamoto
ya kutokuwa na vikundi endelevu kwa kuwa
vikundi vingi ni vya msimu tu,
Manase alisema ili kukabilina na
hilo mkoa umeandaa mpango wa mitaji/nyenzo za miradi,mafunzo ya stadi kazi,kwa
lengo la kupunguza umaskini na utegemezi kwa familia zao hali inayochangiwa na
vijana wengi wanapenda shughuli za kupata fedha kwa haraka ,ilihali kuna sekta
ya kilimo kupitia ardhi iliyopo.
Akiomba ufafanuzi wa mada
wasilishwa Anatoria Cronery alihoji mitaji yao kwa maana ya asilimia tao za
vijana kuwekezwa katika mfuko wa hifadhi ya jamii ya PSPF bila kuwa wanachama
wa mfuko huo,kwa kuwa wengi wameshindwa kujiunga kutokana na ukosefu wa ajira
ya kulipa ada ya sh.20,000 kila mwezi ili wanufaike na huduma ya Bima ya Afya.
Cronery alisema inashangaza
kuingiziwa fedha za kuwakopesha vijana ili wajikwamue kiuchumi badala yake
wanawekeza katika mfuko huo bila kufahamishwa wananufaikaje na rasilimali fedha
hiyo,ilihali hawana vigezo vya kunufaika na asilimia tano hiyo.
Ajabu ofisa huyo alishindwa kutoa
majibu ya papo kwa hapo kwa mujibu wa mada yake badala yake alisema shughuli
zote za kurasimisha vikundi na utoaji wa fedha hizo zinafanyika katika
halmashauri husika na mkoa unasimamia tu,hivyo ni ngumu kujua vikundi hai na
shughuli zingine za vijana.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa
mafunzo hayo Girbert Kusongwa alishauri
watumishi na wataalamu wa idara za umma
wajitambue ,wasipende kukaa ofisini vikundi vingi kuundwa wakati wa ujio wa
mwenge na si kuwainua vijana lengwa kwa mujibu wa serikali kuu.
Akifunga mafunzo hayo ya siku
moja Mratibu wa asasi hiyo Joel Ramadhan alisema watendaji wa kata na wenyeviti
wake wahakikishe wanaweka mabango yenye kuonesha rasilimali zilizopo katika
kata ,vikwazo vya rasilimali na ufumbuzi na kuandaa taarifa ya utekelezaji wa
mradi ili wnanachi wajue fursa na kuzitumia.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269