.

WASHIRIKI WA MATEMBEZI YA ARUBAINI YA IMAM HUSSEIN AS WATOA UJUMBE KWA WALIMWENGU

Nov 19, 2016

Mamilioni ya watu wanashiriki katika matembezi ya kumbukumbu ya Siku ya Arubaini ya Imam Hussein AS ambapo pia wanatia saini waraka wenye ujumbe unaofafanua kuhusu mjumuiko huu mkubwa zaidi duniani.
Washiriki wa matembezi hayo ya Arubaini ya Imam Hussein AS katika njia ya kutoka Najaf hadi Karbala Iraq wameandika barua kwa walimwengu na kueleza kuhusu hali ya leo duniani inayokwenda kwa mujibu wa maslahi ya madola ya kiistikbari na wanaoleta hitilafu baina ya mataifa na watu wa rangi mbali mbali. Kwa msingi huo washiriki wa matembezi hayo wametoa wito kwa watu wa nchi mbali mbali duniani kupambana na dhulma.
Wanaoshiriki katika matembelzi hayo ya Arubaini ya Imam Hussein AS kutoka Najaf hadi Karbala aidha wamesisitiza kuhusu kuunga mkono wanaodhulumiwa na kupambana na dhulma.
Ujumbe huo hadi sasa umetiwa saini na maelfu ya wafanyaziara na inatabiriwa kuwa zaidi ya watu milioni moja watautia saini.
Matini ya barua ya washiriki wa matembezi ya Arubaini ya Imam Hussein AS  imeandikwa kwa lugha sita za Kiarabu, Kifarsi, Kiurdu, Kituruki, Kiingereza na Kifaransa na iko chini ya anuani ya ArbaeenLetter katika mitandao ya kijamii.
Washiriki katika matembezi ya Arubaini ya Imam Hussein AS
Maafisa wa serikali ya Iraq wanatabiri kuwa watu zaidi ya milioni 20 watashiriki katika matembezi ya Arubaini ya Imam Hussein AS mwaka huu.
Inafaa kukumbusha hapa kuwa, matembezi, majlisi na ziara ya siku ya Arubaini hufanyika kila mwaka tarehe 20 Safar, kwa mujibu wa kalenda ya Hijria Qamaria,  baada ya kupita siku Arubaini tangu tarehe 10 mwezi wa Muharram kwa ajili ya kukumbuka kuuawa shahidi mjukuu wa Mtume SAW, Imam Hussein AS na masahaba zake ambao walijitolea roho zao kwa ajili ya kuhuisha dini ya Mwenyezi Mungu katika jangwa la Karbala.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช