.

CCM YAWATEUA RODRICK MPOGOLO KWA NAIBU KATIBU MKUU WA CCM-BARA, HUMPHREY POLEPOLE KATIBU MWENEZI

Dec 13, 2016


Na Bashir Nkoromo, Dar
Chama Cha Cha Mapinduzi (CCM), leo kimeteua viongozi waandamizi watatu kuziba nafasi zilizokuwa wazi, kutokana na waliokuwa wakizishikilia kupewa majukumu mengine ya serikalini.


Uteuzi huo, umefuatia Halamshauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) katika kikao chake, kilichofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli,  na kuridhia mapendekezo ya Kikao cha Kamati Kuu ya CCM, kilichofanyika juzi pia chini ya Dk. Magufuli.Akizungumza na waandishi wa habari leo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, aliyekuwa Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema, kupitia vikao hivyo, CCM imemteua Rodrick Mpogolo anakuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Rajabu Luhwavi ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.


Nape alisema, wapili ni Kanali Ngemela Eslom Lubinga, kuwa Katibu NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Dk. Asha-Rose Migiro aliyeteuliwa kuwa Balozi na Humphrey Polepole aliyeteuliwa kuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Nape mwenyewe aliyeteuliwa kuwa Waziri.


Amesema, kupitia kikao hicho cha Halmashauri Kuu ya Taifa, kilichofanyika leo, mambo kadhaa yaliyopendekezwa na Kamati Kuu, yamejadiliwa na kikao hicho cha NEC na yote yamepitishwa. Kusoma taarifa ya yooote, yaliyojiri katika kikao hicho cha NEC, sasa/BOFYA HAPA

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช