.

HOJA MEYA MPYA KIGAMBONI

Dec 18, 2016

kigano
Meya mteule wa manispaa ya Kigamboni mhe. Maabadi Sulemani Hoja aliye simama akitoa neno la shukrani  baada ya kuchaguliwa kuwa Meya.

Na John Luhende mwambawahabari
Uchaguzi wa Meta na Naibu Meya wa manispaa ya Kigamboni  umefanyika kwa amani na utulivu ambapo wagombea  wa chama cha Mapinduzi CCM wameibuka na ushindi wa nafasi zote mbili.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo  mwenyekiti wa uchaguzi huo ambaye pia ni katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni Rahel Muhando amemtangaza Diwani wa kata ya Pembamnazi
Mhe. Maabadi Suleiman Hoja (CCM) kuwa mshindi wa kiti cha Meya  baada ya kupata kura 9  na kumshinda Mgombea Celestine Maufi wa CHADEMA aliye pata kura 5 kati ya kura zote 15 ambapo Kura moja iliharibika.
Kwa upande wa nafasi ya Naibu meya Mhe. Amin Mzuri Sambo  Diwani wa kata Kibada ameshinda nafasi hiyo baada ya kupata kura 10 na kumbwaga mpinzani wake   Mhe. Ernest Mafimbo (CUF) aliyepata kura 5 katiya kura zote 15 zilizopigwa. 
Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi Meya mteule  Maabadi Selemani hoja amewashukuru wapigakura wote walioshiriki uchaguzi huo na ameahidi kufanya kazi kwa ushirikiano bila ubaguzi wa vyama ili kuleta Maendeleo  kwa wananchi wa  Kigamboni.
Naye aliye kuwa mgombea wa nafasi ya Naibu Meya kwa upande wa UKAWA  akiwakilisha  Chama Cha wananchi CUF, Ernest Ndamo Mafimbo , ameuelezea uchaguzi huo kuwa. Ulikuwa huru na  haki nakukubali kushindwa nakuahidi kushirikiana na washindi hao ili kuwa tumikia wananchi.
“Tumekubali  wenzetu wameshinda maana hata idadi yetu sisi ilikuwa ndogo   wao wlikuwa 10 na sisi tulikuwa 5 tu kwa hiyo unaweza kuona jinsi mambo yalivyokuwa ” 
Mbunge wa Kigamboni Dr Faustine Ndungulile , akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa uchaguzi  amesema nimuda Sasa  wakufanyakazi kwa kuwa mambo mengi yalisimama kwa  muda mrefu kwa kukosa baraza la madiwani kwa kwaajili kupitisha  mipango na miradi mbalimbali ya Maendeleo.(P.T)

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช