NA MAGRETH MAGOSSO,KIGOMA
KITUO
Cha Huduma ya Mtoto (TZ973) Cha Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT )
lililopo katika Manispaa ya Kigoma Ujiji
kwa kushirikiana na Shirika la
COMPASSION Taifa wametumia kiasi cha Fedha
Sh.Milioni 6 kwa
ajili ya zawadi za Krixmas kwa watoto 230 ambao ni Yatima na walio katika
mazingira Magumu.
Hayo yalifahamika juzi
kigoma ujiji katika hafla fupi ya
ugawaji wa zawadi hizo sanjari na kuadhimisha miaka mitatu ya utendaji kazi wa
kituo hicho tangu kuanzishwa kwake ambapo kimesaidia kuokoa maisha ya watoto 320 wanaoishi katika maisha duni na hatarishi,
wakiwemo yatima ambao wengi hunyanyapaliwa na walezi wao hasa kwa
malazi,chakula,elimu,afya kitendo kinachopelekea ongezeko la watoto waishio
mitaani ambapo wengi huishia kwenye makundi ya kihalifu.
Akithibitisha hilo mbele ya JamboLeo Mkurugenzi wa Kituo
hicho Robert Chamungu alisema kulea watoto
yatima ni sehemu ya upendo wa Bwana Yesu Kristo,ambapo alisema wacheni watoto
wadogo waje kwangu,kwa kauli hiyo imemsukuma kushirikiana na Shirika la huduma
kwa watoto Nchini la COMPASSION ili kuwatimizia ndoto zao siku za usoni.
“shirika kwa kushirikiana na kanisa wanaratibu huduma za msingi
kwa watoto wa kituo hicho kuanzia elimu,afya,malazi,chakula na mavazi kwa
ujumla ,kuna watoto walikuwa wanalala chini kwa walezi wao,mfadhili aliwapatia
magodoro na leo tumewapa mchele kilo 5,maharagwe,kilo 3,mafuta lita 12,chumvi
pakti 2 kwa kila mtoto lakini jamii iwajibike isiwachie wafadhili tu “ alieleza
Chamungu.
Alifafanua kuwa kituo kina watoto 320 lakini watoto 196 ndio wamepata wafadhili wa
kuwahudumia kwa kila hitaji la msingi ambapo katika msimu wa sikukuu ya
kuzaliwa Yesu Kristo baadhi yao walitumiwa zawadi za moja kwa moja na watoto 34
wanasimamiwa kihuduma na kanisa katika
kufanikisha ndoto zao siku zijazo .
Alisema jamii iwachukulie watoto yatima ni sehemu ya ibada
kwa kuwalinda kwa hali na mali kama
wanavyowafanyiwa watoto wao,ambao wanatumia walichonacho bila kuwabagua na iwe
hivyo kwa yatima ambao ni watoto wa ndugu na jamaa zao,wasitegemee kufeadhiliwa siku zote kwa kuwa ufadhili una ukomo
wake,hivyo jamii ikubali kubadilika kifikra.
Chamungu alieleza kuwa ifikapo mwanzoni mwa mwaka 2017 wana program
ya kuwapatia mafunzo ya ujasiliamali kwa walezi na wazazi wa watoto husika,ili
kuwajengea uwezo wa kuwahudumia kwa lengo la kuwaratibu watoto wengine wenye
hitaji kama hilo na watakagua kaya za walezi ,ili kutathimini hali ya uchumi baada ya uwezeshaji wao tangu
wapewe huduma kutoka kwao.
Baadhi ya wazazi waliongea na Gazeti hili Jamila Masoud na
Leah Aroun kwa nyakati tofauti walitoa ushuhuda wa mabadiliko ya ufahamu wa
mambo kwa watoto wao ,ambao kwa sasa kabla ya kula na kulala lazima waombe na
wanafanya vizuri darasani na kulishukuru kanisa hilo kwa kutoa huduma ya watoto
bila kujali itikadi za dini.
Kwa
upande wa watoto Leticia Barnabas na Azizi Ally wakiri kupata marifa
ya kiroho na wmepata mwanga wa ndoto zao siku zijazo na kuwasihi wazazi
na walezi wamwamini mungu kwa ibada za kweli,wasimwasi mungu kwa kukiuka
maadili mema na kuzifurahia zawadi walizopewa na wafadhili wao kama
sabuni na biskuts.
Naye Mchungaji wa AICT wa hapao aliwaasa walezi na wazazi walee
watoto katika uchamungu,upendo,imani ambayo itampa mwelekeo wa maadili mema
siku za usoni kwa kusaidia watoto wenye uhitaji ,ambapo kupitia ufadhili wa
shirika la Compassion linajivunia kuwa na vijana wengi wenye uchumi mzuri katika maisha
yao,ambapo wengine leo wanashika nyadhifa kubwa serikalini .
Mwisho.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269