Breaking News

Your Ad Spot

Dec 23, 2016

MBUNGE KIKWETE APONGEZA KASI YA UBORESHAJI WA MRADI WA MAJI WA WAMI


MBUNGE  wa   jimbo la  Chalinze Ridhiwani  Kikwete  amepongeza  jitihada   kubwa  zinazofanywa na  wataaluma  wa Halmashauri ya  Chalinze  katika  kuboresha  mradi  wa maji wa Wami  kwa ajili ya  wananchi  wa Chalinze .


Akizungumza  baada ya  kutembelea  mradi  huo jana mbunge  Kikwete  alisema  kuwa  mradi  huo ambao  ulianzishwa na aliyekuwa  mbunge  wa jimbo   hilo  Dkt  Jakaya  Kikwete  ambae  ni rais mstaafu  wa awamu ya  nne ni  mmoja kati ya  miradi bora  iliyoleta  ukombozi mkubwa wa  upatikanaji  wa  maji safi na  salama kwa wananchi wa  mji  wa Chalinze .

Hivyo  alisema  kusudi la  kufanya  ziara  katika eneo la mradi huo mto  Wami  ni  kuona  shughuli mbali mbali  zinazofanywa na wataalam kwa  ajili ya  kuendelea  kuboresha  mradi huo ili kuwawezesha  wananchi  wake  kupata  huduma ya  uhakika ya maji  safi  na  salama wakati  wote .

" Mradi   huu  ni mkombozi mkubwa kwa wananchi wa  jimbo la Chalinze  na niwapongeze   sana wataalam  wa Halmaszhauri kwa  kazi  nzuri  wanayoifanya  ya  uboreshaji wa maradi huu" alisema  mbunge Kikwete 

Alisema  kuwa  amefurahishwa na  jitihada  zinazoendelea  kufanywa na  wataalam  wa  Halmashauri hiyo  kuhakikisha  wananchi  wanapata  maji na  kazi kubwa yake mbunge  akiwa ni mwakilishi  wa  wananchi ni  kuendelea  kuisimamia  serikali  kwa  kuwawakilisha wananchi  wake  vema bungeni.


  Huku  akiwataka  wananchi  kuendelea  kutunza  miundo mbinu ya maji  ili  kuwezesha mradi  huo  kuendelea kuwa  msaada  kwao .

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages