.

SAINI YA LIONEL MESSI KWENYE FLANA YAWA CHACHU YA NDOTO YA MTOTO WA KI-AFGHANISTAN KUTIMIA

Dec 14, 2016

Picha ya Fred Matuja
Picha ya Fred Matuja
Picha ya Fred Matuja
Lionel Messi ametana na Murtaza Ahmadi mvulana raia wa Afghanistani bingwa wa kuvaa jezi ya plastic
Mtoto huyo wa kiume mwenye umri wa miaka 6 kapata umaarufu mkubwa sana katika tovuti mbalimbali na mitandao ya kijamii kutokana na kitendo chake cha kuvaa jezi ya mfumko wa plastic wenye ranfgi ya bendera ya nchi ya Argentina.Jana mtoto Murtaza Ahmadi amekutana mtu anaemwona kama “role model” wake au shujaa wake anaetaka kufuata nyayo zake.
Mchezaji soka huyo wa klabu ya Catalonia amekutana na Murtaza katika uwanja wa mpira wa miguu huko Doha, nchi Qatar wakati wa mechi kati ya Al-Ahli ya Saudi Arabia na Barcelona bingwa mtetezi wa La Liga nchini Hispania. Katika mchezo huo Al-Ahil alipigwa bao 5 na mabingwa hao wa Hispania licha ya wao kupata goli 3.
Kwa mara ya kwanza kamera zilimpata Murtaza mwezi Januari mwaka huu akiwa amevaa mfuko wa rangi ya blue na nyeupe na nyuma ya jezi kukikiwa na namba 10 iliyoandikwa kwa wino wa kalamu ya kawaida huko Kabul nchi Afganistani. Miezi 11 baadae, picha ya shujaa wa Murtaza imekuwa kitu halisi. Jana Murtaza amekuana na Messi na kuingia nae mpaka katikati ya uwanja.
Ikumbukwe pia mtoto Murtaza, mwezi mmoa tu baada ya kuvaa mfuko wa jezi ya Argentina, shirika la Umoja wa Mataifa linalojihusisha kukusanya fedha kwa ajili ya watoto lilimzawadia “tshirt” halisi yenye saini ya shujaa huyo wa soka Baba wa mtoto huyo anaefahamika kama Muhammad Arif Ahmadi, alizungumza na kituo cha television cha CNN kuwa mwanae alipopata jezi ya Messi, alijona mwenye furaha kubwa sana maishani.

Mimi nawe tunaoishi katika dunia kijiji, tuna ndoto gani ya kuifanya furaha yetu iwe kitu halisi. Dr. Martin Luther King Jr, alisema anayo ndoto. Mahatma Gandhi kiongozi wa mapinduzi na uhuru wa India aliamini katika ndoto ya kuwaunganisha Wahindu kupinga ukoloni wa Uingereza bila kutumia nguvu, vurugu au vitendo vya kihalifu.
Mtoto wa miaka 6 kaonesha ndoto yake bila aibu na miezi 11 baadae amekutana na shujaa wake kwa kusimama nae uwanjani mbele ya mamilioni ya watu duniani kote walioweza kushuhudia tukio hili.
Ndugu yangu unaesoma makala hii, bado hujachelewa, weka ndoto yako kwa kuwashirisha watu wajue nini unataka kuufanyia ulimwengu.
Ipo siku kuna mtu utakutana nae anaeweza kujenga daraja la wewe kufikia ndoto yako.
Kama una ndoto washirikishe wengi wajue nini unataka kufanya. Kuna ambao watakucheka, kuna ambao watakubeza, ila kuna siku utakutana na mtu anaeweza kuwa sehemu ya ndoto na furaha yako kutimia.
Jenerali Colin Powell ambae alipata kuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani alipata kusema, 
“A dream doesn't become reality through magic; it takes sweat, determination and hard work”
Ndoto haitokei kuwa halisi kwa njia ya miujiza, inahitaji kutoa jasho, kudhamiria na kufanya kazi kwa juhudi.
Mtoto wa miaka 6 aliweka ndoto kwa matendo kwa kuchukua mfuko wa plastic, akavaa na kujitokeza hadharani bila kujali aibu au hatari za vita huko Kabul, Afghanistan.
Wewe msomaji wangu, unaona fursa gani, unachukua hatua gani ya kimkakati ili kufikia malengo yako. Je, ni aibu, maneno ya watu au watu watakuonaje ukichukua hatua ya kwanza kupiga hatua kuelekea kwenye ndoto ya furaja maishani mwako?
Dk. A. R. Bernard mmmoja wa viongozi wa dini katika wa New York alipata kusema mafaniko ya mtu ni jumla ya maamuzi anayofanya kwa kujua au kutokujua katika maisha yake juu ya sayari dunia.
Nakutakia siku njema.
Fredrick Matuja
fmatuja@hotmail.com(P.T)

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช