.

SHIRIKA LA TTCL LAHUJUMIWA ZAIDI YA MILIONI 600 KIGOMA

Dec 24, 2016

NA MAGRETH MAGOSSO, KIGOMA
Wafanyabishara wa vyuma chakavu wamedaiwa kuihujumu miunodmbinu ya  Kampuni ya TTCL mkoani Kigoma hali na kuisababishia kampuni hiyo hasara ya zaidi ya  Sh. Milioni  650.
                                                          
Akizungumza jana mjini Ujiji mkoani hapa, Meneja wa shirika hilo Robert  Miala, alisema wafanyabiashara hao wamekuwa chanzo cha kuharibiwa kwa miundombinu ya shirika hali inayoathiri utendaji kazi kwa wateja wake, na kwamba baadhi ya maeneo yaliyoadhirika sana na kutokana na uharibifu huo wa miundombinu katika wilaya ya kigoma mjini katika kata ya Gungu ambayo kwa sasa haina mawasiliano kabisa.

Alieleza kuwa, kitendo cha kuhujumu miundombinu ya mali za umma ni janga kwa taifa kuimarika kwa uchumi, ingawa wezi wa miundombinu hiyo wanahisi wanaondoakana na umaskini wa kipato lakini watambue serikali inaingia gharama kubwa katika kukarabati upya maeneo yaliyoharibiwa ambazo wengi huiba kwa ajili ya kupata madini ya kopa yaliyomo kwenye nyaya hizo.

Miala  alisema katika mkoa wa kigoma eneo ambalo ni salama ni wilaya ya Kibondo tu,huku kigoma mjini na kasulu ni vinara wa kuhujumu miundombinu ya TTCL hali inayowapa changamoto katika kurudisha huduma kwa wateja,ambao wengi wao ni mashirika ya umma na sekta binafsi wenye uhitaji wa huduma hiyo.

“wizi huu ni wa muda mrefu,nimeukuta lakini fedha nyingi zimepotea katika hili,na tunarudisha huduma kwa kile tunachopata ili wadau wetu muhimu wasikose huduma yetu,lakini wandishi tusaidieni kuelimisha umma,kuwa wizi wa miundombinu ya mawasiliano ya serikali ni kosa la uhujumu uchumi,tumeshirikisha jeshi la polisi ili wahalifu watiwe nguvuni” alifafanua Meneja huyo.

Alipohojiwa hilo Kamanda wa Polisi Kigoma Ferdinand Mtui akiri kupokea malalamiko toka kwa shirika hilo na Desemba,20,mwaka huu saa 8.45 mchana  eneo la Rose Corner Manispaa ya kigoma Ujiji wilayani kigoma walifanikiwa kuwakamata wafanyabiahshara  watatu wa chuma chakavu wakiwa na kilo 12 za nyaya za TTCL ambazo  tayari zilichubuliwa gamba na kuzificha ndani ya pipa la chuma.

Kamanda huyo alisema watuhumiwa wote ni wakazi wa mwanga manispaa ya kigoma ujiji na watafikishwa mahakamani pindi uchunguzi utakapokamilika na kutoa rai kwa jamii watambue umuhimu na faida ya kutunza miundombinu ya taifa ni moja ya kuwafichua wahalifu wanaohujumu uchumi wa taifa,ili wachukuliwe hatua za kisheria na iwe funzo kwa wengine.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª