Breaking News

Your Ad Spot

Dec 18, 2016

TRUMP AITAKA CHINA KUHIFADHI MANUWARI YA MAREKANI

Rais mteule wa Marekani Donald Trump
Rais mteule wa Marekani Donald Trump ,amesema kuwa Marekani inafaa kuiomba China kuiweka manuwari ya Marekani iliopatikana katika bahari ya kusini mwa taifa hilo.
Awali Trump alikuwa ameishutumu Beijing kwa kuiba manuwari hiyo katika maji ya kimataifa.
China iliichukua manuwari hiyo katika pwani ya Ufilipino wakati meli za wanamaji wa Marekani zilipojaribu kuichukua, hatua ilioikasirisha Marekani.
Beijing imesema kuwa itaikabidhi Marekani, lakini matamshi ya Trump huenda yakatatiza mpango huo.
Hii ni mara ya tatu katika wiki kadhaa kwa yeye kukosana na China.
Wakati huohuo Trump amekamilisha ziara yake ya wiki tatu ya kusherehekea ushindi , katika mji ulioshuhudia mkutano mkubwa zaidi wakati wa kampeni zake.
Alipowasili katika mji wa Mobile, Alabama, Trump alikaribishwa na kundi la wanawake waliovalia mavazi ya kitamaduni yanayovaliwa na jamii za kusini mwa Marekani.
Katika uwanja uliojaa pomoni, Trump aliahidi kwamba atatimiza ahadi yake ya kujenga ukuta kwenye mpaka wa Mexico na Marekani.
Trump ataapishwa tarehe 20 mwezi Januari.BBC

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages