.

TRUMP AKEJELI MADAI KUWA URUSI ILIVURUGA UHAGUZI

Dec 13, 2016

Trump awakosoa majasusi wa Marekani
Donald Trump ametoa shutuma mpya kupinga madai ya ujasusi nchini Marekania kuwa wadukuzi nchini Urusi waliingilia uchaguzi wa Marekani.
Rais huyo mteule wa Marekani pia aliuliza kuhusu ni kwa nini madai hayo ya udukuzi hayakutolewa kwa umma kabla ya kufanyika kwa uchaguzi.
"Kabla wadukuzi hawajakamatwa kwenye kitendo, ni vigumu sana kubaini ni nani alikuwa akidukua. Mbona hili halikusemwa kabla ya uchaguzi?" Trump aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter leo Jumatatu.
Siku ya Ijumaa maafisa wa CIA walivyambia vyombo vya habari nchini Marekani kuwa, wadukuzi wa Urusi walijaribu kuvuruga uchaguzi na kumpendelea Trump.
Timu ya ilijibu madai hayo na kusema: "Hawa ni sawa na wale watu waliosema kuwa Saddam Hussein alikuwa na silaha za maangamizi."
Trump yuko nyuma ya Trump katika wingi wa kura kwa karibu kura milioni 2.8 licha ya yeye kushinda kwa kura nyingi zaidi za wajumbe katika historia ya Marekani.BBC

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช