.

UZINDUZI WA KAMPENI ' BODABODA' CHANGIA DAMU MWENZIO AISHI YAVUNA DAMU 45 HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI NA KUTOA MISAADA KWA WATU WA AJALI (MOI)

Dec 17, 2016

Afisa Ustawi wa Jamii Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto - Mango wa Taifa wa Damu Salama, Desteria Nanyanga akizungumza na madereva wa Pikipiki (BODABODA), wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya 'Bodaboda changia Damu mwenzio aishi' iliyofanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Meneja Ustawi wa Mahusiano ya Jamii, Taasisi ya Tiba, Mifupa na Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu Muhimbili (MOI)  Jumaa  Almasina (kulia) akifurahia jambo na  Msemaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili,  Aminieli Elgaesha  wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya 'Bodaboda changia Damu mwenzio aishi' iliyofanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Dar es Salaam.
Msemaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili,  Aminieli Elgaesha (kushoto) na Meneja Ustawi wa Mahusiano ya Jamii Taasisi ya Tiba, Mifupa na Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu Muhimbili (MOI)  Jumaa  Almasi , wakijadiliana jambo wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya 'Bodaboda changia Damu mwenzio aishi' iliyofanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Dar es Salaam
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Makwaia Mkani akiwapungia mkono madereva hao kwa lengo la kuwasalimia
Balozi wa Bodaboda Jijini  Dar ws Salaam, Leodiger Mssawe, akimpatia moja ya zawadi walizoziandaa kwa kuwagawia wagonjwa wa Ajali waliolazwa katika Taasisi ya Mifupa MOI na kujionea na ikiwa nimoja ya kujifunza kwa kujionea ili wawapo Barabarani waweze kuwa na umakini
Mmoja wa madereva wa Pikipiki almaarufu kwa jina la Bodabodamba, Faustine Matina akimpaita mkono wa kumtakia apone haraka mara baada ya kumpa msaada  mmoja wa mgonjwa aliyekuwa amepata ajali aliyelazwa katika Taasisi ya Mifupa Mhimbili MOI
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi isiyo ya Kiserikali inayo tambulika kama (APEC)  Shirika la Kupunguza Umasikini na Kutunza Mazingira Tanzania (APEC), Respicius Timanywa (kulia) akitoa msaada wa baadhi ya vitu walivyo wapelekea wagonjwa wa Ajali waliolazwa katika Taasisi ya Mifupa MOI, mara baada ya kuchangia chupa za Damu 45 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Dar es Salaam, 'ambapo alisema' Taasisi  amabayo imeanzishwa tangu mwaka  2002 na kupata cheti cha ukubalifu 1942, mwaka 2007, Taasisi hii ndio mwasisi wa mafunzo ya Usalama Barabarani, Polisi Jamii na Ujasiliamali kwa waendesha Pikipiki Tanzania na tangu  15 Des mwaka 2010 ambapo tuliasisi mafunzo ya Bodaboda Mkoani Dar es Salaam imepelekea tuweze kuwafikia Bodaboda zaidi ya Lakitatu Tanzania na tumeweza kuwafikia Kata, Tarafa na Wilaya zote za Mikoa yote ya Tanzania Bara ispokuwa Mwanza na Kagera, Tumeunda vikundi vya ujasilai mali na tumeunda, tumeunda vikundi vya Polisi jamii na tumeunda vikundi ya Bodaboda Trafik ili waweze kukamatana wenyewe kwa wenyewe,  tumewaandaa katika mfumo wa kutii sheria bila shuruti na tumeweka mazingira mazuri na wakawema mahusiano mazuri na Jeshi la Polisi hasa wale Bodaboda tunao wapa mafunzo, na nikwanini APEC tumeamua kufanya Maadhimisho ya Siku ya Bodaboda kuchangia Damu ni kwamba Tarehe 15 Des ndipo yalipoanza mafunzo haya kwa lengo kubwa lililotutuma kuanzisha Kampeni ya Bodaboda changia Damu mwenzio aishi ni kwa sababu Daktari anapowahudumia wagonjwa na wagonjwa wale wanamfia mikononi mwake lakini sisi watu wa APEC tunapo wahudumia watu wa Bodaboda tunashuhudia ajali huko vijijini wanatufia mikononi mwetu, kwamaana hiyo swalahili likatugusa sana, tukaamua kuungana na Serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, madaktari, manesi na wauguzi ilikwamba kuhakikisha tunachangisha Damu na Bodaboda waokowe maisha ya watu wengine kwa lengo la kuokoa maisha ya Bodaboda wenyewe na kuokoa maisha ya Mama wajawazito wanao kufa kwa wakati wanapojifungua kwa kukosa Damnu na pia tuokoe maisha ya mtoto huyu ambaye anatarajia kufa kwa kukosa Damu, hawa ndio vijana hawandio wenye uwezo na hawa ndio wenye nguvu na niwenye moyo wa kujitolea kuchangia Damu, napenda kuipongeza Serikali yetu inaoy ongozwa na Rais John Pombe Magufuli, nipongeze madaktari na manesi na wauguzi kwa kutupa ushirikiano huu, pia niipokeze Wizara ya Afya kwakutupa ushirikiano wa kazi nzuri inayofanyika na Pia napenda kumpongeza kwa moyo wote Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ndugu yetu na kijana mwenzetu, Paul Makonda kwa namna anavyo ipa ushirikiano APEC na kwanamna alivyo liandaa tukio hili na yeye ameonesha nikiongozi anaye wapenda Bodaboda na ninaimani kwa msimamo aliouonyesha Dar es Salaam na kushirikiana na APEC, tumuombee kwa Mwenyeezi Mungu apate kuwahudumia watanzania kwa wingi zaidi,


Meneja Ustawi wa Mahusiano ya Jamii Taasisi ya Tiba, Mifupa na Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu Muhimbili (MOI)  Jumaa  Almasi (kushoto) akizungumza kwa niaba ya Taasisi, alianza kwa kusema, Nawashukuru kwa kujitowa kwenu na mlicho kitoa kwenu mwaona ni kidogo ila kwetu twaona ni kikubwa na mmewafanya wagonjwa wetu kuwa na mtazamo wakujiona ni sehemu ya jamii ya kitanzania inawafariji, na ninyi ni mashahidi kwa kujionea wenyewe kwa ule mtazamo wakauli inayo sikika mitaani nawaomba muondoke mkiwa na mtazamo mwingine, Jumaa aliuliza swali kwa madereva hao je, kunamtu mmemuona amekatwa mguu? basi kwa niaba ya Kaimu Mtendaji wa Taasisi ya Tiba, (MOI) amenituma kuwapa salamu,  anawashukuru wote walio jitolea Damu na michango yenu na anawaomba mzidi kutembelea wagonjwa wetu na wagonjwa popote walipo kwa kuwafariji kama mlivyofika hapa kwetu na pia napenda kusema asante kwa niaba ya uongozi mzima wa Taasisi ya MOI wote wanasema kwa pamoja Asanteni sana na Mungu awabariki
Picha ya pamoja

Naibu Katibu Mkuu wa Shirika la Kupunguza Umaskini na Kutunza Mazingira (APEC) akizungumza jambo na wanahabari wakati wa Uzinduzi wa 'Bodaboda changia Damu mwenzio aishi' iliyofanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Chama Cha madereva na wamiliki wa Pikipiki Mkoa wa Dar es Salaam,  Maiko Masawe kwa upande wakea aliseama anayo furaha kwa zoezi hili kwa kulikamilisha katika hali ya umoja wakishirikiana na viongozi wao wa APEC na pamoja na Jeshi la Polisi kwa kujitowa kwa hali na mali kujumuika nao na akaendelea kusena, kwa kuishukuru Wizara ya Afya kwa kukubali wito wao


0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช