Breaking News

Your Ad Spot

Dec 22, 2016

WATU 11 KUFIKISHWA KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA WIZI WAI YA SH. MILION 50, KWENYE ATM


NA MAGRETH MAGOSSO,KIGOMA
WATU 11 watafikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi  Wilaya ya Kigoma Mkoa wa Kigoma ,ili kujibu tuhuma za kumiliki na kufanikiwa kutoa fedha zaidi ya Sh.Milioni 50 katika vibanda viwili tofauti vya ATM za Benki mbalimbali katika manispaa ya kigoma Ujiji.

Akizungumza na ofisini kwake Kigoma-ujiji,Kamanda wa Polisi mkoani humo Ferdinand Mtui alisema kwa ushirikiano na raia wema wamegundua mtandao wa watu kumiliki kadi za ATM za watu na kutumia kadi hizo watakavyo.

Alisema  Desemba,20,mwaka huu,saa 5.30 usiku atuhumiwa sita walishikwa na kadi 27 wakiwa na jumla ya fedha kiasi cha sh.milioni 4,830,000 katika kibanda cha mashine za kutolea fedha benki ya NMB ambapo ni kinyume cha sheria.

Alisema mtuhumiwa namba moja alikutwa na ATM kadi  6 na fedha taslimu 450,000.wa pili alikuwa na kadi 6 na fedha kiasi cha sh.milioni 2.2,wa tatu alikuwa na kadi 7 na fedha kiasi cha sh.milioni 1.1 ,mtuhumiwa wa Nne akutwa na kadi 2,fedha sh.450,000wa tano kadi 4630,000 na mtuhumiwa wa sita akutwa na kadi 2 bila fedha.

Kamanda Mtui alifafanua kukamatwa kwa watu watano wengine wa tukio la kumiliki kadi za ATM kutoka benki mbalimbali ikiwemo CRDB,NBC,CRDB na Benki ya Posta  kuwa,Desemba,21,2016 saa  3.15 wakiwa katika kibanda
cha mashine ya kutoa fedha cha hopsitali ya rufaa ya maweni watuhumiwa hao majina hifadhini walikutwa na jumla ya kadi 73 na fedha taslimu sh.milioni 7.110,000  katika mcghanganua ufuatao.

“mtuhumiwa namba moja alikuwa fedha sh.milioni 1.4,na kadi 17 kutoka benki ya CRDB,wa pili alikuwa na sh. Milioni 1.6 nakadi za CRDB 24, watatu akutwa na kadi 11 na fedha sh.milioni 2.7,mtuhumiwa wa Nne alikuwa na kadi moja bila fedha na tano alikutwa na fedha sh.milioni 1.5 na kadi 17 zote ni crdb benki.

Mtui alieleza kuwa,watuhumiwa wamekiri kumiliki kadi hizo kupitia ofisi yao yaliyoitaja kwa jina la Samaria Shopping Center iliyopo barabara ya Lumumba hapo kigoma ujiji na askari waliipekua ofisi hiyo na kukamata kadi 452 za benki mbalimbali.

Uchunguzi wa kubaini uhalali wao wa kumiliki kadi na wamiliki halali wa kadi hizo na kukamilika kwa uchunguzi huo ni hatua ya kujibu tuhuma hizo mahakamani,Huku akitoa rai kwa wananchi wachunge   mali zao kwa kipindi hiki cha sikukuu ya krisimasi na mwaka mpya .

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages