Breaking News

Your Ad Spot

Dec 20, 2016

WAVUVI KIGOMA WAKATAZWA KUVUA DAGAA AINA YA KAUZU NA UGALA ZIWA TANGANYIKA

Kigoma
NA MAGRETH MAGOSSO, KIGOMA
Kitengo Cha Ubora wa Samaki  na  Udhibiti wa Rasilimali za Uvuvi Kanda ya Kigoma   imewataka Wavuvi waache kuvua  Dagaa aina ya Kauzu na Ugala waliopo katika Ziwa Tanganyika lililopo Mkoa wa Kigoma, na wazingatie sheria  ya uvuvi ya mwaka 2009 na kanuni za mwaka 2005,ili wafanye shughuli zao kwakulinda na kuhifadhi mazalia ya samaki na dagaa waliopo katika ziwa hilo.



 Akizungumza na Jamboleo  jana katika Ofisi za kanda hiyo iliyopo Mwalo na Kata ya Kibirizi Manispaa ya Kigoma Ujiji Ofisa Mfawidhi kitengo  hicho Rodlick Mahimbali alisema kutokana na wadau wa mazao ya ziwa Tanganyika(samaki,dagaa) kukiuka sheria za uvuvi bora,kitengo hicho kimefanikiwa kukusanya kiasi  cha fedha sh.Milioni 21.5 katika kipindi cha miezi mitatu tu,kwa maana ya Octoba hadi Desemba 2016.



“wamiliki wa mitumbwi ya kuvulia samaki na dagaa wanajua wajibu wao,ni pamoja na kununua nyavu rafiki wa kulinda mazalia ya samaki na dagaa,ambapo zana aina ya nyavu  zote ziwe  zaidi ya Nchi tatu na si chini ya Nchi mbili,lakini wao wanapenda kutumia makokoro,neti za mbu ambazo kiujumla wanavua watoto wa samaki na wanaharibu mazalia” alisema Ofisa Mahimbali.



Alifafanua kuwa,ili kulinda na kuhifadhi vizazi vya dagaa na samaki Wavuvi hawana budi watumie zana za uvuvui zenye kiwango cha ubora wa nyavu zenye zaidi ya nchi 3 sanjari na  kuvua kwenye kina kirefu cha maji,ambako kuna samaki wakubwa wenye tija ya kuimasrisha afya za walaji na si bora kuvua ambayo inawaghalimu pindi wanaposhikwa na serikali kwa kupewa adhabu ya faini na kuharibiwa zana haramu.



Mahimbali aliongeza kwa kusema serikali ina lengo la kulinda mazao hayo ili yawe endelevu kwa leo na kiazazi kijacho na uvuvvi haramu ni kikwazo  kwa taifa kujiendesha kitaalamu katika kukuza uchumi wa mtu binafsi na taifa kwa ujumla na kuwashauri washirikiane kuwaibua wamiliki na wavuvi wanaovunja sheria ya uvuvi ya mwaka 2009,ili kudhibiti uvuvi  wa zana haramu.



Alipohojiwa  Mwenyekiti wa Chama Cha Wavuvi  mkoani humu Sendwe Ibrahimu alisema uhalisia wa mambo hakuna mmiliki na mvuvi asiyejua wajibu wake katika sekta ya mazao ya ziwani,lakini kutokana na changamoto ya zana bora za uvuvi ndio chanzo cha uvuvi haramu,mitumbwi haina uwezo wa kufika katika kina stahiki sana cha maji hali inayowalazimu wavue karibu na mazalia ya samaki.



Aliwashauri wadau wa sekta hiyo watumie vikundi mtambukwa kuwakopesha zana za kisasa za uvuvi,ili wavue samaki katika kina kirefu cha maji(gazini) kwa lengo la kuvua samaki na dagaa wakubwa ambao bado hawajavuliwa tangu kuumbwa kwa dunia kwa kuwa zana wazitumizo ni za kale ambazo hushawishi baadhi kutumia zana haramu hasa neti za mbu,makokoro  na sumaku ni  nyavu za nchi  ya Burundi,ambayo haichagui samaki wala dagaa.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages