.

YANGA YA LWANDAMINA YAIGARAGAZA JKT RUVU 3-0

Dec 18, 2016

Kikosi cha Yanga SC leo dhidi ya JKT Ruvu FC
Kikosi cha JKT Ruvu SC leo dhidi ya Yanga FC 
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
MABINGWA watetezi wa ligi kuu Vodacom Yanga imefanikiwa kupanda hadi kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JKT Ruvu jioni ya leo Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi 36 baada ya kucheza mechi 16 na kuishusha Simba iliyomalizia kileleni mzunguko wa kwanza kwa pointi zake 35. 
Winga Simon Msuva aliweza kuwa nyota wa mchezo huio baada ya kufanikiwa kuifungia timu yake goli mbili katika dakika ya 57 na 90 huku lingine akipiga pande safi linalomshinda beki Michael Aidan na kuingia nao nyavuni dakika ya 38.
JKT Ruvu waliweza kucheza kandanda safi na wakionekana kutumia mashuti ya mbali kuweza kujaribu nafasi ya kufunga huku mshambuliaji wake Atupele Green akikosa nafasi mbili za wazi.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Yanga, Mholanzi Hans van der Pluijm alikuwepo jukwaa kuu kufuatilia mchezo, wakati kiungo mpya kutoka Zambia, Justin Zulu pia akiwa jukwaani kwa sababu bado hajapatiwa kibali cha kufanya kazi nchini. 
Baada ya mchezo, kocha msaidizi Juma Mwambusi amesema kuwa waliingia uwanjani na mpango wakushinda na wamefaniklisha hilo ingawa mchezo ulikuwa mgumu sana kwao.
Mechi hiyo ilichezeshwa na Hery Sasii akisaidiwa na Hellen Mduma na Kassim Mpanga wote wa Dar es Salaam.
Matokeo mengine ni:
Mwadui 1-0 Toto Africans Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, Mbeya City 0-0 Kagera Sugar Uwanja wa Sokoine, Mbeya na Ruvu Shooting 1-1 Mtibwa Sugar Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani.
Kikosi cha Yanga kilikuwa; 
Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Haruna Niyonzima, Mwinyi Hajji Mngwali, Kelvin Yondan, Vincent Bossou, Simon Msuva, Thabani Kamusoko/Geoffrey Mwashiuya dk84, Donald Ngoma, Amissi Tambwe/Said Juma ‘Makapu’ dk55na Deus Kaseke/Obrey Chirwa dk90

JKT Ruvu: Hamisi Seif, Michael Aidan, Edward Charles, Yussuf Chuma, Kelvin Nashon/Naftal Nasho dk66, Rahim Juma, Ally Bilal/Mussa Juma dk77, Hassan Dilunga, Najim Magulu, Atupele Green/Saad Kipanga dk77 na Edward Joseph.
Mshambuliaji wa Yanga SC,Deus Kaseke (katikati) akiwatoka mabeki wa timu ya JKT Ruvu leo katika uwanja wa Uhuru mchezo uliomaizika kwa Yanga SC kuibuka na ushindsi wa goli 3-0 leo jijini Dar es Salaam. 
Mshambuliaji wa timu ya JKT Ruvu ,Naftal Nashon (wakwanza kulia) akimtoka beki wa timu ya Yanga leo katika uwanja wa Uhuru mchezo uliomaizika kwa Yanga SC kuibuka na ushindsi wa goli 3-0 leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba akijadiliana jambo na Mbunge wa Chalinze, Ridhiwan Kikwete wakati wa mechi ya ligi kuu kati ya JKT Ruvu na Yanga leo Jijini Dar es salaam.
Kiungo mpya kutoka Zambia, Justin Zulu (katikati) akiwa jukwaani kwa sababu bado hajapatiwa kibali cha kufanya kazi nchini. 
Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª