Breaking News

Your Ad Spot

Jan 18, 2017

CHEYO: SERIKALI NDIYO YENYE MAMLAKA YA KUTANGAZA NJAA

Na Lilian lundo- MAELEZO
Serikali ndiyo yenye mamlaka ya kutangaza ikiwa nchi inakabiliwa na janga la njaa na wala si taasisi, asasi za kiraia au wanasiasa.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Chama cha UDP John Cheyo wakati wa mahojiano na mwandishi wa habari hii alipokuwa akitoa maoni yake kuhusu mijadala mbalimbali inayoendelea katika vyombo mbalimbali vya habari kwamba Tanzania imekabiliwa na tatizo la njaa.

Cheyo alisema kuwa, huwezi kusema nchi ina njaa wakati vyakula vipo katika masoko mbalimbali hapa nchini.
Amewataka watanzania kutofautisha kupanda kwa bei za vyakula na janga la njaa.

Aidha, Cheyo alisema kuwa tatizo hilo tayari limetatuliwa na Serikali kwa kutoa tani milioni 1.5 za mahindi  ambazo zitasambazwa nchi nzima kwa ajili ya wananchi kununua.

Aliendelea kwa kusema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa mahindi hayo kuuzwa kwa uangalifu kwani gharama yake itakuwa ni ya chini, hivyo kuna watu ambao watajitokeza kununua kiasi kikubwa na kwenda kukihifadhi kwa ajili ya kukiuza kwa gharama ya juu baadae.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages