.

KAMATI YA BUNGE YA BAJETI YATEMBELEA BANDARI

Jan 17, 2017


Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Injinia Edwin Ngonyani (Mb) (wa kwanza kulia) akisisitiza jambo mbele ya Kamati ya Bunge ya Bajeti wakati Kamati hiyo ilipotembelea Bandari ya Dar es Salaam mapema. Katikati ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Hawa Ghasia(Mb). Kamati za Kudumu za Bunge zimeanza shughuli zake jana ambapo katika wiki hii takribani Kamati za Kisekta 12 zitakuwa zikifanya ziara za kukagua miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali nchini kabla ya kurejea Mjini Dodoma kwa ajili kuendelea na vikao vyake.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti Mhe. Hawa Ghasia (Mb) akizungumza wakati Kamati hiyo ilipotembelea Bandari ya Dar es Salaam.

Wajumbe wa Kamati ya Bajeti wakiendelea na Kikao.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti Mhe. Hawa Ghasia (Mb) akimueleza jambo Kaimu Meneja wa Bandari wa Dar es Salaam Bw. Nelson Mlali wakati wa ziara hiyo.

Kaimu Meneja wa Bandari wa Dar es Salaam Bw. Nelson Mlali akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti wakati wa ziara hiyo. (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช