.

MAJALIWA AZINDUA BARABARA YA MWANAKWEREKWE HADI FUONI- ZANZIBAR

Jan 12, 2017


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua barabara ya Mwanakwerekwe hadi Fuoni yenye urefu wa kilomita 4.1 iliyopo Zanzibar Januari 11, 2017. Kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, Ali Karume .
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia baada ya kuzindua barabara yenye urefu wa kilomita 4.1 ya kutoka Mwanakwerekwe hadi Fuoni Zanzibar ikiwa ni moja ya shughuli za sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar, Januari 11, 2017. Katikati ni Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa rais wa Zanzibar, Mohammed Abood na Kulia ni Mkuu wa mkoa waMjini Magharibi, Mohammed Mahmoud.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa Zanzibar wakati alipowasili kwenye eneo la Barabara ya Mwanankwerekwe hadi Fuoni kufungua barabara hiyo yenye urefu wa Kilomita 4.1 Januari 11, 2017. Kushoto ni Waziri wa Ujenzi, , Mawasiliano na Usafirishaji, Ali Karume.
Baadhi ya wananchi wa Zanzibar wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kuzindua barabara ya Mwanakwerekwe hadi Fuoni yenye urefu wa Kilomita 4.1 ilyopo Zanzibar Januari 11, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki katika dua iliyosomwa baada ya kuzindua barabara ya Mwanakwerekwe hadi Fuoni yenye urefu wa Kilomita 4.1 iliyopo Zanzibar Januari 17, 2017.Wengine pichani kutoka kushoto ni Spika wa Baraza la Wawakilishi, Zubri Ali Maulid, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mohammed Mahmoud na kulia ni Waziri wa Ujenzi, Mawsiliano na Usafirishaji, Ali Karume. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช