Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza na Mwenyekiti wa Taasisi ya Kingdom Leadership Network
Tanzania Ibrahimu Kaduma aliyemtembelea Makamu wa Rais na kumuelezea
mikakati ya kuanzisha Chuo cha Joseph Business School.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
(kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa Taasisi ya Kingdom Leadership
Network Tanzania Ibrahimu Kaduma aliyemtembelea Makamu wa Rais na
kumuelezea mikakati ya kuanzisha Chuo cha Joseph Business School kushoto
ni Meneja Mradi Dkt Charles Sokile.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa
kwenye picha ya pamoja na ujumbe wa Taasisi ya Kingdom Leadership
Network Tanzania uliomtembelea ofisini kwake, Ikulu jijini Dar es
Salaam.
..............................................................
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameuhimiza
uongozi wa Taasisi ya Kingdom Leadership Network Tanzania kuharakisha
mchakato wa kuanzisha Chuo cha Joseph Business School hapa nchini chuo
ambacho kitatoa mafunzo mbalimbali ya biashara, maadili ya uongozi na
ugunduzi wa mawazo ya biashara ili kusaidia mamia ya Watanzania
kuimarisha shughuli zao za kiuchumi.
Makamu wa
Rais ametoa kauli ofisini kwake Ikulu Jijini Dar es Salaam leo
alipokutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Taasisi ya Kingdom
Leadership Network Tanzania ambao walimtembelea Makamu wa Rais kumweleza
hatua ambazo wamefikia katika uanzishaji wa Chuo hicho.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan amesema wazo la uanzishaji wa Chuo hicho
ulitolewa na Dkt Bill Winston ambaye ni Mwanzilishi wa Winston
Ministries mwaka jana katika Maombezi ya Taifa ambaye yeye alikuwa mgeni
rasmi katika maombi hayo, anasema aliupokea kwa furaha mpango huo kwa
sababu chuo hicho kitasaidia watanzania wengi kupata elimu na ujuzi wa
kuimarisha biashara zao wakati taifa likielekea kwenye uchumi wa
Viwanda.
Amesema
hatua za uanzishwaji wa Chuo hicho hapa nchini ni fursa pekee na nzuri
kwa Watanzania kujifunza ubunifu na ugunduzi katika biashara, maadili ya
uongozi katika biashara ili kuongeza ufanisi katika biashara zao kwa
ajili ya manufaa yao na taifa kwa ujumla hasa katika ulipaji wa kodi.
Kwa
Upande wake, Mwenyekiti wa Taasisi ya Kingdom Leadership Network
Tanzania Ibrahimu Kaduma na Meneja Mradi Dkt Charles Sokile
wamemhakikishia Makamu wa Rais kuwa hatua ambazo wamefikia kwa sasa
katika uanzishaji wa Chuo hicho ni nzuri ambapo mpaka sasa wamepata
majengo kwa ajili ya ofisi na maeneo ya kufundishia na hatua za usajili
wa chuo hicho zipo katika hatua za mwisho.
Wamesisitiza
kuwa wanataka kushirikiana ipasavyo na Serikali katika uanzishaji wa
chuo hicho ambacho kitatoa elimu ya biashara hasa ugunduzi wa mawazo ya
biashara nchini kama hatua ya kutekeleza kwa vitendo dhana ya kuelekea
kwenye uchumi wa viwanda nchini.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269