Breaking News

Your Ad Spot

Jan 27, 2017

MUHIMBILI YATOA MSAADA MWINGINE WA VITANDA, HOSPITALI YA WILAYA YA KIBITI YANUFAIKA


Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Agenes Mtawa akimkabidhi vitanda Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri ya Kibiti, Ayub Ngereza kutokana na hospitali ya halmashauri hiyo kuwa na upungufu wa vitanda vinavyotumiwa na kinamama wakati wa kujifungua.  Mhandisi Ngereza amepokea msaada wa vitanda hivyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Wilaya ya Kibiti.


NA JOHN STEPHEN, MNH
KATIKA kuendelea kuboresha mazingira ya utoaji huduma ya afya ya uzazi kwa akina mama, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imetoa msaada wa vitanda viwili vya kujifungulia  kwa Hospitali ya Wilaya ya Kibiti mkoani  Pwani.
Akikabidhi vitanda hivyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili , Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga, Agnes Mtawa, (pichani anayezungumza na waandishi), amesema  lengo ni kuboresha huduma za afya na kumuwezesha mama kujifungua katika mazingira salama.
"Wenzetu wanahuitaji mkubwa wa vitanda vya kujifungulia hivyo tumeona tuwasaidie, natoa wito kwa Watanzania watambue kwamba hospitali hizi ni za kwetu na zinawahudumia Watanzania hivyo wale wenye nafasi ya kusaidia ni vema wakafanya hivyo ili kuendelea kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto" amesema Sister Mtawa.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo wa Huduma za Uuguzi na Ukunga tatizo la ukosefu wa vitanda husababisha Mkunga kupata shida wakati mama anapojifungua.
Naye  Mhandisi Ujenzi wa Halmashauri ya Kibiti,  Ayub Ngereza akipokea msaada huo kwa niaba ya Mkurugenzi wa wilaya ya Kibiti, ameushukuru uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa msaada  huo kwani utasaidia kuboresha huduma za afya.
Hivi karibuni  Hospitali ya Taifa Muhimbili  ilikabidhi msaada wa vitanda vitano vya kujifungulia  kwa  Hospitali ya  wilaya ya Mafya  ambapo  kwa mujibu wa Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo  Abdalah Bhai walihitaji vitanda vitano ambao ulikidhi  mahitaji.



Mhandisi Ngereza akizungumza na waandishi wa habari leo baada ya kukabidhiwa vitanda hivyo na uongozi wa hospitali hiyo.


Baadhi ya wafanyakazi wa Halmashauri hiyo wakipakia vitanda hivyo kwenye gari leo

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages