.

MWENYEKITI MSTAAFU WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI JAJI MSTAAFU LUBUVA AKABIDHI TAARIFA YA UTENDAJI WAKE WA KAZI WA MIAKA MITANO KWA MWENYEKITI WA SASA WA NEC JAJI WA RUFAA SEMISTOCLES KAIJAGE

Jan 26, 2017

 MAKABIDHIANO: Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Damian Lubuva (kulia) akimkabidhi  Mwenyekiti wa sasa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufaa Semistocles Kaijage (kushoto) taarifa ya utendaji Kazi wake kwa kipindi miaka mitano alichokuwa madarakani.

 Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Damian Lubuva akizungumza na Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Sekretarieti ya Tume hiyo mara baada ya kukabidhi taarifa ya utendaji Kazi wake kwa kipindi miaka 5 alichokuwa madarakani

 Mwenyekiti wa sasa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufaa Semistocles Kaijage akizungumza na Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Sekretarieti ya Tume hiyo mara kupokea taarifa ya utendaji Kazi wa Mwenyekiti Mstaafu wa Tume hiyo Jaji Damiani Lubuva jijini Dar es salaam.


 Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Ramadhan Kailima akizungumza jambo wakati wa makabidhiano hayo jijini Dar es salaam. Katikati ni Mwenyekiti Mstaafu wa Tume Jaji Mstaafu Damian Lubuva na Kulia ni  Mwenyekiti wa Sasa wa NEC, Jaji wa Rufaa, Semistocles Kaijage.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Rufaa Semistocles Kaijage akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti Mstaafu wa Tume Jaji Damiani Lubuva , Wajumbe wa Tume na Secretarieti ya Tume hiyo. Picha na Aron Msigwa - NEC.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª