.

RAIS DK MAGUFULI AMTEUA ANNE KILANGO MALECELA KUWA MBUNGE

Jan 21, 2017

Ikulu, Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli, tarehe 21 Januari, 2017 amemteua Anne Kilango Malecela kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam, imesema, Anne Kilango Malecela ataapishwa kwa mujibu wa taratibu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Anne Kilango ameteuliwa ukiwa ni mfululizo waRais kuteua wabunge kwamujibu wa nafasi yake, ambapo wiki iliyopita aliwateua Alhaj Abdalla Bulembo na Profesa Palamagamba Kabudi.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช