Breaking News

Your Ad Spot

Jan 26, 2017

SAKATA LA MAJERUHI ALIYEPIGWA NA MCHINA LACHUKUA SURA MPYA

HUJU
Baadhi ya wafanyakazi wakizungumzia hali ilivyokuwa juu ya kuwepo kwa taarifa ya kupigwa kwa wenzao mgodini hapo.
HUJU 1
Eneo la mgodi Kazi zikiendelea .
HUJU 2
Baadhi ya mawe ambayo yamekuwa yakitoa dhahabu yakiwa yamekusanywa sehemu moja
HUJU 3
Wafanyakazi wa kampuni ya RZ wakijiandaa kuingia kwenye mashimo kwaajili ya utoaji wa mawe ya dhahabu.
HUJU 4
Meneja wa Mgodi huo,Guixue Liu (kulia),akiwa na Mwanasheria wa Mgodi Huo Frances Kiganga wakiangalia namna kazi zinavyoendelea kwenye mgodi.

IMEANDALIWA NA MADUKAONLINE

SAKATA la watu wawili  wanaodaiwa kupigwa na raia wa kigeni wa China akiwemo aliyelazwa katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Geita limechukua sura mpya baada ya kubainika chanzo chao cha kupigwa ni kuiba mawe yanayodhaniwia kuwa na dhahabu na maji walipokuwa  wakifanya kazi katika mgodi wa dhahabu unaomilikiwa na kampuni ya RZ uliopo katika kijiji cha Mawemeru, Mkoani Geita na siyo kutokana na madai  kupandishwa mishahara.
Tukio hilo limetokea Januari 19 wakati wa zamu ya usiku baada ya mfanyakazi Benedict Lumimi Maduhu kudaiwa  kukamatwa  akiwa na mawe yanayodhaniwa kuwa na dhahabu ndani ya mgodi huo wakati akiwa  zamu usiku na baada ya kukamatwa rafiki yake wa karibu,  Elisha Silivester [26] ambaye naye anatuhumiwa kwa  kuiba maji alifanikiwa kukimbia hadi kituo cha polisi cha Nyarugusu kutoa taarifa kuwa  yeye na mwenzake walikuwa wakipigwa na wachina baada ya kudai waongezewe mshahara.
Akithibitsha tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Geita Mponjoli  Mwabulambo amesema wafanyakazi Bedeicto Lumimi Maduhu walikamatwa na polisi kutoka ndani ya mgodi huo baada ya kukuta tayari  amekamatwa na kufungwa kamba na wafanyakazi wengine wa mgodi huo tayari kwa kumpeleka kituo cha polisi cha Nyarugusu pamoja na mawe yanayodaiwa  kuwa na dhahabu .
Ameongeza kuwa Elisha Silvesta anayedaiwa kuiba maji yeye ndiye aliyekimbia na kutoa taarifa kituo cha polisi baada ya kufanikiwa kutoroka kabla  ya kukamatwa na polisi baada ya kufika eneo la tukio waliwachukuwa watuhumiwa  Benedicto pia wafanyakazia baadhi wa mgodi huo hadi kituo cha polisi kwa mahojinao ikiwa ni pamoja na kuwahoji  baadhi ya wafanyakazi wa mgodi huo akiwemo Elisha mwenywe.
”Taarifa  rasmi za uchuguzi ni kuwa chanzo cha kupigwa kwao ni kutuhumiwa  kwa wizi wa mawe yanayodhaniwa  kuwa  na dhahabu na maji kama nilivyoeleza sisi kama polisi pia baada ya kutokea malalamiko hayo kutoka kwa watuhumiwa  pia wanaotuhumiwa tulichukua jukumu la kuwakamata na kuwahoji na kinachoendelea  sasa ni mchakato wa kukusanya ushahidi  kwa hatua za kisheria  hivyo chanzo ni cha wao kupigwa ni kutuhumiwa na siyo madai ya nyongeza za mshahara”alidai Mponjoli.
Hata hivyo polisi imebainisha wazi kuwa zipo changamoto kwa baadhi ya watu kujenga hoja zinazolenga kujipatia
fedha kutoka kwa wachina kwa kujenga hoja ya  kupigwa na kujeruhiwa vitendo alivyodai polisi haina budi kuyafanyia kazi kwa umakini madai hayo  kwa vile tayari ipo mifano ya matukio ambayo yaliwasilishwa lakini yakaisha kwa walalamikaji  kudai pesa na kutelekeza kesi zao.
Ametoa mfano tukio lililtokea julai 6 mwaka jana la Masanja  Shilomero[25] mkazi wa kijiji Nyamitondo  kudai kushambuliwa na wajiri wake ambao ni raia wa china na kufunguliwa kesi namba CC/278/2016 mlalamikaji aliitelekeza kesi hiyo baada ya kudaiwa alikuwa ameomba na kupewa fedha kutoka kwa walalamikiwa  na kuitelekeza kesi yake.
 Kesi hiyo kushindwa kuendelea na siyo kwamba imetelekezwa na polisi,na tukio jingine amelitaja kuwa ni mchimbaji Richard Kasubi anayelalamikiwa na baadhi ya watu wanaodaiwa kufanya kwake kazi ya kushusha mifuko ya saruji kutoka katika gari kuiweka katika
ghala lake badaye  walidai kudhurika  hata hivyo tayari inadaiwa walilipwa pesa na mlalamikiwa huyo baada ya kutaka malipo kwa ajili ya matibabu na baada ya kiasi cha shilingi 500,000 wanachodaiwa kupewa kukimaliza walianza tena kudai upya na hivyo kuibua mgogoro.
kutokana na uwepo wa mazingira ya aina hiyo polisi wanatakiwa kufanya kazi kwa umakini ili kutenda haki kwa pande zote na kuwa Benedicto na wenzake tayari amefunguliwa kesi ya wizi wa mawe yanaodhaniwa  kuwa na dhahabu katika kituo cha polisi cha Nyarugusu na upelelezi wake unaendelea ikiwemo wanaodaiwa kuwapiga nao wamefunguliwa kesi na inachunguzwa.
Awali akizungumzia matukio hayo Meneja wa mgodi huo wa RZ Gui Xue Liu kupitia msemaji wa kampuni hiyo Francis Beatus Kiganga amesema vitendo vya wizi kwa wafanyakazi wanavyofanya na kisha kuwageuzia kibao kunaweza kuwakatisha tama kuwekekeza katika sekta hiyo ya madini kwani imekuwa  ikiwapa usumbufu mkubwa.
Amesema kwa kawaida wao wamekuwa wanapowakamata  watuhumiwa huamua kuwafukuza kazi badala ya kuwapeleka
kwenye vyombo vya sheria ili kuepuka kupoteza muda na usumbufu na watuhumiwa kutumia mwanya huo huwageuzia kibao hatua waliyodai inaonekana kuwaathiri na kuiomba serikali kulifanyia kazi kwa umakini wimbi hilo la wachina kutuhumwia kupiga watumishi.
Mganga wa zamu katika hospitali hiyo Elias Hambuhambu amethibitisha juzi jioni kwa Elisha Sivesta kulazwa hospitalini hapo kwa madai ya kupigwa na kuwa hata hivyo hali yake ilikuwa inaendelea  vizuri  na alikanusha uwepo uvumi wa kujeruhiwa sehemu za siri za majeruhi huyo kwani alikuwa amewekewa  mpira wa haja ndogo kama hatua ya kawaida kwa wagonjwa wanaolazwa wanaokuwa na madai ya kusikia maumivu ya mwili.
Baadhi ya wafanyakazi wa mgodi huo wakiwemo Amani Silivesta na Annicent Masanja walidai mwenzao elisha aliondoka kwenda kuropiti Kituo cha polisi akijihami baada ya Benedicto kukamatwa akiwa na mawe yanayodhaniwa kuwa na dhahabu wakati alipokuwa  zamu ya usiku na waliondoka na Polisi baada ya yeye kwenda kutoa taarifa na wakati huo wote hakuwa  amepigwa na madai ya kupigwa yamejitokeza siku mbili baada ya kutokea uhalifu huo hivyo kuibua sintofahamu.
Akizungumzia tuhuma hizo Elisha Silvesta akiwa wodini alimolazwa juzi katika hopitali teule ya mkoa wa Geita alikiri kuwa chanzo cha wao yeye na Benedicto kupigwa ni kutuhumiwa yeye  kuiba maji na mwenzake Benedicto kuiba mawe yanaodhaniwa kuwa  na dhahabu  na baada ya kufanikiwa kukimbia alikwenda kutoa taarifa kituo cha polisi  Nyarugusu  kuwa mwenzake Benecto Lumimi Maduhu alikuwa amefungwa kamba akipigwa bakora na wachina ili kujihami

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages