Spika wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai (Mb)
akimkaribisha Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran Nchini Tanzania Mhe.
Mohammad Dehghani aliefika Ofisini kwake Dodoma kwa ajili ya kuwasilisha
salam na mualiko rasmi kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislam
ya Iran ukimualika Mheshimiwa Ndugai kutembelea Bunge la Iran kwa lengo
la kuimarisha uhusiano wa mabunge haya mawili.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai (Mb) akipokea mwaliko toka kwa Balozi wa Jamhuri
ya Kiislam ya Iran Nchini Tanzania Mhe. Mohammad Dehghani mara aliefika
Ofisini kwake Dodoma kwa ajili ya kuwasilisha salaam na mualiko rasmi
kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislam ya Iran ukimualika
Mheshimiwa Ndugai kutembelea Bunge la Iran kwa lengo la kuimarisha
uhusiano wa mabunge haya mawili.
Spika wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai (Mb)
akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran Nchini Tanzania Mhe.
Mohammad Dehghani aliefika Ofisini kwake Dodoma kwa ajili ya
kuwasilisha salaam na mualiko rasmi kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri
ya Kiislam ya Iran ukimualika Mheshimiwa Ndugai kutembelea Bunge la
Iran kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa mabunge haya mawili.
Spika
wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai (Mb)
mara baada ya kupokea mwaliko kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Kiislam ya Iran
uliowasilishwa na Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran Nchini Tanzania
Mhe. Mohammad Dehghani kutembelea Bunge la Iran kwa lengo la kuimarisha
uhusiano wa mabunge haya mawili (PICHA ZOTE NA OWEN MWANDUMBYA, BUNGE)
Na Owen Mwandumbya, Bunge
Spika wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai (Mb)
amesema Bunge la Tanzania litaendelea kudumisha mahusiano yaliyopo na
Bunge Irani ili kubadilishana uzoefu katika maeneo mbalimbali.
Mhe.
Ndugai ameyasema hayo Mjini Dodoma leo alipokutana na Balozi wa Jamhuri
ya Kiislam ya Iran Nchini Tanzania Mhe. Mohammad Dehghani aliefika
Ofisini kwake Dodoma kwa ajili ya kuwasilisha salaam na mualiko rasmi
kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislam ya Iran ukimualika
Mheshimiwa ndugai kutembelea Bunge la Iran kwa lengo likiwa...
ni kuimarisha uhusiano wa nchi zetu mbili.
ni kuimarisha uhusiano wa nchi zetu mbili.
Nashukuru
kwa Salaam hizi kutoka kwa Spika wa Bunge la Iran na naahidi
kuzifikisha salaam hizi kwa Waheshimiwa Wabunge na pia Ofisi yangu
itatolea taarifa juu ya mwaliko huu na kujipanga kutembelea Bunge la
Irani kwa kadri muda utakavyoruhusu. Alisema Mhe. Ndugai.
Pamoja na
mwaliko huo wa Kibunge kutoka kwa Spika wa Bunge la Iran, Balozi huyo
Irani pia alitumia fursa hiyo kuwasilisha ombi la Rais wa Iran Mhe.
Hassan Rouhani la kumwalika Mhe. Ndugai ili aweze pia kuhudhuria
Mkutano wa Kimataifa wa kusaidia kutatua mgogoro wa muda mrefu kati ya
Palestina na Israel uliopangwa kufanyika tarehe 22 Februari, 2017
Jijini Tehran jambo ambalo pia aliahidi kulitolea majibu hivi karibuni.
Akizungumzia
namna ya kuimarisha mahusiano ya Mabunge haya mawili, Mhe. Ndugai
alisisitiza umuhimu wa kuanzisha Chama Rafiki cha Kibunge (Parliamentary
Friendship Group) baina ya Bunge la Tanzania na Bunge la Iran kwa kuwa
kitasaidia sana Wabunge wa Mabunge yote mawili kubadilishana uzoefu na
kuimaisha uhusiano uliodumu kwa muda mrefu baina ya Tanzania na Iran.
Kwa
upande wa Mhe. Mohammad Dehghani aliipongeza Tanzania kwa kuendelea
kuimarisha demokrasia ambayo kwa kiasi kikubwa nchi yake ya Iran imekuwa
ikithamini na kuheshimu misingi imara iliyowekwa na Baba wa Taifa
Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
Nchi yenu
imekuwa na historia kubwa sana ya kimahusiano na Iran, pamoja na mambo
yote napongeza sana jitihada mnazozichukua kuimarisha demokrasia ikiwa
ni pamoja na kuongeza idadi ya Wabunge wanawake Bungeni na nimatumaini
yetu kuwa mtayafikia malengo mliyojiwekea ya kufikia idadi ya 50 kwa 50.
Alisema Bolozi Dehghani
Awali,
akimkaribisha mgeni wake, Mhe. Ndugai alimshukuru Mhe. Balozi kwa
kutenga muda na kusafiri kutoka Jijini Dar es Salaam kuja Dodoma ambapo
pia alitumia nafasi hiyo kumpa pole Mhe. Balozi kwa matukio mawili
makubwa yaliyoikumba nchi ya Iran hivi karibuni.
“Mhe.
Balozi, kabla ya yote kwa niaba ya Bunge la Tanzania natoa pole kwa
msiba mkubwa wa kifo cha Rais wa Nne wa Iran Hayati Akbar Hashemi
Rafsanjani kilichotokea taehe 08 Januari, 2017 na pili ni tukio la
kuanguka kwa jengo kubwa la kibiashara Jijini Tehran lililosababisha
vifo vya watu ishirini (20) na majeruhi zaidi ya 200, tarehe 19 Januari,
2017”. Alisema Mhe. Ndugai
Aidha
Mhe. Ndugai alitumia fursa hiyo pia kumshawishi Mhe. Mohammad Dehghani
kuanza kufikiria kuhamia Dodoma kwani miundombinu ipo na Ardhi inatosha
kabisa kuuwezesha Ubalozi wa Irani kujenga Ofisi na kuendesha shughuli
kutokea Dodoma.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269