.

USHUPAVU NI MSINGI WA KUYAMUDU MAZINGIRA NA KICHOCHEO CHA MAENDELEO. II

Jan 13, 2017

Makala iliyopita tumeona dondoo za malezi ya watoto na vijana wenye mafanikio (How to Raise Successful Kids) kutoka kwa Bill Murphy. Kama tulivyoweza kusoma dondo nne za mwanzo, msingi wa maarifa haya yanaweza kutumiwa hasa na wazazi, walezi na mtu yeyote mwenye ushawishi katika jamii ambae anawajibu wa kucheza nafasi yake ya kizalendo kuwajenga watoto na vijana kuwajibika kwa maendeleo yao binafsi yenye mguso kwa jamii yake na taifa hili katika ujumla wake.
Tuendelee na dondoo zilizobakia…
5. Mwache kila mmoja atatue matatizo lake mwenyewe. (Let others solve their own problems.)
Haimaanishi kuwaachia watoto na vijana wakumbane na mambo magumu yenye kuwakwamisha.Isipokuwa, kuna mengi ya kuwafanya kukua kuifahamu pale unapowapa watoto, vijana au watu unawaongoza wewe kama kiongozi, kujifunza namna ya kutatua matatizo yaliyo ndani ya uwezo wao, na ikitokea wamekwana na kuhitaji msaada, mzazi, mlezi au kiongozi aingilie kati baada ya wahusika kuonesha juhudi kwanza. 
“Watoto na vijana wajue tupo kwa ajili ya kuwasaidia, ila, wape fursa wao wawe sehemu ya kichocheo cha kuona suluhusho la changamoto za maisha”
6. Simama kama rafiki unaemkuza kiakili na si “mwokozi” (Be a mentor not a savior.)
Kuna nyakati jambo bora ambalo linaweza kusababisha kosa kubwa na kuishi na matokeo ya kosa hilo lililofanyika. Makosa wanayofanya watoto na vijana yana athari ndogo ukilinganisha na makosa wanayofanya ukubwani. Hivyo basi, ni bora watoto na vijana kujifunza kutoka katika makosa madogo hasa pale wanapokuwa umri mdogo. Zaidi ya yote, kuruhusu watoto na vijana wawe na maisha ya yenye mfumo wa udhibiti kutokana na kile wanachochagua kufanya ina faida pia. Hii inadhihirisha kuwa kuna nafasi ya kujifunza kutokana na makosa ambayo wamewahi kuyafanya katika makuzi yao hivyo kujifunza pia kwa kuonywa na kuadibiwa pele inapobidi.
7. Jifunze kukubali kushindwa inapotokea. (Learn to embrace failure when it happens)
Imekuwa kama msemo kwa wajasiliamali, pale ambapo kushindwa (kufeli) kunakuwa kichocheo au fursa ya kufanikiwa. Hakuna mtu anaefanikisha jambo kubwa maishani pale anapokuwa hana changamoto ya uwoga wa kushindwa.
Luteni Kamanda Eric anasisitiza "Katika kushindwa, watoto na vijana wanajifunza “kupiga msuli” dhidi ya magumu na kukabili hali ya uwoga. Kwa kupiga picha kuwa na taswira ya kufeli kunavyoweza kutokea, watoto na vijana wanaweza kujaribu kufanya jambo hilihilo kwa namna bora zaidi ili kupata matokeo yanayotarajiwa.”
8. Watie moyo kuthubutu. (Encourage risk-taking)
Kuthubutu na kufeli kuko sambamba. Watu wenye uwoga wa kupoteza kile kidogo walicho nacho, wana uwezekano mkubwa kutofanikisha jambo lolote maishani. 
 Leteni Kamanda Eric anasema “kuwa mtu Yule ambae hukuwahi kuwa, tuna wajibu wa kufanya jambo ambalo hajuwahi kufanya”
9. Ingiza mamlaka yako pale inapolazimu (Assert your authority where it's sensible.)
Leteni kamanda Eric anawataka viongozi, wazazi na walezi wenye nia ya kuongeza uwezo wa ushupavu kwa wale wanaowaongoza, kuwasaidia watoto na vijana kujua, “si kila kuthubutu ni kuzuri.” Kuna nyakati tunahitaji uzoefu na mtu mwenye mamlaka kutuonesha njia nzuri ya kupita. Jambo hili, linaweza kufanyiwa kazi sehemu yoyote ambapo watu wanakua katika mafunzo ya kazi au taaluma ili kuwa na ufanisi kwa yale wanayofanya maishani.
10. Onesha upendo kwa watu unaowajali (Express your love for the people you care about.)
Watu shupavu wanajua kuwa wanachokifanya kina mguso kwa watu na jamii ambayo wao wanaipenda na wanaijali.
Moja ya njia ni kuhimiza namna ya kuonesha hisia zako za upendo kwa watoto na vijana ili wajue moja kwa moja kuwa unawajali, unawapenda na mafunzo wanayoyapata toka kwako ni sehemu bora ya wao kukua na il wawe watu wenye mchango chanya katika mahali pa kazi, jamii na taifa.
Kwa kweli inahitaji kufanyia mazoezi jambo mara kwa mara ili liwe sehemu ya tabia na hatimae kupata mwenendo unaotarajiwa. Kwa kuwajenga watoto, vijana au watu unaowangoza kwa misingi mizuri ya mahusiano, inaweka alama ya uhakika wa mshikamano na kuaminiana kwa misingi ya maadili kutoka kizazi kimoja na kwenda kingine.
Nihitimishe makala ya leo kunukuu mafunzo kutoka kwa mfalme Suleiman. Mfalme huyu kaandika methali nyingi sana katika vitabu vitakatifu na kuna misingi na kanuni kaziweka ambazo zaweza kuwa nguzo ya familia, jamii na taifa katika ujumla wake. Mfalme Suleiman amesema “Mfundishe mtoto katika njia anayotakiwa kwenda, maana hataiacha hata atakapokuwa mzee au mtu mzima.
Dhana ya Mfalme Suleiman inashabihiana kabisa na walimu wengi au makocha wa maendeleo ya watu. Mmoja ya mwalimu wa maendeleo ya watu ni Dk. A. R. Bernard ambae aliwahi kutoa tafsiri ya mafunzo. Dk. Bernard anakazia sana mafunzo kama njia ya kuleta mabadiliko ya kitabia kwa watu na jamii kwa ujumla. Kwa alichokisema Luteni Kamanda Eric na Dk. Bernard tukichanganya vyote tutapata kizazi kipya chenye “akili” za ushupavu wenye lengo la kuchangia maendeleo ya nchi hii kwa kutatua matatizo na kubabili changamoto zilizopo na zitakazokuja.
Dk. Bernard ametafsiri mafunzo (traning) kamakumkuza mtu kupitia maelekezo (instructions), nidhamu (discipline) and na mazoezi ya kile anachoelekezwa (practice).
Tanzania, tuna nafasi ya kuzijenga familia zetu hususani watoto, vijana na wale tunaowaongoza makazini kwa kuwafunda (mentor) katika misingi sahihi ya kizalendo na ushupavu. Tunahitaji Tanzania ya leon na hatimae kesho iwe na watu wenye mtazamo wa kuleta majibu kwa matatizo na changamoto. Mambo haya hayatotokea pasipo sisi kwa pamoja kucheza nafasi zetu kwa kuyasababisha yatokee.
Mungu Ibariki Tanzania. Kwa pamoja tunaweza kujenga vijana shupavu watakao kuwa chachu ya kulijenga Taifa letu.
Fredrick Matuja

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช