.

WAKONGO WATAKA KUSITISHWA UUZWAJI HOLELA WA SILAHA KWA MAKUNDI YA WANAMGAMBO

Jan 17, 2017


Kiongozi mmoja wa mkoa wa Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ametaka kuwepo mapambano ya kukabiliana na wimbi la biashara za silaha kwa makundi ya wanamgambo nchini humo.

Iciba Mboko mmoja wa viongozi wa serikali katika mkoa huo, ameyasema hayo alipokutana na jumuiya za kiraia ambapo ametaka kuwepo ushirikiano wa wananchi katika sekta za utumishi wa umma kwa ajili ya kupambana na tatizo hilo sanjari na kuwataja watu wanaomiliki sihala kinyume cha sheria.Makundi ya waasi nchini humo

Kadhalika Mboko amewataka wananchi kuwataja wamiliki wa maduka ya silaha hizo ambazo zimekuwa zikitumiwa na makundi ya wabeba silaha katika kuvuruga usalama na amani nchini. Akitoa maagizo hayo kwa wakazi wa mji wa Bukavu, makao makuu ya mkoa wa Kivu Kusini, Iciba Mboko ameongeza kuwa, umefika wakati wa raia na viongozi wa serikali kushirikiana ili kurejesha usalama nchini humo.Mateso wanayoyapata raia wa kawaida kufuatia machafuko 

Maeneo ya mashariki na kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yamekuwa yakishuhudia machafuko kwa kipindi cha miaka 20 sasa. Kushindwa jeshi la serikali na kadhalika askari wa kofia ya buluu wa Umoja wa Mataifa kuyatokomeza makundi ya wanamgambo, inatajwa kuwa sababu ya kuendelea wimbi la machafuko hayo.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช