Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Angellah J. Kairuki akizungumza na waandishi wa habari juu ya
safari ya kuhamia Dodoma iliyoanza rasmi leo kwa kuhamisha vifaa vya
ofisi vya kundi la kwanza la watumishi wa ofisi hiyo. Kushoto kwa Waziri
ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais -Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt.
Laurean Ndumbaro na Naibu Katibu Mkuu-Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Susan Mlawi.
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Angellah J. Kairuki akizungumza na watumishi wa ofisi yake juu ya
safari ya kuhamia Dodoma iliyoanza rasmi leo kwa kuhamisha vifaa vya
ofisi vya kundi la kwanza la watumishi wa ofisi hiyo.
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Angellah J. Kairuki na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Dkt. Laurean
Ndumbaro wakiuaga msafara wa magari yaliyobeba vifaa vya ofisi vya kundi
la kwanza la watumishi wa ofisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam
wakielekea Dodoma kwenye makao makuu ya nchi.
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Angellah J. Kairuki, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Dkt. Laurean
Ndumbaro na Naibu Katibu wa Ofisi hiyo Bi. Susan Mlawi wakifuatilia kwa
makini uamishwaji wa vifaa vya Ofisi yao kabala ya kuondoka kwenda
Dodoma leo hii. Picha na Daudi Manongi-MAELEZO.
Na Daudi Manongi-MAELEZO.
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Angellah J. Kairuki amezindua rasmi safari.....
ya awamu ya kwanza kwa kuaga msafara wa magari yaliyobeba vifaa vya Ofisi vya kundi la kwanza la watumishi wa ofisi hiyo kuelekea Dodoma.
ya awamu ya kwanza kwa kuaga msafara wa magari yaliyobeba vifaa vya Ofisi vya kundi la kwanza la watumishi wa ofisi hiyo kuelekea Dodoma.
Akizungumza
katika uzinduzi huo Mhe. Kairuki alisema umefika wakati wafanyakazi wa
Serikali kuanza safari ya kuamia makao makuu Dodoma ili kutimiza ahadi
iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe
Magufuli wakati wa Maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya Mashujaa.
“Kufuatia
agizo la Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Waziri Mkuu kama kiongozi na
mratibu wa shughuli za Serikali alihamia Dodoma Mwezi Septemba
2016, Wizara nyingine zimeendelea na maandalizi ya kutekeleza azma hii ya
serikali, nami leo napenda kutumia fursa hii kuuarifu umma wa
watanzania kuwa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora imekamilisha maandalizi ya kuhamia Dodoma na hivi punde vifaa vya
kundi la kwanza vitaondoka kwenda Dodoma”,Aliongeza Mhe. Kairuki.
Amesema
katika kundi la kwanza jumla ya watumishi 87 watahamia Dodoma na
litahusisha uongozi wa Juu wa Wizara ukiwajumuisha Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Katibu Mkuu na
Naibu Katibu Mkuu na Baadhi ya Wakurugenzi, Wakurugenzi Wasaidizi,
Maafisa Waandamizi na Watumishi wengine.
Katika
hatua nyingine Mh. Kairuki alisema wale wote wanaohitaji kukutana na
Waziri,Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wake wafike katika Ofisi
zilizopo Dodoma na kwa masuala yote yanayohusuu Sera na Sheria za
Utumishi wa Umma na Utawala wa Utumishi wa Umma kwa Ujumla yatatekelezwa
Mjini Dodoma lakini.
Aidha
masuala ya Mishahara,Uendelezaji rasilimali watu,Ukuzaji maadili,Anuai
za jamii,Uchambuzi ushauri na Utendaji kazi na Huduma ya teknolojia ya
habari na mawasiliano yataendelea kushughulikiwa na ofisi ya Dar es
Salaam.
Alisema
Ofisi yake itafunguliwa Rasmi Mjini Dodoma Tarehe 30 Januari 2017 na
itakuwa katika Jengo la College of Humanities and Social Sciences katika
eneo la Chuo Kikuu cha Dodoma kama makao yake ya muda mpaka hapo
itakavyoelezwa vinginevyo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269