.

WAZIRI MWIJAGE APONGEZA KWA UJENZI WA KIWANDA CHA VIGAE

Jan 22, 2017


Waziri Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akiwa na  Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete wakati walipokuwa wakitembea na kukagua maendeleo ya awali ya eneo litakalojengwa kiwanda kikubwa cha kutengeneza vigae "Tiles" lililopo katika Kijiji cha Pingo, Chalinze Mkoani Pwani. 
Waziri Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akiwa na  Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete wakati walipokuwa wakitembea na kukagua maendeleo ya awali ya eneo litakalojengwa kiwanda kikubwa cha kutengeneza vigae "Tiles" lililopo katika Kijiji cha Pingo, Chalinze Mkoani Pwani. 
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete wa Mwisho Kulia akitoa maelekezo kwa Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TwyFord Tanzania Cereramics, Jack Feng.
Waziri Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akiwa na  Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TwyFord Tanzania Cereramics, Jack Feng,wakati walipokuwa wakitembea na kukagua maendeleo ya awali ya eneo litakalojengwa kiwanda kikubwa cha kutengeneza vigae "Tiles" lililopo katika Kijiji cha Pingo, Chalinze Mkoani Pwani. 
Waziri Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akiwa na  Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete (wa tatu kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TwyFord Tanzania Cereramics, Jack Feng (kushoto) wakati walipokuwa wakitembea na kukagua maendeleo ya awali ya eneo litakalojengwa kiwanda kikubwa cha kutengeneza vigae "Tiles" lililopo katika Kijiji cha Pingo, Chalinze Mkoani Pwani. 
 Waziri Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akiwa na  Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete,Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TwyFord Tanzania Cereramics, Jack Feng,wakiwa na timu ya ukaguzi wa eneo litakalojengwa kiwanda kikubwa cha kutengeneza vigae "Tiles" lililopo katika Kijiji cha Pingo, Chalinze Mkoani Pwani. 
 Eneo litakalojengwa kiwanda kikubwa cha kutengeneza vigae "Tiles" lililopo katika Kijiji cha Pingo, Chalinze Mkoani Pwani. Picha na Othman Michuzi

Na.Mwandishi Wetu
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles
Mwijage amepongeza jitihada zinazofanywa na muwekezaji wa kampuni TwyFord
Tanzania Cereramics,kwa ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza vigae
"Tiles" katika Kijiji cha Pingo, Chalinze Mkoani Pwani.

Waziri Mwijage, amesema hayo alipotembelea na
kukagua maendeleo ya awali ya eneo, litakalojengwa kiwanda hicho cha
kutengeneza vigae "Tiles" kitakachotoa ajira kwa watanzania zaidi ya
elfu mbili katika mfumo rasmi,na ajira elfu nne zisizo rasmi.

Waziri Mwijage aliongeza kuwa," bidhaa hizo pia
zitauzwa katika nchi majirani kama Zambia,Malawi, DRC,Rwanda, Burundi,Uganda na
Jamhuri ya watu wa Afrika Kati na kusafirishwa nje ya bara.

Kwa upande Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani
Kikwete, alisema kuwa ujenzi  wa kiwanda
hicho kipo katika hatua ya mwanzo ya Ujenzi na kinataraji kukamilika Mwezi wa
Saba na kufunguliwa Rasmi mwezi wa Nane mwaka huu.

 Ridhiwani
alisema kuwa kiwanda hicho kitasaidia kufungua mji wa Chalinze na kufanya mji wa
viwanda na biashara na hivyo kufungua fursa za kiuchumi na kupanua mji huo,katika
sekta ya viawanda inayosimamia vyema na serikali ya awamu ya tano.

 “ujenzi wa
kiwanda hiki ni Alama Chanya ya jinsi serikali ya awamu ya Tano ilivyojidhatiti
kufungua fursa za viwanda katika Nchi yetu.Wananchi wa Chalinze na Pwani
wameaswa kuendelea kujipanga kwa viwanda na fursa nyingi zaidi.”alisema
ridhiwani

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª