.

MTOTO LATIFA ALIYEIBIWA SAA 2 ASUBUHI IRINGA MJINI APATIKANA USIKU KIJIJI CHA MKUNGUGU

Feb 28, 2017

 Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela akiwa amembeba mtoto huyo.
Jana mida ya saa 2 asubuhi katika maeneo ya Stand kuu ya mabasi aliibiwa mtoto mchanga mweneye umri wa miezi 5. Mtoto huyo aliibiwa na binti ambaye alikuwa amekuja kutafuta kazi.

Akieleza tukio hilo Mama yake Bi Asha Shaban Lauza alisema ” nikiwa naosha vyombo binti huyu ambaye toka jana alikuwa anatafuta kazi alianza kumpa maziwa mtoto yaliyo kwenye chupa mpaka mtoto akamaliza , baadae mtoto akajinyea basi bila wasiwasi nikampa shilingi elfu kumi ili akanunue pampasi duka la pili tu akanyanyuka na mtoto kwenda dukani toaka asubuhi mpaka sasa usiku hatuja muona” .

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh, Richard Kasesela alifika eneo la tukio baada ya kumhoji mzazi akagundua walichelewa kutoa taarifa polisi. Baada ya msako muda was saa 3 usiku mtoto alipatikana eneo la Mkungugu km 33 kutoka Iringa Mjini.

Binti wa miaka 14 (Jina linahifadhiwa) alikuwa akitoroka na mtoto huyo gari la polisi la doria likishirikiana na wananchi wa kijiji cha Mkungugu lilifanikiwa kumuweka chini ya ulinzi mwizi huyo wa mtoto. Mkuu wa Wilaya alifika akiongozana na mama Mzazi wa mtoto pamoja na Diwani wa kata ya Kisinga Mh, Ritha Mlagala.

Binti mwizi yupo kituo cha polisi akiendelea kuhojiwa na mama mzazi baada ya kuandika maelezo alipewa fomu ya matibabu na kumpeleka mtoto hospitali.

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh, Richard Kasesela amekemea vikali kitendo cha uzembe wa mama huyu na wazazi kwa ujumla “pamoja na mama huyu kuwa na uchungu wa mtoto bado ana mashtaka ya kujibu ya uzembe, watu tusio wajua tusiwape watoto wetu hata kidogo huu ni uzembe wa hali ya juu” alisisitiza

Mkuu wa wilaya. Pichani anaonekana mtoto Latifa akiwa ambebwa na Mkuu wa wilaya walipofika kituo cha polisi. Picha zingine ni za eneo la kijiji cha Mkungugu barabani alipokamatwa binti mwizi akiwa na mtoto usiku wa saa 3.

TFDA YATOA UFAFANUZI KUHUSU UVUMI WA DAWA AINA YA P-500 (PARACETAMOL)

MAJALIWA ASISITIZA MASHIRIKA YA UMMA KUSHIRIKIANA ILI KULETA MAENDELEO

Image result for majaliwa
Na Daudi Manongi-MAELEZO
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amewataka wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Mashirika ya Umma na Mamlaka za udhibiti kuwa wabunifu na kutumia fursa na rasilimali zilizopo nchini ili kuleta maendeleo chanya.
Amebainisha hayo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa kujadili nafasi ya Mashirika ya Umma katika utekelezaji wa mpango wa pili wa Taifa wa maendeleo wa miaka mitano.
“Rai yangu leo ni kwamba kwenye majadiliano yenu pendekezeni na kufanya mashirika ya umma yawe endelevu,yapanuke zaidi na kuliongezea Taifa mapato na ndio maana nafarijika sana kuona mkutano huu unajumuisha wadau wote muhimu ili pamoja na kuweka mikakati ya namna mashirika ya umma ya Tanzania yanavyoweza kushiriki kwenye utekelezaji wa mpango wa Maendeleo,”Alisema Majaliwa.
Akielezea hali ya mashirika ya umma nchini,Waziri Mkuu amesema kuwa utegemezi wa mashirika unaendelea kupungua na mchango na gawio kutoka kwenye mashirika hayo unaendelea kuongezeka na kuhimiza kuongezeka kwa ubunifu na matumizi mazuri ya rasilimali chache zilizopo na kuongeza kati ya mashirika 65 ya kibiashara,mashirika 8 yanaendeshwa kwa Ruzuku ya Serikali,wakati mashirika 57 hayategemei ruzuku ya Serikali.
Ameagiza kuboreshwa kwa mwongozo wa kupata wajumbe wa Bodi na kuwaagiza kuweka mwongozo rasmi wa namna ya kupata wajumbe hawa kwani ni sehemu inayolalalmikiwa sana na wananchi.
Amesema kuwa wameyashirikisha mashirika ya umma kwenye utekelezaji wa mpango wa maendeleo kwa sababu vipaumbele vya mpango wa pili wa maendeleo wa Taifa wa miaka mitano ambayo ni ujenzi wa viwanda vya kuimarisha kasi ya ukuaji wa uchumi,miradi mikubwa ya kielelezo na miradi wezeshi kwa maendeleo ya viwanda ikiwemo barabara,reli,nishati,bandari maji na mawasiliano.
Aidha ameagiza kuondolewa kwa urasimu katika shughuli za mashirika ya umma kwani unakwamisha uboreshaji na maendeleo ya mashirika ya umma.
Waziri Mkuu pia ametoa rai kwa viongozi wote wa mashirika ya umma kutosaini mikataba isiyo na tija kwa Taifa ambayo inapelekea kupata hasara kubwa na kuhimiza mashirika haya kushirikiana na mashirika ya nje pamoja na sekta binafsi ili kupata nguvu ya pamoja katika kukuza uchumi.
“Ni lazima mashirika ya umma yakafanya kazi kwa pamoja na kwa kushirikiana ikiwemo kubadilishana mbinu na utaalamu ili kulifikisha Taifa hili katika azma yake ya kukuza Uchumi wa viwanda kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi yetu”,Alisisitiza Mh.Majaliwa.

WAZIRI DK.CHARLES TIZEBA KUFUNGUA KONGAMANO LA WADAU WA KILIMO JIJINI DAR ES SALAAM KESHO

Enles Mbegalo
WAZIRI wa Kilimo ,Chakula,Mifugo na Uvuvi Dk. Charles Tizeba (pichani), anatarajia kufungua kongamano la siku  tatu la wadau wa sera za kilimo kesho jijini Dar es Salaam.
 Aidha, kongamano hilo litahudhuriwa na wadau zaidi ya 200 kutoka nchi mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam , Mwenyekiti wa  Kampuni ya Agricultural Non State Actors Forum (ANSAF), Audax Rukonge, alisema serikali imekusudia kuweka kipaumbele kwenye viwanda vya uchakataji wa mazao ya kilimo.
Kongamano hilo litalenga kuongeza uelewa miongoni mwa watunga sera kuhusu mchango wa kilimo katika kuhamasisha ukuaji wa viwanda Tanzani.

“Wadau  watajadili kupata tafsiri halisi ya sekta ya uchakataji mazao ya kilimo katika muktadha wa mageuzi ya viwanda Tanzania,”alisema
Rukonge alisema kongamano hilo limedhaminiwa na USAID, Benki ya Dunia,ANSAF,JICA na wadau wengine ambao wamesaidia kuleta watalamu wakiwamo wakulima, watafiti,wafanyabiashara na watunga sera.

Mratibu wa Jukwaa la Sera ya Kilimo na Mchumi mwandamizi Wizara ya Kilimo, Sophia Mlote alisema kongamano hilo la tatu litajadili maendeleo ya kilimo nchini ikiwamo kujadili namna ya kutetea sera,sheria,kanuni.
Pia alisema kongamano hilo litajikita katika kujadili juu ya mpango wa kilimo cha mihogo,mikunde, samaki, mazao, usafirishaji pamoja na vifungashio kwa kuwa wazalishaji wengi hawana vifungashio.

AZANIA GROUP KUWAKILISHA TANZANIA KATIKA MASHINDANO YA A.MASHARIKI YA STANDARD CHARTERED

  Timu ya Azania Group, ndiyo itakayowakilisha Tanzania katika mashindano ya kikanda ya Afrika Mashariki, ya Benki ya “Standard Chartered-Road to Anfield” yatakaofanyika uwanja wa Jakaya Kikwete Youth Park Jumamosi, Machi 4. Azania walipata ushindi huo kwa kuichakaza timu ya H&R Consultancy mabao ya 6-5 kwa penati dhidi ya mchezo wa kukata na shoka uliofanyika mwishoni mwa wiki na kufanikiwa kuipeperusha bendera ya Tanzania. Kwa maana hiyo, Azania Group wanatarajia kumenyana uso kwa uso na washindi wa michuano hiyo kutoka nchi za Kenya na Uganda. Washindi wa michuano hiyo nchini Uganda ni timu ya Cocacola wakati kidedea wa kombe hilo nchini Kenya ni Radio ya Capital FM.
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Tanzania Sanjay Rughani (kushoto) na Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki hiyo, Juanita Mramba wakikabidhi kikombe kwa Bw Sikaba Hamisi ambaye ni Nahodha wa timu Azania Group, Mshindi wa kitaifa wa mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 (Road to Anfield), mashindano yaliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya JK Youth Park, Gerezani jijini Dar es Salaam.
Akiongea na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kutwaa ushindi huo, Nahodha wa Azania Group, Bw. Shabaka Hamisi alisema maandalizi yao mazuri ndiyo siri ya ushindi wao na kuongeza kwamba wapo tayari kuwanyoa hao wageni asubuhi kabisa. “Katika jambo lolote kama unataka kufanya vyema, maandalizi mazuri yanasaidia sana. Kwa upande wetu, tulifanya mazoezi yakutosha na ndiyo maana leo tumeibuka washindi.” Alisema. Aliongeza, “Siyo kwamba wenzetu walikua wabovu, ila umakini na utulivu kwa upande wa wachezaji wangu ndiyo kilichotusababishia kupata matokeo mazuri.” Alisema mazoezi ya kujipanga kwa ajili ya mechi tayari yameshaanza kwa ari na nguvu mpya, akiongeza kuwa ushindi kwao ni lazima. Kwa upande wake, Phillip David, nahodha wa H&R Consultancy alisema kukosekana kwa ukosefu wa umakini katika ushambuliaji ndiyo uliosababisha timu yake kupoteza mechi hiyo, hata hivyo alishukuru kwa kuibuka mshindi wa pili wa mashindano hayo.
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Tanzania Sanjay Rughani (kushoto) na Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki hiyo, Juanita Mramba (kulia) wakifurahi katika picha ya pamoja na timu ya Azania Group wakikabidhi kikombe kwa timu Azania Group,Mshindi wa kitaifa wa mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017(Road to Anfield), mashindano yaliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya JK Youth Park,Gerezani jijini Dar es Salaam.
“Kama ulivyoona, mechi ilikuwa moja moja hadi tukaingia kwenye matuta. Wenzetu walipata penati sita wakati sisi tulifunga tano. Nafasi ya kushinda ilikuwa upande wetu lakini Mungu hakupenda iwe ivyo,” alisema. Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania Limited, Sanjay Rughani aliwaasa wachezaji wa Azania Group kuwa wajiandae kikamilifu ili waubakishe ubingwa nchini Tanzania. “Sisi hakuna zawadi nzuri ambayo tunaitaka kutoka kwenu zaidi ushindi. Fanyeni mazoezi ya kutosha ili Jumamosi inayokuja muweze kushinda mechi zenu zote dhidi ya hizo timu kutoka Kenya na Uganda. Na sisi kama wadhamini tutakua pamoja nanyi ili kuhakikisha kwamba mnapata ushindi hapa nyumbani,” alisema Sanjay. Naye Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Benki hiyo, Juanita Mramba, aliwapongeza kwa ushindi huo lakini akiwatahadharisha kuwa safari yao ndiyo kwanza imeanza. “Leo mmeshinda mashindano haya, Jumamosi kazi yenu ni kubwa zaidi kwani mtacheza na wageni wawili, hivyo jipangeni vizuri zaidi mkiutumia vyema uwanja wa nyumbani,” alisema. Ukiachia mbali Azania ambao waliondoka na kombe za dhahabu, washindi wa pili H&R Consultancy walijitwalia kombe la shaba, huku washindi wa tatu PWC wakitwaa kombe la Bronze.
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Tanzania Sanjay Rughani (kushoto) akikabidhi kombe kwa Nahodha wa timu ya HR Consultants, Phillip David ambao ni washindi wa pili wa mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 (Road to Anfield), yaliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya JK Youth Park, Gerezani jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia tukio hilo ni Mkuu wa Wateja Binafsi wa Benki ya Standard Chartered, Michael Shio (kulia).

ZAIDI YA SHILINGI MILIONI NNE ZAPATIKANA KWENYE HARAMBEE ILIFANYWA NA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA ILEJE

 Mkurugenzi wa halmashauri ya Ileje Haji Mnasi akiwa kwenye harambee ya uchangiaji wa vifaa vya ujenzi wa zahanati ya ushirika wa Rungwa iliyopo katika wilya ya Ileje.
 Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi  alihesabu kiasia cha shilingi milioni nne na zaidi kwa lengo la ufanikishaji wa upatikanaji wa vifaa vya kumalizia ujenzi wa zahanati ya ushirika wa Rungwa.


Na fredy Mgunda.

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi afanikisha azima ya ujenzi wa zahanati bora katika ushirika wa rungwa kwa lengo la kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa wilaya ya Ileje.


Akizungumuza wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa zahanati hiyo  mkurugenzi Mnasi alisema kuwa wameamua kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuboresha hutuma za afya kwa wananchi ili wafanye kazi kwa kujituma.

“Kauli mbiu ya Rais wetu ni hapa kazi tu sasa ukiwa na jamii ambayo dhohofu huwezi kufikia malengo ya hapa kazi hivyo nimefanya harambee hii kumuunga mkono Rais kwa kuboresha huduma za afya katika wilaya yetu ya Ileje na kuwafanya wananchi kufanya kazi kwa kujituma huku wakiwa na afya njema na kuendelea kulijenga taifa kwa kufanya kazi kwa kujituma”.alisema Mnasi

Mnasi alisema wananchi wanatakiwa kujitoalea kwa hali na mali kufanikisha ujenzi wa zahati hiyo unakamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa jamii.

“Leo hii tumefanya harambee ya kuchangia kupatikana kwa vifaa vya kumalizia ujenzi wa zahanati unaogharimu kiasi cha shilingi milioni sita na nashukuru mungu nimefanikiwa zaidi  kupata shilingi milionii nne  hivyo lengo limetimia kilicho baki ni utekelezaji tu labda niwaombe kuzitumia pesa hizi vizuri kununua vifaa ya ujenzi ili wananchi waanze kupata huduma bora”. Alisema Mnasi

Aidha Mnasi alizitaka taasisi nyingine kuiga mfano wa ushirika wa Rungwa kwa ujenzi wa zahanati hiyo ambayo itarahisisha uwepo wa huduma bora kwa jamii husika.

“Tuna taasisi nyingi sana katika wilaya yetu hivyo naziomba nazo zijitahidi kuwa na malengo ya ujenzi wa zahanati ili kuendeleza kutoa huduma bora kwa jamii na kuifanya jamii kuwa huru kufanya kazi kwa nguvu huku wakiwa na afya bora”.alisema Mnasi

Nao baadhi ya waumini wa ushirika wa Rungwa walimushukuru Mkurugenzi huyo kwa kuendelea kujituma kufanya kazi kwa wananchi wa chini na kuwaboresha huduma za afya.

“Tulikuwa tunahitaji zaidi ya milioni sita lakini uwepo wa mkurugenzi Mnasi katika harambee ya leo kumesaidia kupata pesa nyingi ambazo zimefanisha azma ya umaliziaji wa ujenzi wa zahanati yetu”.walisema washirika

MAGAZETI YA LEO TANZANIA NA NJE FEB 28,2017

RC MRISHO GAMBO ATEMBELEA NYUMBANI KWA HAYATI EDWARD SOKOINE

Feb 27, 2017

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo wikiendi hii alipata nafasi ya kutembelea nyumbani kwa aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani Hayati Edward Moringe Sokoine huko Monduli juu Wilayani Monduli. 

Mh.Gambo alipata wasaaa wa kuzungumza na wajane wa kiongozi huyo mkubwa wa Kitaifa aliyefariki kwa ajali ya gari mwaka 1984 eneo la Dumila huko Mkoani Morogoro, Mkuu wa mkoa alipata wasaa wakuzungumza na familia hiyo pamoja na wakazi majirani wanaozunguka familia hiyo na kusema maneno machache ambapo Alisema 

"Kutembelea maeneo haya ambapo zipo kumbukumbu za mashujaa wetu waliolipigania Taifa letu kwa uzalendo mkuu, inatusaidia sisi viongozi vijana kuzirudia hadhiri zetu za uongozi ili tuweze kuwatumikia wananchi wanyonge kwa Uadilifu na uwajibikaji,ili kuacha alama katika nafasi tulizopewa na kuwatumikia wananchi kama walivyofanya wazee wetu hawa." 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo,Akisalimiana na Mjane wa Hayati Sokoine.
Kutoka Kulia ni Diwani wa Monduli juu akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli na pia ni Diwani wa Monduli Mjini Mh:Issack Joseph,akisalimiana na Mjane wa Hayati Sokoine .
Mh: Gambo akiwa ameambatana na Mjane wa Sokoine Pamoja na watumishi mbalimbali wa Serikali,Wakitoa Heshima kwenye kaburi la Hayati Sokoine.  
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mh: Mrisho Gambo akipanda mti wa kumbukumbu nyumbani kwa Hayati Sokoine.Picha na Msumbanews.com
ยช