.

ADAM BARROW AAPISHWA URAIS NCHINI GAMBIA

Feb 18, 2017

Rais mpya wa Gambia Adama Barrow, leo atatawazwa nchini humo huku taifa hilo likisheherekea kuondoka kwa rais wa zamani Yahya Jammeh. Viongozi wa mataifa kadhaa watahudhuria sherehe hizo. Barrow aliapishwa kama rais mpya wa Gambia mwezi uliopita katika ubalozi wa Gambia wa nchi jirani ya Senegal, wakati Jammeh alipogoma kuondoka madarakani licha ya kushindwa katika uchaguzi mkuu. Shinikizo la kimataifa lililotishia kuingilia kati mvutano huo wa kisiasa kwa kutumia nguvu ya jeshi lilimlazimisha Jammeh kukubali kushindwa na kukimbialia uhamishoni. Barrow ameahidi kurekebisha matendo maovu aliyoyafanya Jammeh wakati wa uongozi wake, ikiwa ni pamoja na kudumisha uwanachama wa Gambia katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC, pamoja na kuirejesha nchi hiyo katika Jumuiya ya Madola - Commonwealth.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช