.

HOSNI MUBARAK: VISIWA VYA TIRAN NA SANAFIR NI VYA MISRI

Feb 14, 2017

Dikteta aliyepinduliwa madarakani huko Misri amesisitiza kuwa visiwa vya Tiran na Sanafir ni milki ya nchi hiyo.

Hosni Mubarak Rais wa zamani wa Misri aliyepinduliwa madarakani amesisitiza katika ujumbe wa sauti akiwahutubu wananchi katika kumbukumbu ya kutimia mwaka wa sita tangu apinduliwe madarakani nchini humo kuwa kwa mujibu wa hukumu iliyotolewa na mahakama ya nchi hiyo visiwa viwili vya Tiran na Sanafir ni mali ya Misri.

Saudi Arabia na Misri zinahitilafiana kuhusu umiliki wa visiwa hivyo viwili vilivyopo kaskazini mwa bahari Nyekundu.

Visiwa vya Tiran na Sanafir ambavyo ni milki ya Misri 
Itakumbukwa kuwa Cairo mwaka iliafiki kuipatia Saudi Arabia visiwa hivyo viwili kufuatika makubaliano yaliyofikiwa kati ya nchi mbili hizo; na mkabala na hatua hiyo; Wasaudia pia wanapaswa kuwekeza katika uchumi wa Misri, hata hivyo mapatano  hayo yalibatilishwa na mahakama ya Misri.

Wananchi wa Misri wamekuwa wakiandamana pakubwa katika mji mkuu Cairo na katika maeneo mengine ya nchi  kulalamikia hatua hiyo ya serikali ya kuipatia Saudia visiwa vyao. Watu zaidi ya 200 wametiwa mbaroni na wengine kadhaa kuhukumiwa vifungo jela kwa kosa la kushiriki katika maandamano hayo.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช