Breaking News

Your Ad Spot

Feb 15, 2017

MAMA MAGUFULI NA MAMA MAJALIWA WATEMBELEA GEREZA LA MAHABUSU LA TABORA, WATOA ZAWADI KWA WAFUNGWA

MKE wa Rais Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wametembelea Gereza la Mahabusu Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu gerezani hapo. 

Wake wa viongozi wametembelea gereza hilo jana ( Februari 14, 2017) wakiwa katika ziara mkoani Tabora, ambapo Mama Janeth amesema wameamua kuwatembelea wafungwa na mahabusu hao kwa nia ya kuwafariji kwa kuwa wao ni sehemu ya jamii. 

“Vitabu vitakatifu vinasema kwamba ukiwasaidia watu wenye mahitaji utakuwa umetoa sadaka kubwa kwa Mwenyezi Mungu, hivyo tumeamua kuja kutembelea wafungwa na mahabusi kwenye gereza hili na kuwapa zawadi kwa kuwa nanyi mnahitaji faraja,” amesema. 

Amesema wameamua kwenda kuwaona wafungwa na mahabusu hao kwa lengo la kuwafariji na kuwatia moyo kwa sababu wanaimani kwamba wakitoka watakuwa raia wema na hayo wanayopitia ni sehemu ya kufanya marekebisho ya tabia. 

“Ni siku kubwa kwangu, nimejifunza mengi baada ya kufika hapa. Kitendo cha kwenda kuwaona wenye mahitaji wakiwemo wagonjwa, wafungwa ni jambo jema tunaamini hizi zawadi tulizozitoa zitawasaidia kwa sababu tunajua mnamahitaji mengi,” amesema. 

Katika gereza hilo wake hao wa viongozi wamekabidhi zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu, ambapo mwakilishi wa wafungwa hao Deo Kitave aliwashukuru kwa niaba ya wenzake. “Tunawashukuru kwa kutukumbuka, tunamuomba Mwenyezi Mungu muendelee kuwa na moyo huo,”. 
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipokea risala toka kwa Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tabora Mkuu wa gereza SSP Nahman Koko wakati yeye na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa walipotembelea Magereza ya mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa mahabusu.

 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimkabidhi zawadi  Naibu Mkuu wa gereza la Mahabusu Tabora Mrakibu wa Magereza Godliver Makwaruzi  wakati yeye na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa walipotembelea Magereza ya mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu jana Februari 14, 2017.
 Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa zawadi  Naibu Mkuu wa gereza la Mahabusu Tabora Mrakibu wa Magereza Godliver Makwaruzi  wakati yeye na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa walipotembelea Magereza ya mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu
 Mke wa Rais Mama Janeth magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakitoka katika gereza la wanawake Tabora walipotembelea Magereza ya mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu
 Mke wa Rais Mama Janeth magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwanri akiwashukuru sana kutembelea Magereza ya mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu

 Mke wa Rais Mama Janeth magufuli akiongea wakati yeye na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa  walipotembelea Magereza ya mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu
 Mke wa Rais Mama Janeth magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakitoa zawadi kwa ajili ya wafungwa na mahabusu walipotembelea Magereza ya mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu
Mke wa Rais Mama Janeth magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakiagana na askari magereza bada ya kutembelea Magereza ya mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu (PICHA NA IKULU)

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages