Breaking News

Your Ad Spot

Feb 8, 2017

MFUMUKO WA BEI WA MWEZI JANUARI 2017 UMEONGEZEKA KWA ASILIMIA 0.8

Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa kuhusu mfumuko wa bei wa mwezi Januari 2017 jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Meneja Idara ya Takwimu za Ajira na Bei, Ruth Minja.
Waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.
Wanahabari wakiwa kazini.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale

MFUMUKO wa Bei wa mwezi Januari 2017 unaopimwa kwa kipimo cha mwezi umeongezeka kwa asilimia 0.8 ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 0.7 ilivyokuwa mwezi Desemba 2016.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakati akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

"Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 105.92 mwezi Januari 2017 kutoka 1-05.04 mwezi Desemba 2016" alisema Kwesigabo.

Alisema kuongeza kwa fahirisi za bei kumechangiwa na kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula.

Alitaja baadhi za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi ni pamoja na mahindi kwa asilimia 6.3, ndizi za kupika kwa asilimia 5.8, magimbi kwa asilimia 5.3 na viazi vitamu kwa asilimia 6.5.

Alisema kwa upande mwingine baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilichochangia kuongezeka kwa fahirisi ni pamoja na mkaa kwa asilimia 3.2 na majokofu kwa asilimia 2.4.

Kwesigabo alisema thamani ya shilingi ya Tanzania hupima badiliko la uwezo wa shilingi ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma zilezile za mlaji ambazo shilingi ya Tanzania ingeweza kununua katikavipindi tofauti.

"Ikiwa fahirisi za bei za Taifa zinaongezeka, uwezo wa shilingi ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma hupungua" alisema Kwesigabo.

Alisema uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia shilingi 94 na senti 42 mwezi Januari, 2017 ikilinganisha na shilingi 95 na senti 20 ilivyokuewa mwezi Desemba 2016.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages