.

RAIS DK. MAGUFULI AMJULIA HALI NYUMBANI KWAKE,WAZIRI MKUU WA ZAMANAI CLEOPA MSUYA

Feb 18, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsalimia Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya, alipofika kumjulia hali, nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam, leo. Msuya alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako alikuwa akipatiwa matibabu mpaka aliporuhusiwa kurejea nyumbani kwake mara baada ya kupata nafuu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akimuombea Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya mara baada ya kumaliza mazungumzo yao nyumbani kwa Msuya, Upanga jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akimuombea Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya mara baada ya kumaliza mazungumzo yao nyumbani kwa Msuya, Upanga jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya mara baada ya kumjulia hali nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam.PICHA NA IKULU

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช